• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

CHANGAMOTO ZISIWE KIKWAZO CHA KUACHA KUUTUMIA MFUMO - KAIMU NAIBU DPP

 Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa Upelelezi Bi. Neema Mwanda amewataka Wakuu wa Mashtaka wa Wilaya na Waendesha Mashtaka Viongozi kutokuacha kuutumia mfumo wa kielekitroniki sababu ya changamoto yoyote ile itakayotokea wakati wakitumia mfumo huo kwani changamoto ni sehemu ya kuendelea kujifunza na hutokea katika mfumo wowote ule. Na endapo watakutana na changamoto yoyote ile basi wasisite kutoa taarifa kwa viongozi husika wa mfumo huo.


"Tutakapoanza kuutumia mfumo huwa kuna changamoto nyingi ambazo pia ni sehemu ya kujifunza, changamoto hizi zisiwe kikwazo cha kuacha kuutumia mfumo wetu."

Amezungumza hayo Kaimu Mkurugenzi Mwanda wakati akihitimisha Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya kesi kwa Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa na Wilaya pamoja na Waendesha Mashtaka Viongozi yaliyoanza  tarehe 22 Februari, 2022 na kumalizika tarehe 25 Februari, 2022 Jijini Dar es Salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)


Aidha, Kaimu Mkurugenzi alieleza kuwa kuanzishwa kwa mfumo huu kumelenga kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma pasipo kujali muda wala sehemu ya kijografia, ikiwa ni pamoja na kuongeza uwazi na kupunguza mianya ya rushwa kwenye taasisi.



Pia Kaimu Mkurugenzi alitoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kuwa anawasihi na kuwaomba kwenda kuufanyia kazi mfumo huo vizuri na kutoa elimu kwa  wengine waliopo katika vituo vyao vya kazi.


Share:

KAIMU MKURUGENZI ATOA WITO KWA WAKUU WA MASHTAKA WA WILAYA NA WAENDESHA MASHTAKA VIONGOZI

 Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda amewataka Wakuu wa Mashtaka wa Wilaya na Waendesha Mashtaka Viongozi  kwenda kuwa waalimu kwa wengine kwenye vituo vyao vya kazi ili kila mtumishi apate uelewa zaidi juu ya namna ya kuutumia mfumo huu katika majukumu yao ya kila siku kwani kazi zote zinatakuwa zinafanyika kwa njia ya mfumo na sio tena makaratasi.

                                                                               
 

"Tujaribu kujifunza huu mfumo, na tukishamaliza kujifunza tukirudi sisi ni waalimu kwa wale ambao tumewaacha kule, tunategemea mkapeleke hii elimu ambayo mmeipata kwa wengine"

Amezungumza hayo Mkurugenzi Mwanda wakati  akifungua  Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Kesi kwa Wakuu wa Mashtaka wa Wilaya na Waendesha Mashtaka Viongozi wanaoshughulika na Takwimu yaliyoanza  tarehe 22 Februari, 2022 na kumalizika tarehe 25 Februari, 2022 Jijini Dar es salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM).



Pia Mkurugenzi Mwanda alitoa pongezi kwa Wakuu wa Mashtaka wa Wilaya na Waendesha Mashtaka Viongozi kwa utendaji wao wa kazi mzuri kwenye vituo vyao vya kazi katika kuhakikisha taasisi inasonga mbele.

                                                                       


 





 

mzuri kwenye vituo vya kazi katika  kuhakikisha Taasisi inasonga mbele.

Share:

FANYENI KAZI KWA WELEDI NA UADILIFU-SIMBACHAWENE

 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene  amewasihi  Mawakili wote wa Serikali wanaohusika na Uendeshaji wa Mashtaka kutekeleza wajibu wa kazi zao kwa ufanisi, weledi, uadilifu na uzalendo mkubwa.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo wakati  akifungua mafunzo juu ya makosa ya mtandao kwa Mawakili wa Serikali yanayofanyika katika ukumbi wa chuo cha VETA mjini Morogoro kuanzia tarehe 21 hadi 25 Februari,2022.

                                                    


Alisema mara kwa mara Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa akizungumzia suala la  kesi na Upelelezi kuchukua muda mrefu  wakati mashauri yapo mahakamani  na hivyo ameahidi kushirikiana na Mkurugenzi wa Mashtaka kusaidiana naye kutatua changamoto zinazopelekea kuwepo kwa changamoto katika jukumu la kuratibu Upelelezi.


Mhe. Simbachawene alisema yapo malalamiko ya watu kubambikiwa kesi na Upelelezi kuchukua muda mrefu wakati shauri limeshafunguliwa mahakamani na kuwataka Mawakili kwa idhini waliyopewa  na Mkurugenzi wa Mashtaka kutatua changamoto kwa kuratibu upelelezi.

                                                             


Alisema akiwa Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria ataendelea kushirikiana na Wizara zingine, Wakuu wa Taasisi pamoja na wadau wa Maendeleo kuhakikisha utamaduni wa kutoa elimu endelevu kwa wadau wote muhimu wa Haki  Jinai ili kuhakikisha lengo la kudhibiti Uhalifu linatumia.

 Alisema katika mazingira tuliyonayo Sehemu kubwa ya uhalifu unapangwa na unatekelezwa kwa njia ya mtandao kupitia vifaa wezeshi vya mawasiliano kama vile simu na kompyuta ingawa changamoto zake zinaathiri mila,desturi na tamaduni.

 "Sote tunashuhudia namna makosa ya jinai kwa njia ya mtandao yanavyoshamiri katika jamii yetu. Makosa kama vitisho kwa njia ya mtandao, usambazaji wa taarifa za uongo, usambazaji wa picha zenye maudhui ya ngono na Uhalifu kwa njia ya mtandao yameongezeka kwa kiasi kikubwa katika jamii ukilinganisha na miongo miwili iliyopita kutokana na matumizi makubwa ya Mfumo na vifaa vya mawasiliano ambayo kimsingi ndiyo maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Alifafanua kuwa makosa ya kimtandao hayaishii tu katika matukio ya kimtandao kama vile utakatishaji fedha, rushwa, ugaidi, kujipatia mali  au fedha kwa njia ya udanganyifu, kujihusisha na dawa za kulevya na usafirishaji haramu wa  binadamu.

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akimkaribisha mgeni rasmi alimshukuru kwa kukubali kufungua mafunzo hayo aliwataka washiriki kutumia vizuri elimu watakayoipata katika kuboresha utendaji kazi na kuwafundisha kuwarithisha wengine ambao hawakupata nafasi ya kushiriki.

                                                         


 Mafunzo  ya juu ya sheria ya makosa ya mtandao, upelelezi na uendeshaji kesi dhidi ya Makosa ya mtandao kwa Mawakili wa Serikali yanafanyika katika chuo cha VETA mjini Morogoro kuanzia tarehe 21 hadi 25 Februari, 2022.

Share:

MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA KATIKA MASUALA YA KESI KWA WAKUU WA MASHTAKA WA MIKOA NA WILAYA PAMOJA NA WAENDESHA MASHTAKA VIONGOZI

 


Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa Mashtaka Jijini Mwanza Bw. Idrisa Swalehe akifundisha namna ya kusajili taarifa za kesi kwenye mfumo katika Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya kesi kwa Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa na Wilaya pamoja na Waendesha Mashtaka Viongozi yanayofanyika Jijini Dar es Salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)




Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya kesi wakimsikiliza Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Jijini Mwanza Bw. Idrisa Swalehe wakati akifundisha katika mafunzo hayo yanayofanyika Jijini Dar es salaam





Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya kesi wakimsikiliza Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Jijini Mwanza Bw. Idrisa Swalehe wakati akifundisha katika mafunzo hayo yanayofanyika Jijini Dar es salaam


Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .