
Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP).Biswalo Mganga amebainisha hayo
wakati akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe mkoani
Kagera ambapo amesema kuwa mkoa huo unakabiliwa na kesi nyingi za mauaji.
Biswalo ameeleza baada ya kutembelea magereza mbalimbali na kuongea na mahabusu walioko ndani ameamua
kuwafutia washtakiwa 57 toka wilaya ya Karagwe, 54 Bukoba, 48 Biharamulo na Muleba 26 huku katika ziara hiyo akikutana
na badhi ya washtakiwa ambao ni wahamiaji haramu 15 waliokuwa wamekaribishwa na wazawa wa mkoa wa
Kagera.
"Kimsingi kuna makosa mengi na kesi nyingi
ambazo walengwa hawastahili kuwemo gerezani hivyo nimeamua kuwaachia kikubwa
niwaombe viongozi wa dini muendelee kuhubiri amani,upendo ili vitamalaki kwani
vitasaidia kupunguza hizi kesi"amesema Mganga.
Aidha, Bw.Biswalo ametanabaisha kuwa hatosita kumchukulia hatua
mtu yoyote bila kujali nafasi aliyonayo kisiasa,dini au Serikali ikigundulika kuwa
amejihusisha na vitendo vya Uhalifu
ambapo amesisistiza suala la amani ni jukumu la kila mtu hivyo wanawajibika
kuitunza kwa kuepuka kufanya makosa ya jinai.
Hata hivyo, Bw. Biswalo amewataka wahusika wote wenye
jukumu la kuendesha Mashtaka kutoka Taassi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU),
Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) na Polisi wote kutumia Ofisi ya
Taifa ya Mashtaka ya wilaya hiyo kinyume
cha hapo hatasita kuwanyanganya nyenzo alizowapatia za kibali cha kuendesha Mashtaka kwa Niaba ya Mkurugenzi wa
Mashtaka.
"Ninawaagiza waendesha Mashtaka wote wa
wilaya hii kuanzia leo majarada yote nataka leo yahamie kwenye ofisi hii ,na wote
mnaohusika na kuendesha mashtaka uwe Tanapa,Takukuru mtakuwa chini ya Mwanasheria
huyu Haruna Shomari na atakayekwambia mimi nipo chini ya DCI niambie sitasita kumtengua na nitamnyanganya nyenzo
zangu."amesma DPP Mganga.
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kagera Mhesimiwa
Ntemi Kilekamajenga amesema mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji
ambapo amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani ili kupunguza vitendo
vya uhalifu.
Jaji Ntemi amesema kesi
nyingi zinaweza kuishi kwa njia ya
usuluhishi nje ya mahakama hivyo kuipunguzia Serikali gharama za
uendeshaji wa kesi.
Aidha, Jaji Ntemi amesema mkoa wa Kagera kesi ambazo zipo katika hatua ya kusikilizwa
zinakaribia kuvuka 450 hivyo mkoa wa Kagera
unaweza kuwa wa pili au watatu kwa Tanzania kuwa na kesi nyingi za
mauaji
Askofu wa Jimbo Katoliki
la Kayanga Mhasham, Almachius Rweyongeza amebainisha
kuwa kufunguliwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
katika wilaya ya Karagwe kutasaidia
wananchi kupata haki kwa wakati sambamba na kuwakumbusha viongozi wenzake wa
dini kutimiza wajibu wao wa kuhubiri upendo na amani kwa mujibu wa maandiko
matakatifu.
Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) mkoa
wa Kagera Liberatha Bamporiki ameeleza kufunguliwa
kwa Ofisi hiyo ya Mashtaka katika wilaya ya Karagwe kutapunguza gharama na muda mwingi waliokuwa
wakiutumia kwenda Manispaa ya Bukoba kufautilia kesi zao hali itakyoaaidia kasi
ya mashauri kuongezeka na kusaidia kukamilika kwa wakati
Nao baadhi ya wakazi wa Karagwe akiwemo Clemence Isherenguzi na Selestine John wamesema kuwa kufunguliwa kwa ofisi hiyo ni ukombozi kwao kutokana na awali walikuwa wakitumia gharama kubwa kusafiri toka Karagwe kwenda Manispaa ya Bukoba umbali mrefu kufuata huduma za Mashtaka ambapo kwa sasa uwepo wa ofisi hiyo utasaidia kupunguza mzigo wa gharama kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera







Wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia hotuba za Viongozi mbalimbali.
Wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia hotuba za Viongozi mbalimbali. 








No comments:
Post a Comment