OFISI ya Taifa ya Mashtaka imesema imejiipanga kufungua matawi katika wilaya mbalimbali hapa nchini ili kuwasogezea wananchi huduma muhimu kisheria.
Akiongea wakati wa hafla fupi ya kufungua jengo la ofisi hizo katika wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, Mkuruhenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo Mganga amesema ofisi yake imejipanga vyema kuboresha mifumo ya haki, utawala bora na amani hapa nchini.
Aidha, amewahakikishia wananchi wilayani Mufindi kwamba hatua ya Serikali kufungua ofisi hizo italeta mafanikio chanya katika kuchochea kasi ya maendeleo kwa kupunguza, ama kuondoa kabisa maonevu katika jamii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bw. Jamuhuri William amepongeza jitihada zilizofanywa na Serikali katika kusogeza huduma za kisheria kwa wakazi wa wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment