• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

KAMISHNA WA KAZI ATOA RAI KWA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

 


Kamishna wa Kazi Brigedia Jenerali Francis Mbindi amelitaka Baraza la Wafanyakazi litumike kuimarisha Taasisi katika kazi zake kwa kufuata matakwa ya kisheria na katiba kwa kuwa ni chachu ya kuimarisha mahusiano mema mahali pa kazi.

Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka uliofanyika leo tarehe 24 Septemba, 2021 katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.

Kamishna huyo ametoa rai kwa Menejimenti pamoja na uongozi wa TUGHE kuzingatia Kalenda za vikao vya Baraza la Wafanyakazi ya kwamba kufanya vikao kwa mujibu wa sheria.

Brigedia Jenerali aliendelea kueleza kuwa Taasisi za umma ambazo bado hazijaunda Mabaraza ya Wafanyakazi, kuunda maramoja na pia kufanya vikao kwa mujibu wa sheria iliyounda mabaraza hayo kwani kufanya hivyo ni kujenga na kudumisha utawala bora katika utumishi wa umma.




Nae pia Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu ameeleza kuwa Baraza la Wafanyakazi ni chombo muhimu katika Taasisi za Utumishi wa Umma kwa maana ni chombo ambacho kinashauri Menejimenti kwenye masuala mbalimbali ambayo yanaweza kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Ofisi na pia kuishauri Menejimenti kuhusu haki,  wajibu, maslahi na mazingira bora ya watumishi pamoja na kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sheria, bajeti, miongozo na Sera za Ofisi ili ziweze kufanya kazi ni lazima zipitishwe na baraza.

''Hivyo basi kuzinduliwa kwa baraza hili kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni hatua kubwa na ni muhimu sana kwetu"
Amezungumza hayo Bw. Mwakitalu.




Aidha Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Juma Katanga ambaye pia Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ameahidi kudumisha ushirikiano na Wafanyakazi wote katika kutekeleza  majukumu yake ya Uratibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Share:

UFUNGUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA



 

Share:

PROFESA KABUDI AITAKA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA(NPS) KUONGEZA KASI YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA.

 Waziri wa Katiba na Sheria (Kushoto) Mh.Profesa Palamagamba Kabudi akifungua jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara lililoko katika Mji Mdogo wa Mugumu

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Profesa Palamagamba Kabudi amesema umefika,wakati sasa wa  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuongeza kasi ya kusimamia makosa ya uharibifu wa mazingira kwa ukubwa wake badala ya kazi hizo kufanywa na Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira ( NEMC) pekee kwakuwa uharibifu wa mazingira ni kosa ni uhujumu uchumi.

Mazingira yetu yanazidi kuharibiwa sana, kuharibu mazingira ni kosa la jinai. Tunakata miti bila huruma. Umefika wakati sasa jukumu la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kusimamia na kutunza mazingira lionekane wazi ili watu wajue kuwa kuharibu mazingira ni kosa la jinai na ni uhujumu uchumi.

Mhe. Kabudi ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Serengeti zilizofanyika mjini Mugumu leo tarehe 21 Septemba, 2021 ambapo alisema sasa kuna umuhimu wa kuipitia  Sheria kuu “Penal Code” ili kuhakikisha baadhi ya makosa yanayohusiana na uharibifu wa mazingira na maliasili yanaingizwa.

Alisema uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Serengeti litasaidia kusogezwa kwa karibu kwa  huduma za mashtaka kwa wananchi pamoja na kuipunguzia serikali gharama za uendeshaji kesi na pia itasaidia kupambana na ujangili katika wilaya ya Serengeti.

Mhe. Kabudi  alisema uhifadhi wa  maliasili za nchi yetu unahitaji ukali wa sheria ili kudhibiti vitendo viovu na kutaka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuyachukulia kwa uzito makosa hayo kwa kuwa yanahujumu uchumi ambapo alitaka maeneo yote yenye maliasili kuwa na Mawakili wa Serikali ili kupambana na makosa ya uharibifu wa mazingira.

Aidha, Mhe. Kabudi alitumia fursa hiyo kuipongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua ya kupata ofisi na wadau wote waliohisani na kuhakikisha kuwa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka linajengwa.

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka Ndg. Slyvester Mwakitalu alisema uwepo wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilayani Serengeti utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuongeza kasi ya utendaji kwakuwa mazingira ya utendaji kazi utakuwa umeboreshwa.

Alisema ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Serengeti ni jambo la kujivunia kwakuwa ni jengo la kwanza kujengwa tangu kuanzishwa kwa Ofisi yaTaifa ya Mashtaka mnamo mwezi Februari 2018. Aidha. Aliwashuru wadau wa Makampuni ya GRUMET kwa kufadhili ujenzi wa jengo hilo na kuwaomba wadau wengine pia kujitokeza kufanya hivyo wanapoombwa kuhisani ujenzi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Vincent Mashinji akizungumza katika hafla hiyo alisema uwepo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Serengeti utasaidia kuboresha huduma na utaipunguzia serikali gharama za uendeshaji wa kesi na upelelezi ambapo aliahidi kuongeza ushirikiano katika utendaji wa kazi.

Aidha, Mhe. Mashinji aliwataka wakazi wa Serengeti kutii sheria bila shuruti na kuitumia ofisi hiyo kwa kutoa ushirikiano mzuri pale wanapohitajika kutoa ushahidi hali ambayo itapelekea kesi kuisha kwa wakati.Mwonekano wa  mbele wa  Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya  ya  Serengeti Mjini Mugumu Mkoani Mara 

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba  Kabudi akikata utepe  kuashiria Ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mugumu-Serengeti Mkoani Mara.

Baadhi ya Viongozi wakeindelea kufautailia Burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendele wakati wa Ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani Serengeti Mkoani Mara.

Baadhi ya wakazi wa Serengeti wakiedelea kufuatilia hotuba za Viongozi 

Viongozi mbalimbali wakiendelea kufautilia na kutazama burudani wakati wa ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashataka Seregenti Mara

Viongozi mbalimbali wakiendelea kufautilia na kutazama burudani wakati wa ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashataka Seregenti Mara


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba  Kabudi akitoa zawadi wa wacheza ngoma  wakati wa ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti.

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba  Kabudi akitoa tuzo ya  zawadi  kwa Mkurugenzi Mkuu wa Grumet Fund Bw. Noel Mbise ikiwa ni sehemu ya kkutambua mchango wao kwenye ujenzi wa jengo hilo wakati wa ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti. 


 

Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .