Waziri
Wa Katiba na Sheria Mhe. Damas Ndumbaro
amezindua kikosi kazi cha ulinzi kwa watoto dhidi ya biashara haramu ya
Usafirishaji wa binadamu.
Kikosi
kazi hicho kimeanzishwa chini ya Mradi wa kupambana na Uhalifu mkubwa wa
kupangwa ( Serious Organised Crime- SOC), ambacho kitatekelezwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizindua
kikosi kazi hicho, Waziri wa Katiba na Sheria, leo Julai 21, 2022 Dkt. Damas
Ndumbaro, amesema athari ya uhalifu mkubwa wa kupangwa ni kubwa na inakuwa ya
kushtukiza.
"Sisi,
Tanzania tunayo mifano hai kuhusu madhara ya uhalifu wa aina hii, kwa mfano
uripuaji wa mabomu katika ubalozi wa Marekani uliotekelezwa hapa kwetu, Kenya
na Uganda kwa wakati mmoja." Amesema Dkt.
Ndumbaro na kuongeza
Amesema
kutokana na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika mapambano
dhidi ya ukatili na udhalilishaji wa wanawake
na watoto, wameanza kushuhudia kuibuka kwa taarifa kuhusu uhalifu wa aina hiyo
katika jamii na umeonesha bayana juu ya kazi kubwa iliyopo katika kukabiliana
na janga hilo.
"
Kwa maelezo hayo ninajenga hoja kwamba mradi huu wa kupambana na uhalifu mkubwa
wa kupangwa hasa ule wa usafirishaji haramu wa Binadamu, unyonyaji na
udhalilishaji wa watoto kingono ni muhimu sana na umekuja kwa wakati unaofaa
katika nchi yetu" amesema Dkt. Ndumbaro.
Kwa
msingi huo, sisi sote tuliopewa dhamana ya kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa
kwa Makosa ya Biashara Haramu ya Binadamu, Ukatili na Udhalilishaji wa Watoto
Kingono na Uhalifu Unaovuka Mipaka ya Nchi katika jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, hatuna budi kuitumia fursa hii ili kuleta tija na ufanisi katika
utekelezaji wa majukumu yetu ya kuhudumia taifa hili. Huu ni wakati wa kubuni
mbinu mbali mbali zitakazoweza kubainisha hila na ghilba za wahalifu pia
kubainisha changamoto zinazowakabili wapambanaji wa kazi hii na kutafuta mbinu
muwafaka za kukabiliana nazo ili kufikia malengo tuliojiwekea.
Ubunifu
wa mbinu mpya ni lazima utekelezwe sambamba na kuongeza uwezo wetu wa
teknolojia ya mitandao ambayo baadhi ya wakati inatumika vibaya ili
kuwanufaisha wahalifu wanaotaka mafanikio bila ya kufuata na kuheshimu sheria
za ndani ya nchi na kimataifa.
"
Kwa msingi huu sisi sote tuliopewa dhamana ya kupambana na uhalifu mkubwa wa
kupangwa kwa Makosa ya Biashara Haramu ya Binadamu, Ukatili na Udhalilishaji wa
Watoto Kingono na Uhalifu Unaovuka Mipaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, hatuna budi kuitumia fursa hii ili kuleta tija na ufanisi katika
utekelezaji wa majukumu yetu ya kuhudumia taifa hili." Amesema Dk Ndumbaro
na kusisitiza
"
Huu ni wakati wa kubuni mbinu mbali mbali zitakazoweza kubainisha hila na
ghilba za wahalifu pia kubainisha changamoto zinazowakabili wapambanaji wa kazi
hii na kutafuta mbinu muwafaka za kukabiliana nazo ili kufikia malengo
tuliojiwekea" amesisitiza.
Amesema
Ubunifu wa mbinu mpya ni lazima utekelezwe sambamba na kuongeza uwezo wa
teknolojia ya mitandao ambayo baadhi ya wakati inatumika vibaya ili
kuwanufaisha wahalifu wanaotaka mafanikio bila ya kufuata na kuheshimu sheria
za ndani ya nchi na kimataifa.
Akizungumzumzia
mradi huu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania ( DPP) Bw. Slyvester
Mwakitalu amesemea mradi huo ni wa miaka minne kuanzia Desemba, 2021 hadi
Desemba 2025 na unatekelezwa kwa gharama ya dola za Kimarekani 6,434,320 ambapo
zitatumika kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
"Mradi
huu unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza na Jumuiya ya Umoja wa
Nchi za Ulaya kupitia Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
likishirikiana na UNICEF pamoja na Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM)"
amesema Mwakitalu.
Mwakitalu
amesema mradi huo umelenga kujenga uwezo wa kiutendaji kwa taasisi za Serikali
zinazohusika katika utekelezaji wa sheria za kupambana na uhalifu mkubwa wa
kupangwa ambapo kwa Tanzania Bara utajikita zaidi katika makosa ya biashara
haramu ya usafirishaji wa binadamu na udhalilishaji (unyanyasaji) wa watoto.
"Lengo
kuu la mradi huu wa SOC ni kuvijengea uwezo vyombo vya ulinzi na usalama
vinavyohusika katika utekelezaji wa sheria za mapambano dhidi ya uhalifu mkubwa
wa kupangwa hasa katika nyanja za upelelezi, uendeshaji wa mashtaka na ulinzi
kwa wahanga na manusura" Amesema Mwakitalu.
Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima amesema uzinduzi wa kikosi hicho umekuja wakati muafaka wakati Serikali ikiendelea kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.











No comments:
Post a Comment