• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

DPP AWATAKA WAAJIRIWA WAPYA KUFANYA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu ametoa wito kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  kufanya kazi kwa Uadilifu na Weledi ili kuhakikisha Haki, Amani  na Usalama vinapatikana nchini. 

Mkurugenzi Mwakitalu ameyasema hayo wakati akitoa neno la utangulizi kwenye Mafunzo elekezi ya awali kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 15 hadi 21 Aprili, 2023

Mafunzo hayo yanalenga katika kuwajengea uwezo watumishi waajiriwa wapya ili kuwawezesha kufahamu namna ya kuenenda na kufanya kazi kama watumishi wa  Serikali.

Akizungumza katika mafunzo hayo Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mhe. Ayub Mwenda amewataka waajiriwa wapya kujibidiisha kwa Weledi na kimaadili katika kutekeleza majukumu ya kikatiba waliyopewa.

Naye Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam Mhe. Edwin Kakolaki aliwapongeza waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na  kuwataka kuepuka tamaa na kuridhika na watakachokuwa wanapata na kujenga uaminifu.



Share:

WAENDESHA MASHTAKA WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA BILA KUMUONEA MTU - WAZIRI NDUMBARO

 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  amewataka Waendesha Mashtaka na Makatibu Sheria wapya kwenda kusimamia Sheria bila kumwonea mtu wala kumpendelea mtu yeyote wakati wa utendaji wao wa kazi ili kuhakikisha haki inapatikana kwa usawa.

Waziri Ndumbaro amebainisha  hayo wakati akifungua Mafunzo elekezi ya awali kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 15 hadi 21 Aprili, 2023.

Dkt. Ndumbaro amesema Waendesha Mashtaka wanapaswa kwenda kusimamia haki za msingi za kiraia kama  unyanyasaji wa kijinsia ambao ni ukatili mbaya sana na kuwataka  mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na  vitendo hivyo kuhakikisha anahukumiwa ipasavyo.

Waziri Ndumbaro ameendelea kwa kusema Waendesha Mashtaka wanatakiwa kusimamia kwa umakini kesi zinazohusiana na mazingira na Ikolojia ambapo tabia ya watu kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa imeonekana ni mtindo wa  kawaida, kwani sheria hiyo ya mazingira imeingia kwenye makosa ya jinai.

"Tumekuwa na mgogoro mrefu Tanzania kati ya wakulima na wafugaji wakipigana na kuuana, vitendo hivyo ni jinai. Msiingie kwenye mtego wa kumpendelea mkulima wala mfugaji bali tendeni haki. Aliokiuka sheria ashughulikiwe." Ameyasema hayo Dkt. Ndumbaro.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imebahatika kupata jumla ya watumishi  353 ambao wote ni waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

"Ajira hiyo mpya ni mwendelezo wa jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inafungua ofisi zake kila Wilaya ili wananchi waweze kupata huduma kwa ukaribu na uharaka zaidi." Amezungumza Mkurugenzi Pande.

Amesema  kazi ya Uwakili wa Serikali ni kazi nyeti  kwasababu inagusa haki za watu wengi kwa maramoja, hivyo Wakili wa Serikali asipotambua jukumu lake la kuendesha mashtaka anaweza asifikie malengo husika yaliyokusudiwa.

Aidha, Naibu Mkurugenzi amewataka waajiriwa hao wapya kujiepusha na vitendo vya rushwa kazini.

"Anayeweza kukataa rushwa ni mtu ambaye mwenye hofu ya Mungu, ukikosa kuwa na hofu ya Mungu unaingia kwenye kishawishi cha kuchukua rushwa." Ameyasema hayo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.



Share:

OFISI ZA MASHTAKA WILAYA KUENDELEA KUIMARISHWA - DPP

 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inaendelea kuimarisha huduma za utoaji haki kwa wananchi ambapo katika kuboresha huduma hizo inatarajia kufungua Ofisi mpya za wilaya  50 katika mwaka wa fedha 2022/2023.

 


Mkurugenzi wa Mashtaka ameyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kinachofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 6 Aprili, 2023 Mjini Morogoro.

Sambamba na kufungua Ofisi mpya amesema Ofisi za Mashtaka za Mikoa na Wilaya zilizokuwepo zinaendelea kuimarishwa kwa kuongeza vitendea kazi, kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza maslahi kwa watumishi pamoja na kutoa mafunzo mbalimbali yakayowaongezea ufanisi katika utendaji kazi.

 


Amesema ili kuhakikisha utendaji kazi unaboreshwa ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 ofisi imezingatia vipaumbele vya kuimarisha utoaji wa huduma za kimashtaka kwa wananchi, kuimarisha shughuli za kuratibu Upelelezi pamoja na kufanya Ukaguzi kwenye maeneo ambayo washtakiwa au wahalifu wanatunzwa.

"Katika uimarishaji huu tumeweka kipaumbele kwenye kupata vitendea kazi vikiwepo magari, kompyuta, na printa ambavyo vitatuwezesha katika kutoa huduma bora na kwa ukamilifu kabisa kwa wananchi." Amefafanua  Mkurugenzi Mwakitalu." .

 


Aidha, Mkurugenzi wa Mashtaka aliwataka Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kushiriki kikamilifu kwenye mijadala na majadiliano na pia kufikia maamuzi na maazimio ya kikao hicho cha Baraza kwa maslahi ya Watumishi, maslahi ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kwa Taifa kwa ujumla.

"Tunalo jukumu kubwa la kuwahudumia wananchi kwenye eneo hili ambalo tumekabidhiwa na ili tuweze kulitekeleza kikamilifu jukumu hili tunatakiwa kushiriki kikamilifu kwenye mijadala na majadiliano katika kikao hiki." Alisisitiza.

 Naye  Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande  akizungumza katika kikao hicho alisema katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi Menejimenti inapata nafasi ya kusikia sauti ya watumishi pamoja na kupata malalamiko na mapendekezo na mawazo ya watumishi kwa ujumla yanayosaidia katika kuboresha utendaji kazi.

Kwa upande wake Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Samwel Nyungwa ameishauri Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuhakikisha inafanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi mara mbili kwa mwaka ili   kutekeleza takwa la kisheria linaloloelekeza kufanyika kwa  vikao viwili kwa mwaka.

 Alifafanua kuwa kikao kimoja ni kwa ajili ya mipango na kikao cha pili ni kwa ajili ya tathmini baada ya kumaliza robo ya kwanza ya mwaka wa fedha ili kuisaidia menejimenti kufanya uboreshaji wa  mipango iliyopangwa mwanzoni.

 Naye mwakilishi wa TUGHE Taifa Bw. Nsubisi Mwasandende ameishauri Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuendelea kuzingatia uboreshaji wa maslahi ya watumishi na kuhimiza uwajibikaji kwa  kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi ili kuleta tija na  kutimiza malengo yaliyokusudiwa na ofisi.


Bw. Mwasandede ameyasema hayo wakati akitoa salamu na nasaha kutoka TUGHE Taifa.


 

Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .