
BUKOBA-KAGERA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba katika Shauri Na. Ec 05/2020 imewatia hatiani washtakiwa sita akiwepo Deziderius Dominician na wenzake watano kwa kosa la kupatikana na nyavu haramu za uvuvi wa Samaki na kuwapa adhabu ya kulipa faini ya Shilingi Laki tano (500,000/=) kila mmoja au kwenda jela miaka mitatu pamoja na kutaifishwa mali zao zilizotokana na makosa ya uhalifu waliyoyafanya.
Hukumu hiyo imetolewa tarehe Desemba 30 baada ya washtakiwa kukiri Makosa na kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka ambayo ni (plea bargaining) .
Katika shauri hil0 Mahakama pia imewaamuru washtakiwa kuilipa Serikali fidiia ya kiasi cha shilingi Milioni Hamsini ambapo washtakiwa wamelipa fedha hizo kupitia akaunti ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Sambamba na amri hizo Mahakama pia imetoa amri ya kutaifishwa mali za washtakiwa zikiwepo gari aina ya Mitsubishi Canter lenye namba ya usajili T.683 CPL , Nyumba ya kulala Wageni, Nyumba ya kupangisha, Kiwanja kilicho na Mashine ya Kusaga na Kukoboa vyote vikiwa na thamani ya Shilingi za kitanzania Milioni Mia Moja na Hamsini na Tisa (159,000,000/=)
Kesi hiyo imeendeshwa na Wakili wa Serikali Shomari Haruna







No comments:
Post a Comment