Aidha, Bi. Neema aliwashukuru Uongozi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa ushirikiano wao waliotuo katika kufanikisha suala zima la mafunzo ya mfumo huo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
-
Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti
Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.
-
UKATAJI WA UTEPE
UKATAJI
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.
-
KAIMU MKURUGENZI AWATAKA MAKATIBU SHERIA NA MAWAKILI KUZINGATIA WALIYOFUNDISHWA
KAIMU MKURUGENZI KWEKA ASISITIZA JUU YA MATUMIZI YA MFUMO KATIKA UPANDE WA TAKWIMU
Kaimu Mkurugenzi Divisheni ya Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma amewataka Makatibu Sheria na Mawakili kutumia nafasi hii ya mafunzo, kujifunza namna ya kuutumia mfumo huu vizuri ili kuwasaidia katika kazi zao mbalimbali za kila siku hususani kwa upande wa Takwimu ambapo kwa kupitia mfumo huu utasaidia kuingiza taarifa zilizo sahihi.
Aidha, alieleza kuwa kwa kupitia Takwimu zilizopo kwenye mfumo zitatoa majibu ya mahitaji yote ya kiofisi na pia itawasaidia Mawakili pamoja na Makatibu Sheria kujua ni idadi ngapi za kesi zilizopokelewa kutoka nchi nzima.
"Roho ya Taasisi yoyote ni Takwimu kwani ndio roho ya nchi. Ni wajibu wenu kuhakikisha kwamba huu mfumo mnauelewa vizuri na kuutunza."
Amezungumza hayo Mkurugenzi Kweka wakati akifanya ufunguzi wa awamu ya pili ya Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Kesi kwa Makatibu Sheria na baadhi ya Mawakili wa Serikali wanaoshughulika na Takwimu yaliyoanza mnamo tarehe 5 Januari 2022 na kumalizika tarehe 8 Januari, 2022 Jijini Dar es salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
KAIMU MKURUGENZI KWEKA AWATAKA MAKATIBU SHERIA KUJIFUNZA MFUMO KWA DHATI
Kaimu Mkurugenzi Divisheni ya Utenganishaji wa shughuli za Mashtaka na Upelelezi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma Bw. Tumaini Kweka amewataka Makatibu Sheria na Mawakili kujifunza mfumo kwa dhati kwa vitendo na kuuelewa vizuri ili iwasaidie na kuwarahishia katika majukumu yao ya kiutendaji kazi wa kiofisi wa kila siku.
Mkurugenzi Kweka amezungumza hayo wakati akitoa salamu fupi kwa washiriki wa Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Kesi kwa Makatibu Sheria na baadhi ya Mawakili wa Serikali wanaoshughulika na Takwimu yaliyoanza jana tarehe 5 Januari 2022 na kumalizika tarehe 8 Januari, 2022 Jijini Dar es salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Kesi kwa Makatibu Sheria na baadhi ya Mawakili wa Serikali wanaoshughulika na Takwimu wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Divisheni ya Utenganishaji wa shughuli za Mashtaka na Upelelezi Bw. Tumaini Kweka wakati akitoa salamu fupi kwenye mafunzo hayo yaliyoanza jana tarehe 5 Januari 2022 na kumalizika tarehe 8 Januari, 2022 Jijini Dar es salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
Baadhi ya washiriki wakiendelea kujifunza kwa vitendo na kuelekezana namna ya kutumia mfumo katika utendaji wao wa kazi kwenye Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Kesi kwa Makatibu Sheria na baadhi ya Mawakili wa Serikali wanaoshughulika na Takwimu yaliyoanza jana tarehe 5 Januari 2022 na kumalizika tarehe 8 Januari, 2022 Jijini Dar es salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
MKURUGENZI KADUSHI AWATAKA MAKATIBU SHERIA KUTUMIA VIZURI MFUMO NA KUWA WAALIMU KWA WENGINE.
Mkurugenzi Divisheni ya Utaifishaji mali, Makosa yanayovuka mipaka na kupangwa kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma Bw. Paul Kadushi amewataka Makatibu Sheria na baadhi ya Mawakili wa Serikali kwenda kuwa waalimu wazuri wa kufundisha jinsi ya kutumia mfumo katika kufanya kazi za Taasisi kwa watumishi wengine wote wa Mikoa na Wilaya, kwani mfumo huu utakuwa na manufaa makubwa sana katika kuhifadhi na kuongeza ufanisi wa kazi za kiofisi, kwani wengi walikuwa wakipata changamoto nyingi katika uandaaji wa taarifa.
"Mnaporudi katika Mikoa yenu mkawe waalimu na mkawafundishe watumishi wengine yale yote mtakayofundishwa. Na ninaamini kwamba mtatoka hapa mkiwa na uwezo na mtautumia mfumo huu kwa ueledi na nidhamu ya hali ya juu"
Aliyasema hayo Mkurugenzi Kadushi wakati akifungua Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Kesi kwa Makatibu Sheria na baadhi ya Mawakili wa Serikali wanaoshughulika na Takwimu yaliyoanza leo tarehe 5 Januari 2022 na kumalizika tarehe 8 Januari, 2022 Jijini Dar es salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Aidha Mkurugenzi Kadushi alieleza kuwa mfumo huu unajukumu kubwa la kukusanya, kuchakata na kutunza taarifa zote zinazohusiana na uendeshaji wa kesi za Jinai nchini ambapo sehemu kubwa ya majukumu haya yanafanyika kwa mfumo wa zamani.
Pia Mkurugenzi aliishukuru Mamlaka ya Mtandao Serikali (eGA) kwa ushirikiano wao waliouonyesha katika mchakato wa uandaaji wa mfumo huu, kwani kwa kupitia Taasisi hiyo Serikali imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba Taasisi za Serikali zinaongeza kasi ya kuhamishia majukumu yake katika mtandao.





