JIEPUSHENI NA VITENDO VYA RUSHWA HAKIKA SITAMVUMILIA MTUMISHI ATAKAYEHUSIKA NA RUSHWA AMESEMA DPP BISWALO MGANGA

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Ukusanyaji, Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa  kwa njia ya  Kidijitali kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara.
SINGIDA.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga amewataka  Makatibu Sheria nchini  kuhakikisha wanatumia vizuri mfumo mpya wa Ukusanyaji, Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa  kwa njia ya  Kidijitali hali itakayowezesha utoaji wa Takwimu sahihi kwa maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi  wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga  wakati akifunga Mafunzo ya siku 6 ya Makatibu Sheria kutoka Mikoa yote ya Tanzania bara mafunzo yaliyofanyika Manispaa ya Singida yakiwa  na lengo la kuwajengea uwezo makatibu hao katika  Ukusanyaji, Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa  kwa mfumo wa Kidijitali.

Ameeleza kuwa jukumu la watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni kuwajibika kwa umma  na serikali hivyo Makatibu  Sheria wanalo jukumu kubwa la kuhakakikisha huduma bora za mashtaka zinawafikia wananchi na kuiona ofisi kuwa yao.

Naomba niseme jukumu kubwa tulilonalo ni kuwajibika kwa Umma, Taasisi na Serikali kwa kuhakikisha tunatoa huduma bora na za  kuvutia kwa wananchi,  nisingependa kusikia lugha mbaya toka kwenu zikiwahusu watu wanaokuja kwenu kutafuta msaada badala yake tumieni lugha nzuri kwani majalada yote yanapitia kwenu”amesema Bw.Biswalo 

Biswalo amesema Makatibu Sheria ndiyo mlango wa Kupokea majalada hivyo wasiwe chanzo cha kujihusisha na vitendo vya rushwa kwani kufanya hivyo kunadhoofisha maendeleo ya Nchi na Taifa kwa ujuma

Sitaki kusikia ninyi  Makatibu  Sheria mnakuwa vyanzo vya kujihusisha na vitendo vya Rushwa ndani ya taasisi kwa sababu tu watu wote wanaanzia kwenu  na wala msidanganyike kwani mkifanya hivyo mtaishia  pabaya, siko tayari kumvumilia mtu anayekula RushwaBw.Biswalo

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Biswalo amewaasa watumishi hao kutoharibu taaluma yao ya Ukatibu Sheria  kwa kujihusisha na uvujishaji wa siri za Nyaraka za Ofisi kwani kufanya hivyo ni kinyume cha maadili pia hali ambayo inahatarisha usalama wa nchi.

Niwaombe ninyi Makatibu Sheria mnayo nafasi kubwa ya kutupatia na kusaidia  taarifa za siri juu ya watu wanaofutilia majalada yetu hususani makanjanja ili tumfahamu mtu anayefuatilia ana lengo gani na tujue tunaanzia wapi kumchukulia hatuaBw.Biswalo

Aidha, Biswalo akizugumzia suala la Mfumo mpya wa Ukusanyaji,Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa  kwa mfumo wa Kidijitali amewataka kuhakikisha taarifa zinaingizwa kwenye mfumo kwa uhakika na umakini huku akiwaonya Makatibu hao kwenda kufanya kazi zao kwenye internet Café ambako nyaraka za serikali husalia  na kuhataraisha usalama wa ofisi na nchi kwani watu wabaya wanaweza kuzitumia kwa maslahai yao binafsi.

Ni marufuku kutumia barua pepe  za Ofisi kwenye Kompyuta za internet  café utumike ndani ya ofisi na Kompyuta za ofisi tu kwani kutumia huko taarifa zinabaki  na watu wanaanza kudukua hivyo kwa hili atakayebainika sitamwonea huruma lazima hatua kali zichukulie dhidi yakeBw.Biswalo

Biswalo ameongeza kuwa utumiaji wa mfumo huo mpya wa Uchakati na utumaji wa taarifa  isiwe sababu ya kuachana na mfumo wa zamani wa regista  ambapo amesisitiza mifumo yote kwenda samabmba hadi pale mfumo wa kidijitali utakapokuwa umeimarika na kusimama vizuri

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa Upelelezi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  ambaye anashughulikia Usimamizi wa Kesi  Bw. Tumaini Kweka amesema kuwa  Makatibu Sheria ni watu muhimu sana hivyo mafunzo hayo yamejikita kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotarajiwa pamoja na kuwawezesha kukabiliana na changamoto wanazokutana  nazo

Naomba  kukutaarifu kuwa mafunzo haya yameshirikisha washiriki 30 kutoka Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara  hivyo tuna imani kuwa kile walichojifunza hapa kinaenda kuwa chachu kubwa kwa wengine waliosalia kwenye maeneo yao”amesema Bw. Kweka 

Kweka ameongeza kuwa katika mafunzo hayo jumla ya Mada nane zimewailishwa kutoka kwa watalaamu wa ndani na nje ya taasisi hiyo waliowasilisha mada kwa kina na washiriki kupata nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa”

Naye mwakilishi wa washiriki wa Mafunzo hayo ya Ukusanyaji,Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa  kwa njia ya  Kidijitali Bi Faraja amesema kuwa mafunzo hayo kwao ni chachu kubwa ya kuboresha  utendaji kazi wao hususani kuendana  na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Mafunzo  hayo  yameandaliwa kwa ushirikiano wa  Idara  ya  Usimamizi wa Kesi  na uratibu wa upelelezi na Programu ya BSAAT kupitia Divisheni ya Makosa ya Udanganyifu, Utakatishaji fedha na Rushwa Ofisi ya Taifa  ya Mashtaka.  Idrisa Heri Swalehe Afisa Tehama, kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka(NPS) Mkoani Mwanza  akitoa elimu ya Ukusanyaji,Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa  kwa mfumo wa KidijitaliWashiriki wakiendelea kujifunza kwa vitendo wakati wa mafunzo ya  Ukusanyaji, Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa  kwa njia ya  Kidijitali kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara.Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga akitazama namna  zoezi la elimu kwa vitendo linavyofanyika baada ya Makatibu Sheria  kupata Mafunzo  ya Ukusanyaji, Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa kwa mfumo wa  Kidijitali.Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa Upelelezi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  ambaye anashughulikia usimamizi wa Kesi Tumaini Kweka akifuatilia kwa ukaribu mafunzo.Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga akiwa ameketi kwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa Upelelezi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  ambaye anashughulikia usimamizi wa Kesi Tumaini Kweka wakiendelea kufuatilia mafunzo.

Bi Faraja mwakilishi wa washiriki wa Mafunzo hayo ya Ukusanyaji,Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa  kwa njia ya  Kidijitali akishukuru kwa niaba ya washiriki wenzake.
Baadhi ya  washiriki wakiedelea kujifunza kwa vitendo namna ya kutumia mfumo mpya wa kidijitali  wa Ukusanyaji, Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai, na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa.
Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .