KAMISHNA WA KAZI ATOA RAI KWA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

 


Kamishna wa Kazi Brigedia Jenerali Francis Mbindi amelitaka Baraza la Wafanyakazi litumike kuimarisha Taasisi katika kazi zake kwa kufuata matakwa ya kisheria na katiba kwa kuwa ni chachu ya kuimarisha mahusiano mema mahali pa kazi.

Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka uliofanyika leo tarehe 24 Septemba, 2021 katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.

Kamishna huyo ametoa rai kwa Menejimenti pamoja na uongozi wa TUGHE kuzingatia Kalenda za vikao vya Baraza la Wafanyakazi ya kwamba kufanya vikao kwa mujibu wa sheria.

Brigedia Jenerali aliendelea kueleza kuwa Taasisi za umma ambazo bado hazijaunda Mabaraza ya Wafanyakazi, kuunda maramoja na pia kufanya vikao kwa mujibu wa sheria iliyounda mabaraza hayo kwani kufanya hivyo ni kujenga na kudumisha utawala bora katika utumishi wa umma.




Nae pia Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu ameeleza kuwa Baraza la Wafanyakazi ni chombo muhimu katika Taasisi za Utumishi wa Umma kwa maana ni chombo ambacho kinashauri Menejimenti kwenye masuala mbalimbali ambayo yanaweza kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Ofisi na pia kuishauri Menejimenti kuhusu haki,  wajibu, maslahi na mazingira bora ya watumishi pamoja na kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sheria, bajeti, miongozo na Sera za Ofisi ili ziweze kufanya kazi ni lazima zipitishwe na baraza.

''Hivyo basi kuzinduliwa kwa baraza hili kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni hatua kubwa na ni muhimu sana kwetu"
Amezungumza hayo Bw. Mwakitalu.




Aidha Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Juma Katanga ambaye pia Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ameahidi kudumisha ushirikiano na Wafanyakazi wote katika kutekeleza  majukumu yake ya Uratibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .