Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (Mb)Florent Kyombo akieleza namna ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga litakavyosaidia kutoa huduma kwa karibu kwa wananchi.Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Katiba na Sheria leo tarehe 15 Machi, 2023 imetembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga ambalo linaendelea kujengwa kwa lengo la kurahisisha zaidi huduma za kimashtaka kwa wananchi.
Akitoa taarifa za ujenzi wa jengo hilo kwa kamati hiyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amesema kuwa mnamo tarehe 26 Septemba, 2022 Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliingia Mkataba na kampuni ya Mkandarasi Eliroi Construction kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.15 ikijumuisha ongezeko la thamani VAT.
Mhe. Gekul amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya muda wa miezi 8 ambapo ulianza kutekelezwa tarehe 22 Novemba, 2022 mbapo unataraji kukamilika June 22 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 35.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul,akitoa taarifa za ujenzi wa jengo hilo kwa kamati hiyo iliyoembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Aidha Naibu Waziri Mhe. Gekul ameongeza kwa kusema kuwa mpaka sasa Mkandarasi amekwisha lipwa fedha za awali kiasi cha shilingi milioni 323 kati ya bilioni 2.15 huku Mkandarasi Mshauri Mwelekezi wa mradi huo Water Institute kawazulite maombi ya kulipwa kiasi cha shilingi milioni 335.5
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu ameishukuru Kamati hiyo kwa juhudi zake kubwa za kuipigania Ofisi hiyo ambapo kwa mwaka huu wa fedha unaoendelea jumla ya mikoa sita imepatiwa fedha za ujenzi wa Ofisi ikiwa ni pamoja na Shinyanga, Geita, Manyara, Rukwa, Katavi na Njombe na kufanya idadi ya ofisi zinazojengwa kufikia kumi.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu akieleza namna kamati hiyo imekuwa msaada wa upatikanaji wa fedha za ujenzi wa Ofisi hiyo.
Mkurugenzi Mwakitalu ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Christine Mndeme kwa kuwapatia eneo la Kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo ambayo itasaidia na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii juu ya masuala ya Mashtaka ambapo amesema eneo hilo awali ilipewa taasisi nyingine.
Mkurugenzi wa Mashtaka aliendelea kueleza kuwa ujenzi huo utakapokamilika utarahisisha utaoaji wa huduma kwa jamii ambapo watumishi watakuwa na sehemu bora na mazingira rafiki ya utaoji wa huduma.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christine Mndeme ameihadi kamati hiyo kuwa atahakikisha anasimamia kwa ukaribu ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na kuleta tija iliyokusudiwa ya utaoji wa huduma kwa jamii.
Kwanza Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Christine Mndeme akiwa pamoja na kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala , Katiba na Sheria.
Mndeme ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo kwani ni muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga huku akiongeza kwa kusema kuwa mradi huo unakwenda kubadili mandhari ya Mkoa wa Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (Mb)Florent Kyombo amemtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuwa muda aliyopewa mpaka sasa ni zaidi ya miezi minne mradi huo bado uko asilimia 35 ambapo ulipaswa kuwa asilimia zaidi ya 50.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (Mb)Florent Kyombo akisikiliza maelezo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Kyombo amesema kuwa lengo la ujenzi wa Ofisi hizo ni kusogeza huduma karibu na wananchi hivyo usimamizi Madhubuti unapaswa kuwepo ili kuondoa mikwamo isiyokuwa na tija katika ujenzi huo.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu akisalimiana na mmoja wa mafundi wanaojenga jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Aidha Kyombo ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itakayosaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Meneja Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Ezrael Masawe akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala, Katiba na Sheria namna ambavyo jeno hilo litakavyojengwa.
Kamati hiyo iko katika ziara ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
@NPS-HQ
@NPS-Shinyanga






No comments:
Post a Comment