• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

MWENYEKITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA NA TIMU YAKE WATEMBELEA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA.

 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala  Bora Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu akiwa ameongozana na Makamishna wa Tume ya  Haki za Binadamu na Utawala Bora wametembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa lengo la kujenga ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Makamishna wa Tume hiyo wamepata nafasi ya kuzungumza na wajumbe wa menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kikao kifupi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Dodoma.

Mwenyekiti huyo wa Tume alitumia nafasi hiyo kutoa elimu juu ya majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  na kuainisha maeneo ambayo Tume hiyo na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wanaweza kushirikiana katika utendaji kazi.

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu alimshukuru Mwenyekiti huyo wa Tume ya  Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuitembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kuahidi kwamba Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itashirikiana na Tume hiyo.

Ziara ya Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefanyika jijini Dodoma tarehe 14 Februari, 2023.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni wadau muhimu katika utoaji Haki.



Share:

MKURUGENZI WA MASHTAKA AMEITAKA MENEJIMENTI NA WAKUU WA MASHTAKA WA MIKOA KUANGALIA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI MFUMO WA HAKI JINAI NCHINI

 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu ameitaka Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa kuangalia changamoto zinazokabili utekelezaji wa Mfumo wa Haki jinai nchini.

"Ninyi mkiwa kama wasimamizi wa Majukwaa ya Haki jinai Mikoani lakini kwa mujibu wa majukumu yetu ninyi ni kiungo kikubwa kwenye ule mnyororo wa Haki jinai. Nafahamu mnajua mengi na mna mapendekezo mengi ambayo mnadhani yakitekelezwa Mfumo wa Haki jinai utakuwa bora. Kupitia kikao kazi hiki tutajadiliana na tutatoka na msimamo mmoja." Amezungumza  Mkurugenzi Mwakitalu.

Aidha, amewataka Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa kutekeleza majukumu  ya uendeshaji wa Mashtaka  kikamilifu na kwa mafanikio ili kuhakikisha kesi zinasikilizwa na kuisha kwa wakati.

Bw. Mwakitalu ameyasema hayo wakati akifungua Kikao kazi cha  Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa kinachofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.

Kikao kazi hicho kimelenga katika  kujadililiana na kukumbushana juu ya namna ambavyo majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatatekelezwa kikamilifu na kwa mafanikio. 

"Katika majadiliano yetu ya siku mbili tutapitia taarifa ya utendaji kazi ili kuangalia jinsi majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yanatekelezwa kwa mujibu wa Sheria, Katiba na kwa mafanikio." Amefafanua  Mkurugenzi Mwakitalu."

Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa kinafanyika  kuanzia tarehe 13 hadi 14 Februari, 2023 Jijini Dodoma.



Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .