• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

KAILIMA ATAKA KUTATULIWA KWA CHANGAMOTO YA UPELELEZI KUCHELEWA


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhani Kailima ameitaka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kushughulikia mambo muhimu sita ili kuboresha utendaji kazi na kutatua changamoto za uratibu wa Upelelezi.



Akizungumza katika hafla ya Ufunguzi wa mafunzo juu ya Makosa ya Mtandao, Uchunguzi na mbinu za Mashtaka Naibu Katibu Mkuu Kailima ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka Waendesha Mashtaka wa Serikali kutumia Mamlaka waliyopewa kisheria kutatua changamoto mbalimbali za kiutendaji. 

Katika hotuba yake Bw. Kailima    aliyataja mambo sita ambayo angependa yashughulikiwe.

Jambo la kwanza alilohitaji lishughulikiwe ni kuwepo kwa changamoto ya upelelezi kuchukua muda mrefu hivyo alitaka eneo hili lifanyiwe kazi kwa kuhakikisha upelelezi unaratibiwa vizuri na kwa haraka.

Eneo la pili Bw. Kailima aliomba Waendesha  Mashtaka kushirikiana na Jeshi la Polisi ili  kutatua changamoto za ucheleweshaji mafaili.

Tatu alitaka Waendesha Mashtaka kukataa rushwa wanapotekeleza majukumu yao kwakuwa rushwa ni adui wa haki.

Nne aliwashauri kutimiza wajibu wao ipasavyo kwakuwa majukumu yao yanaakisi utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Mashtaka.

"Ukitembea, ukiongea, ukifanya kazi uonekane kama DPP kwakuwa huna namna ya kutenganisha majukumu yako na DPP". Alisema Naibu Katibu Mkuu Kailima.

Jambo la tano Naibu Katibu Mkuu Kailima alisisitiza umuhimu wa kuwa waadilifu kwa kuhakikisha kila jambo wanalolitenda kulifanya kwa uadilifu mkubwa.

Na jambo la sita aliwataka Waendesha Mashtaka kuendelea kutunza siri za Serikali.

Akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu aliwataka Mawakili wa Serikali kuyatumia mafunzo hayo kikamilifu na kuboresha utendaji wao wa kazi.

Alisema ukuaji wa teknolojia huja na mambo mema lakini pia huambatana na changamoto hivyo mafunzo yaliyotolewa yatawaongezea weledi wa kupambana na uhalifu.


Bw. Mwakitalu alisema baadaye ofisi itawapima kutokana na utendaji wao wa kazi baada ya mafunzo.

Naye Wakili wa Serikali Mkuu Bi. Veronica Matikila  alisema Makosa ya Mtandao yanaangukia katika Makosa ya kupangwa ambapo alieleza kuwa mafunzo wanayopatiwa Waendesha Mashtaka wa Serikali yanalenga kuwajengea ufahamu wa namna bora ya kuratibu upelelezi wa Makosa ya Mtandao na Makosa yanayoendana na hayo.


Naye Wakili wa Serikali Bi. Prosista Minja kutoka Songwe kwa niaba ya Washiriki wengine alimshukuru mgeni rasmi kwa kuwafungulia mafunzo na alishukuru Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kuwaandalia mafunzo ambapo aliahidi kwa niaba ya wenzake kuyatumia mafunzo kuboresha utendaji kazi.

Share:

MKUU WA MKOA AMEWATAKA WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI KUFANYA KAZI KWA WELEDI

 Mkuu Wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Mhandisi Robert Gabriel aliwataka Waendesha Mashtaka na Wapelelezi kufanya kazi kwa weledi   na ubunifu katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

Akifunga mafunzo kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi kutoka katika Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini yaliyofanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 28 Februari hadi 4 Machi,2022  yaliyohusu taratibu za Kisheria ya Utaifishaji Mali na Makubaliano ya Kukiri Makosa alisema elimu na ujuzi watakayoipata yatawasaidia  kutekekeza kwa ukamilifu majukumu yao na kupunguza msongamano wa mahabusu mahakamani.



Alisema wahalifu wanatumia mbinu mbalimbali katika kufanya Uhalifu hivyo kushiriki kwenye mafunzo ni muhimu ili kuendana na mbinu mpya za kupambana na Uhalifu.

"Nalinganisha tukio hili la mafunzo  na kazi mkata kuni ambapo ili kuweza kukata kuni vizuri ni vizuri kulinoa shoka".

Aliyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Akizunguza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu aliwashukuru Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa ambao walikuwa ni Sehemu ya Wakufunzi kwa kukubali kufika kutoa mada licha ya majukumu makubwa waliyonayo wakati huu wa kuanza kwa Mwaka Mpya wa Mahakama.

Aliwataka washiriki wa mafunzo kuonyesha matokeo ya mafunzo waliyopewa kuleta matokeo na mabadiliko yenye tija katika utendaji wao  wa kazi.



Naye Mwakilishi kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la PAMS Bw. Samson Kassala aliwapongeza washiriki kwa moyo wa kujitoa na kuzingatia mafunzo waliyopewa ambapo aliahidi Shirika la PAMS kuendelea kuiunga mkono Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  kwa kudhamini shughuli mbalimbali na kuliletea taifa Tija.



Naye Bw.Paul Kadushi ambaye ni Mkurugenzi wa Divisheni ya Utaifishaji Mali, Makosa ya Kupangwa na Uhalifu Mahsusi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka


 alisema Malengo makuu ya mafunzo ni kuwajengea uwezo Waendesha Mashtaka na Wapelelezi katika kuboresha utendaji wa kazi.

Share:

MFUMO UTASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA KIUTENDAJI - DPP

 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amesema kuwepo kwa mfumo wa kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kutasaidia kutatua changamoto nyingi za kiutendaji na hii ni kulingana na kuwepo kwa idadi kubwa ya mrundikano wa kesi katika Mahakama tangu mwaka 2000 kesi nyingi zinakuwa upelelezi wake bado haujakamilika.

"Tumekuwa na changamoto ya kupata taarifa za takwimu sahihi ya shughuli tunazozifanya hususani katika kujua idadi sahihi ya kesi zilizoendeshwa na kuisha mahakamani"



Amezungumza hayo Mkurugenzi wa Mashtaka wakati akifungua Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya kesi kwa Waendesha Mashtaka wa Polisi, Mawakili wa Serikali, Makatibu Sheria pamoja na Watumishi wengine wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yaliyoanza  tarehe 28 Februari, 2022 na kumalizika tarehe 29 Machi, 2022 Jijini Dar es Salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)

Aidha, Mkurugenzi Mwakitalu alieleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani yatasaidia katika ukusanyaji, uchakataji na utoaji wa taarifa mbalimbali za majukumu  ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.



Mkurugenzi Mwakitalu alitoa shukrani zake kwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  kwa ufadhili wa kuwezesha mafunzo hayo. Na pia aliwashukuru wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Kitengo cha TEHAMA pamoja na wataalamu kutoka  Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kutengeneza mfumo huu mzuri na kueleza kuwa mfumo huu ungeweza kununuliwa kwa gharama kubwa sana lakini wataalamu kutoka ndani wameweza kufanikisha hili.

Pia Mkurugenzi alitoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kuweka nguvu zaidi kujifunza kwa bidii ili wanaporejea katika vituo vyao vya kazi wakaanze kuutumia mfumo huo vizuri kwani utawasaidia katika utatuaji wa changamoto nyingi za kiutendaji. Na pia endapo kutakuwa na changamoto nyingine zitatokea wakati


 wakitumia mfumo huo basi wasisite kutoa taarifa kwa wakati.

Share:

UPELELEZI MZURI NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTOAJI HUKUMU YA HAKI - DPP


Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester  Mwakitalu amesema Upelelezi mzuri ni nguzo muhimu katika kuhakikisha kuwa hukumu inatolewa vizuri na kwamba usipofanyika vizuri wahalifu hawataweza kupatikana.

“ Upelelezi usipofanyika vizuri hakuna namna Mwendesha Mashtaka ataendesha kesi vizuri. Uchunguzi na upelelezi wa mali lazima ufanyike vizuri ili kupelekea mashtaka kuandaliwa vizuri  ili mhalifu asinufanike  kwa mali alizozipata kwa njia ya uhalifu.Mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu zitafutwe, zifuatiliwe na zitaifishwe ili kuhakikisha kuwa uhalifu unakomeshwa na kuwapa taarifa wahalifu kuwa uhalifu haulipi. Alisisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka.

                                                                                   


Bw. Mwakitalu alisema  Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yanawarahisishia Wahalifu kufanya uhalifu, kuficha na kuzitakatisha  kutokana na uhalifu kufanyika katika mifumo ya  kiektroniki hivyo inabidi kutobaki nyuma na kuhakikisha Waendesha Mashtaka na Wapelelezi wanajengewa uwezo ili waweze kudhibiti uhalifu.

Alisema ni matarajio yake kuwa mafunzo wanayoyapata yanatarajiwa kuwa na matokeo bora na kuboresha utendaji kazi. “ kufundisha watu sabini na tano tu siyo jambo kubwa ila ninachotaka kukipata baada ya mafunzo haya ni kuona maboresho yakitokea katika utendaji kazi na kuona namna uendeshaji wa mashtaka unavyobadilika na kuendeshwa kwa weledi na  kuhakikisha kuwa majalada yanayofikishwa mahakamani yanakuwa na ushahidi unaojitosheleza kwa kuwa na mashtaka kamili badala ya kuwa na ushahidi wa kuungaunga.

                                                                                     


 

Alisema kumekuwa na changamoto na kelele nyingi na  manung’uniko juu ya taratibu za Makubaliano ya Kukiri Kosa( Plea-Bargaining) kwa kuwa ni utaratibu mpya lakini ni  mzuri ambao ukitumika vema utasaidia kupunguza msongamano wa mahabusu na wafungwa hivyo alisema mafunzo yanayotolewa yatawezesha kuboreshwa kwa utaratibu huo.

“ Nategemea mkitoka hapa kwenye mafunzo kuhusu Utaratibu wa Makubaliano ya Kukiri Kosa ( Ple- bargaining) mtaenda kufanya kazi kwa weledi na pia nahitaji mjitahidi kujifunza kwa bidii ili muweze kufanya kazi vizuri katika eneo hilo.

Akifungua Mafunzo juu ya taratibu za Kisheria za Utaifishaji Mali na Makubaliano ya Kukiri Makosa kwa waendesha Mashtaka na Wapelelezi kwa Waendesha Mashtaka na wapelelezi kuanzia tarehe 28 Februari, 2022 hadi Machi 4 Machi, 2022 Bw. Mwakitalu alisema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imepewa jukumu kubwa la kuhakikisha nchi inakuwa na amani na utulivu hivyo aliwataka Waendesha Mashtaka na Wapelelezi kufikisha ujumbe kwa wahalifu kuwa uhalifu haulipi kwa kufanya kazi kikamilifu.

Alilishukuru Shirika lisilo la Kiserikali la PAMS foundation kwa kuona umuhimu wa kufadhili mafunzo na tafiti mbalimbali kwa watumishi wanaopambana na uhalifu.

                                                                                 


Aidha, aliwataka kuzingatia mafunzo wanayoyapata na kuyapa uzito unaostahili  kwakuwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi ni watu muhimu katika suala zima la utoaji wa Haki Jinai.

Mkurugenzi wa Mashtaka pia alitumia nafasi hiyo Kumshukuru Jaji  Mkuu wa Tanzania Mhe. Ibrahim Juma na Mahakama ya Tanzania kwa kukubali kutoa Waheshimiwa Majaji , Mahakimu na Wasajili kushiriki katika mafunzo kwa kutoa mafunzo(mada) kwa kwani kuwa nao ni nafasi adhimu na isiyoweza kupatikana kwa urahisi utokana na majukumu waliyonayo  na pia  uzoefu walionao wanapoutoa utasaidia kurekebisha makosa yanapojitokeza.

Mafunzo Mafunzo juu ya taratibu za Kisheria za Utaifishaji Mali na Makubaliano ya Kukiri Makosa kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi kuanzia tarehe 28 Februari, 2022 hadi Machi 4 Machi, 2022 yameandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kufadhiliwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la PAMS.


 

 

Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .