• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAPONGEZA WATUMISHI WA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA MKOA WA ARUSHA

 Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka  amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Arusha kwa kazi nzuri wanayoifanya katika  Uendeshaji wa Mashauri ya Jinai katika mkoa huo na  kuwataka kuendelea na moyo huo wa kujitoa kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa mshikamano ili kutimiza malengo ya Taasisi.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo wakati alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Arusha mara baada ya kumaliza kushiriki  kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika tarehe 1 Mei, 2024 Jijini Arusha.

"Kwa niaba ya timu nzima ya Menejimenti ninaahidi tutaendelea kupambana usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba maslahi ya watumishi wote wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yanaboreshwa na pia kuhakikisha kwamba mipango yote ya Taasisi tuliyonayo yanafikiwa." Amebainisha hayo Naibu Mkurugenzi Bibiana.



Share:

NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA AMEWATAKA WATUMISHI WA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA HAKI

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo amewataka watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kufanya kazi kwa kuzingatia haki, ushirikiano kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo ya Jamii na Taifa kwa ujumla.

Naibu Mkurugenzi amebainisha hayo mapema tarehe 30 Aprili, 2024 wakati akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma alipowasili kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake.

"Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kuniteua kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka,  ninaahidi kujitahidi kwa uwezo wangu wote kusaidia majukumu yako kwa weledi na uadilifu mkubwa." Amesema Mkurugenzi Bibiana.

Naibu Mkurugenzi amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ina jukumu la kikatiba chini ya Ibara 59B ya kusimamia Uendeshaji wa Mashtaka nchini na jukumu hili linapaswa kufanyika kwa kuzingatia misingi ya haki na maslahi makubwa ya umma. Ofisi hiyo pia imepewa jukumu kubwa la kuamua juu ya hatma za watu, maisha ya watu hivyo watumishi hao wanapaswa kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuzingatia sheria bila kuwa na upendeleo wala kumwonea mtu.

"Niwaombe tushirikiane pamoja katika kutimiza jukumu hili ili kuifanya taasisi yetu kuwa bora na inayoongoza kwa kutenda haki ndani ya nchi hii." Amefafanua hayo Naibu Mkurugenzi.

Sambamba na hilo Naibu Mkurugenzi ametoa pongezi kwa Uongozi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ushirikiano wanaoutoa kwa kupambana usiku na mchana ili kuifanya taasisi izidi kusonga mbele ili kuwawezesha wananchi kupokea huduma wanazostahili kutoka kwao ambapo imepelea kupunguza malalamiko kwa wananchi na kesi kusikilizwa kwa wakati.



Share:

RAIS SAMIA AMWAPISHA BIBIANA KILEO KUWA NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  tarehe 28 Aprili, 2024 amewaapisha Viongozi watatu katika nyadhifa mbalimbali, akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo.

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika katika Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi wengine wakuu wa Kitaifa, akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma. 

Wengine ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Hassan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi na wengine wengi.

Viongozi wengine walioapishwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria ambae ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Winfrida Korosso na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali,  Bi. Alice Mtulo.

Waapishwa hao waliteuliwa na Rais Samia kushika nyadhifa hizo tarehe 4 Aprili, 2024. Kabla ya uteuzi huo, Bi. Bibiana alikuwa Mkuu wa Mashtaka wa Mkoa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mwanza na Bi. Alice alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Kesi na Udhibiti wa Ubora katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.



Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .