Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amon Mpanju ,Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga wakijadiliana jambo baada ya kutoka kukagua gereza la Kayanga-Karagwe Mkoani Kagera.Jumla ya Washtakiwa 57 wanaume 54 na wanawake 3 wamefutiwa mashtaka katika Gereza la Kayanga, wakati Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju,pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Godfrey Mheluka walipotembelea na kukagua hali ya gereza hilo wilayani Karagwe Januari 21.
Bw. Biswalo amewaachia washtakiwa hao na kuwataka waliofutiwa mashtaka kujirekebisha na kwenda kuwa raia wema watakaporudi uraiani ikiwa ni pamoja na kujishulisha na shughuli za uzalishaji.
Washtakiwa wamefutiwa mashtaka mbalimbali yaliyokuwa yanawakabili ikiwepo wizi wa mifugo,ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi na ugomvi wa mipaka ya mashamba.
"Nendeni mkawe raia wema, badilikeni na msirudie tena kutenda uhalifu". Amesisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga.
Katika kundi la Washtakiwa walioachiwa huru wapo raia toka nchi jirani ya Burundi ambapo amewataka kufuata taratibu za kisheria endapo wanataka kuishi nchini.
Aidha Bw.Biswalo amewataka , Washtakiwa waliobaki gerezani kuendelea kujifunza na kubadilika wakati pia wakiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kuwasamehe na kuwafungulia nuru ili siku moja warejee uraia na kuendelea na maisha yao kama kawaida.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga na viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka walipotoka kukagua gereza lae Kayanga, Karagwe,mkoani kagera
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amony Mpanju mara baada ya kutembelea na kukagua hali ya Gereza la Kayanga-Kagera Januari 21,2020.

Mwonekano wa Nje wa Jengo la Gereza la Kayanga wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.






No comments:
Post a Comment