Wa Kwanza Kulia ni Mkurugenzi wa Divisheni ya Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Tumaini Kweka akiwa pamoja na viongozi wengine katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliohama vituo vya kazi na kuwakaribisha waliofika Mkoani Shinyanga July 22,2023.
Na Ofisi ya Mashtaka-Kahama Shinyanga.
Mkurugenzi wa Divisheni ya Utenganishaji wa Shughuli za
Mashtaka na Upelelezi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Tumaini Kweka amewataka Watumishi wapya kuwa makini kwa kujiepusha na
vitendo vya rushwa kwa kuwa Shinyanga ni mojawapo ya Mikoa yenye vishawishi
vingi hivyo wafanye kazi kwa weledi kwa kuongozwa na uadilifu, hofu ya Mungu,
kwa kuwa ni jukumu lao huku akiwataka
kuongozwa na weledi na ufanisi ili kutenda haki iliyo na usawa kwa wananchi.
Bw. Kweka ameeleza hayo wakati akifungua halfa fupi ya kuwaaga
waliokuwa Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga na
kuwakaribisha Watumishi wapya wakiwemo waliojariwa na waliohamia Mkoani
Shinyanga wa ofisi hiyo pamoja na kupata chakula cha jioni kiliyoandaliwa na
Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Kweka amesema kuwa kuajiriwa ni sehemu ya
kuaminiwa kuwatumia wananchi hivyo jukumu lao ni kuendelea kufanya kazi kwa
ushirikiano na kuhudumia wananchi kwa
kuzingatia weledi wa kazi yao na taaluma yao
Aidha Mkurugenzi Kweka ameeleza kuwa kazi hiyo ngumu na
inavishawishi vingi hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kuzingatia miiko ya
utumishi wa umma kwa kujiepusha na rushwa pamoja na kupindisha haki hali ambayo
itasababisha kudhohofika kwa utendaji.
Bw. Kweka pia ameishukuru Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani
Shinyanga kwa kufanya kazi zake kwa kujituma na kuleta ufanisi katika
kushughulikia mashauri ya kesi
mbalimbali ambapo wamefanya kazi kubwa na yenye kutukuka.
“Miongoni mwa
watumishi waliokuwepo hapa Shinyanga na Kahama ambao ni wanawake wameweza
kufanya kazi zao kwa uweledi na umakini mkubwa na kuleta tija kwa jamii pamoja
na wao wenyewe ambapo wapo waliopanda na kuwa Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa na
Wilaya kwenye maeneo mbalimbali hivyo watumishi
wapya wanapaswa kuiga mfano wa wengine.” Amesema Mkurugenzi Kweka”
Bw. Kweka amesema kuwa Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga imekuwa mfano katika utendaji kazi wake na kuamsha hali katika maeneo mengine ambapo amewataka waajiriwa wapya kuwa mabalozi wazuri wa kazi za Ofisi hiyo.
Akizungumza kwa niaba Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kahama Bw. Robert Kwela amewataka
watumishi hao kuishi katika misingi ya ajira kwa kuwa ni wengi wanaotafuta,
sambamba na kuwakata Vijana waliongia kazini katika ajira mpya kuhakikisha
wanafanya kazi zao kwa weledi na kutenda haki.
Naye Mkuu wa
Mashtaka Mkoa wa Shinyanga Bi. Ajuaye Zegheli amewahakikisha ushirikiano na watumishi wapya sambamba na kuwataka wanaposhughulika na mashtaka kutanguliza maslahi mapana ya umma na si kutanguliza mahitaji yao binasfi.
Aidha watumishi hao pia wametoa azwadi mbalimbali ikiwemo tunzo za heshima kwa watumishi wenzao ikiwa nis ehemu ya kutambua mchango wako katika utumishi wakati wakiwa Mkoani Shinyanga.ambapo pia Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Sylvester Mwakitalu amepewa tunzo ya heshima kwa mchango wake katika usimamizi na usikilizaji wa changamoto za watumishi hao.
Tazama Picha mbalimabali katika matukio yaliyofanyika









