• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

NAIBU KATIBU MKUU KATIBA NA SHERIA AFUNGUA JENGO JIPYA LA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu leo tarehe 16 Machi, 2024 amefungua jengo jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Shinyanga lililopo katika eneo la Uzunguni.

Akizungumza katika hafla ya  ufunguzi huo, Naibu Katibu Mkuu amewataka watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuimairisha na kuboresha utendaji kazi kutokana na Serikali kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa kujenga majengo ya kisasa ili waweze kutoa huduma bora za kimashtaka kwa wananchi.

Pia Naibu Katibu Mkuu amefungua jengo jipya la  Ofisi  ya Taifa ya  Mashtaka  Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Mikoa mitano ambayo majengo yake yamekamilika ikiwemo Mkoa wa Pwani, Ilala, Manyara, Katavi na Rukwa.Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Slyvester Mwakitalu amesema kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Shinyanga na maeneo  mengine itasaidia kuboresha na kuimarisha utendaji wa shughuli za uendeshaji wa Mashtaka

Mwakitalu amesema mpaka sasa wamekwisha fungua Ofisi za Kimashtaka katika Wilaya 92 za Tanzania bara hali inayochangia kusogeza karibu huduma kwa  wananchi na kuwaondolewa usumbufu wa kusaifiri umbali mrefu.

Aidha Mwakitalu amesema mradi wa Shinyanga umegharimu bilioni 2.153 hadi kukamilika kwake ikijumuisha thamani za ndani ya ofisi hiyo pamoja na miundo mbinu yote.Kwa upande wao baaadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo akiwemo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga Mhe. Jaji Frank Maimbali amewataka Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuongeza kasi na ufanisi katika uendeshaji wa Mashataka kwa kuwa mazingira ya kazi yameboreshwa na kuimarishwa zaidi kupitia Serikaliya awamu ya sita ya rais Samia Suluhu Hassan.

Naye Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Boniface Butondo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga  amepongeza kwa dhati hatua zilizopigwa za kuimairisha ofisi za Mashataka katika mikoa mbalimbali hivyo matarajio ya kamati ni kuona mashauri mengi yana kwenda kwa kasi kubwa huku akisema kuwa kamati yao iko tayari kupitisha maombi yote ya bajeti  yanayowasilishwa kwao.Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) ambaye ni Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Bi  Stella Butabihilwa amesema kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuimairisha ushirikiano wake na Ofisi ya Taifa ya Mashataka kwa kuwa wamekuwa wakishirikiana  kwa hali na mali.

Naye  Mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA)  ambaye ni Kamishna wa Huduma za Sheria wa mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bi.  Veronica Matikila amesema jitihada kubwa zinafanywa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kusogeza huduma karibu na wananchi 

Bi. Veronica amesema uwepo wa ofisi hiyo ni tija kwao kwa kuwa wamekuwa wakitumia  katika shughuli zao na kuwaletea tija kubwa.

Ufunguzi huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya mpango makakati wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ya kusogeza huduma karibu na Wananchi. 

Share:

WANAWAKE KUTOKA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA WASHIRIKI KUFANYA MATENDO YA HURUMA.

 Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika tarehe 8 Machi, 2024 wanawake kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  Makao Makuu Jijini Dodoma wameshiriki kwa pamoja kutoa Misaada mbalimbali kwenye Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. 

Akizungumza baada ya kukabidhi misaada hiyo  Hospitalini hapo leo tarehe 6 Machi, 2024 Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Chivanenda Luwongo amesema wanawake kutoka Idara na Vitengo mbalimbali vya Ofisi ya taifa ya Mashtaka, wamechangishana fedha ambazo wamezitumia kununulia mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kuwapa msaada wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo ya Rufaa.

Bi. Luwongo amesema kuwa wametoa matibabu kwa wagonjwa wanaume 3 na wanawake 2 waliolazwa kwa muda mrefu ambapo watagharimia matibabu yao kwa muda wa siku 7 kwa kuwapa Dawa, Gharama za mtoto mmoja anayefanyiwa upasuaji pamoja na dawa za siku tatu pamoja na wagonjwa wenye mahitaji maalumu.

Ametaja misaada mingine  kuwa ni pamoja na Sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kupaka, Asali kwa ajili ya wagonjwa wenye majeraha na Maziwa kwa ajili ya watoto wadogo wanaotibiwa na kuhudumiwa hospitalini hapo bila kuwa na wazazi.



Kwa upande wake Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Bw.  Stanley Mahundo ameishukuru Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kuchagua Hospitali hiyo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia  wanawake na watoto wanaougua maradhi mbalimbali huku akiahidi misaada hiyo kuwafikia walengwa kama ilivyokusudiwa. 

“Baadhi ya wanawake na watoto hawana ndugu wa kuwahudumia ambao wanapata matibabu hapa hivyo kwa wanawake wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kutoa misaada hii mmefanya jambo la muhimu kwani misaada hii itawasadia kwa kiwango kikubwa." Amebainisha hayo Muuguzi Mfawidhi. 



Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatafanyika Kitaifa tarehe 8 Machi, 2024 katika Wilaya ya  Chamwino, Makao Makuu Jijini Dodoma.




Share:

DPP AFUNGUA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amefungua  Kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kinachofanyika tarehe 10 hadi 11 Machi, 2024 Mkoani Pwani.



Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwani kinalenga kukumbushana,  kujadiliana na kupanga maazimio mbalimbali yatakayowezesha utekelezaji wa majukumu yao kuwa rahisi ili kuweza  kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia.

"Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni ofisi nyeti kwa maana tunatoa huduma na kugusa haki za wananchi, maamuzi yetu yanakwenda kugusa haki za watu, tusipokuwa makini na kufanya kazi hii kwa weledi na kwa uaminifu kuna watu tutawaumiza." Amefafanua hayo Mkurugenzi Mwakitalu.

Pia Mkurugenzi wa Mashtaka ameeleza kuwa kupitia kikao kazi hicho watajadiliana na kutafuta suluhu yale maeneo ambayo yamebeba changamoto nyingi zaidi, na maazimio yatakayotolewa na kukubaliana kupitia kikao hicho yazingatiwe na kutelezwa kwa wakati.

"Tuzitumie siku mbili hizi vizuri ili tuweze kujadiliana na tutoke na maazimio ya pamoja, na kwa kufanya hivyo basi tutaendelea kuimairisha ofisi yetu na utoaji wetu wa huduma kwa watu ambao tumepewa jukumu la kuwahudumia." Ameyasema hayo DPP

Sambamba na hilo Mkurugenzi wa Mashtaka amewasisitiza watumishi ambao wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NEST) kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kufanya manunuzi yale ambayo yatasaidia katika kuimairisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Tunatumia fedha za umma na fedha hizi lazima zitumike kwa utaratibu na kwa miongozo ya fedha za umma iliyopo." Amebainisha hayo Mkurugenzi Mwakitalu.



Share:

"Tumieni Mfumo wa NEST ili kuepukana na Changamoto za Manunuzi." Kaimu Naibu DPP

 Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bi. Javelin Rugaihuruza amewataka Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuutumia  Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NEST) kwa lengo la kuondokana na changamoto za manunuzi walizokuwa wakikabiliana nazo katika kununua mahitaji mbalimbali ya kiofisi yanayohitajika kufanyika kupitia Mfumo huo.

Kaimu Naibu DPP amebainisha hayo wakati akifungu Mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NEST) yaliyofanyika tarehe 9 Machi, 2024 Mkoani Pwani.

"Niwasihi mtumie siku ya leo kikamilifu ili kuweza kujifunza na kufahamu vema mfumo huu na baada ya kutoka hapa natumaini changamoto zilizokuwepo zitaondoka." Amefafanua hayo Kaimu Naibu Javelin.

Mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NEST) yametolewa kwa Wahasibu na Watumishi wengine wanaofanya kazi za Manunuzi katika Mikoa.



Share:

DPP ASISITIZA JUU YA MATUMIZI YA MFUMO KWA MAKATIBU SHERIA NA WATUNZA KUMBUKUMBU.

 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amewasisitiza Makatibu Sheria pamoja na Watunza Kumbukumbu kuusimamia na kuutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya, Kuchakata na Kutunza Kumbukumbu za Kesi za Jinai (Case Management Information System) kwa lengo la kuweza kuwasaidia kupata takwimu zilizo sahihi za kesi zitakazosaidia katika kufanya maamuzi na kupanga mipango ya maendeleo. 

Mkurugenzi Mwakitalu amebainisha hayo wakati akifungua Kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu Sheria pamoja na Watunza Kumbukumbu kinachofanyika tarehe 29 Februari, 2024 hadi 1 Machi, 2024 Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa kikao kazi hicho kimelenga kufahamiana, kubadilishana mawazo na kukumbushana majukumu yao kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa na Wawezeshaji.

Aidha Mkurugenzi wa Mashtaka amewataka washiriki hao kutumia fulsa hiyo kujadiliana na kutafuta suluhu ya changamoto ambazo wanakabiliana nazo wakati wa utendaji kazi wao  ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Tunataka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iwe ni ofisi bora zaidi katika maeneo yote ya kiutendaji hususani katika Usimamizi na Uendeshaji wa Kesi. Kila mmoja atekeleze majukumu yake kwa uadilifu, bidii nakwa nguvu zake zote." Ameyasema hayo Mkurugenzi Mwakitalu.






Share:

DPP AMEWATAKA WAAJIRIWA WAPYA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA.

 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amewataka Waajiriwa Wapya ambao ni Makatibu Sheria 36 na Mtakwimu 1 kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo, miiko na maadili ya utumishi wa umma kwa lengo la kuisaidia Taasisi katika uendeshaji wa kazi za kiofisi.

Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo wakati akifungua Mafunzo Elekezi kwa Waajiriwa Wapya wa Ofisi ya  Taifa ya Mashtaka (Induction Course)  yanayofanyika tarehe 26 hadi 28 Februari, 2024 Jijini Dodoma.

Pia Mkurugenzi Mwakitalu ameeleza kuwa Makatibu Sheria ndio nguzo na msingi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo majukumu yake yanagusa haki za watu, hivyo maamuzi yanayofanywa na ofisi hiyo yanagusa haki za wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Kampasi ya Singida Dkt. Hamisi Amani ametoa pongezi kwa uongozi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kutenga muda na fedha kwa ajili ya kuwagharamikia watumishi wapya katika kufanya mafunzo elekezi ya awali. 

Dkt. Hamisi amesema kuwa utekelezaji wa Mafunzo Elekezi ni takwa la kisheria na kwa mujibu wa waraka wa utumishi No.5 wa mwaka 2011 umeelekeza kwamba Waajiri wote nchini wanapopata watumishi wapya wanapaswa kuwapeleka katika mafunzo elekezi ya awali.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha Waajiriwa Wapya kuuelewa utumishi wa umma na misingi yake zkiwemo sera, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za utendaji kazi serikalini.

Sambamba na hilo Dkt. Hamisi amebainisha kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha Waajiriwa Wapya kuyafahamu majukumu yao kwa ujumla wakiwa kama watumishi wa umma, wajibu na namna ya kuifahamu serikali jinsi inavyofanya kazi, juu ya taratibu za utendaji kazi serikalini, maadili, nidhamu, uadilifu na ustahimilifu.

"Kwa kada ya Makatibu Sheria wanayo nafasi kubwa ya kutekeleza jukumu la serikali la kuhudumia wananchi kwasababu mnapotekeleza majukumu yenu mnakutana moja kwa moja na wananchi hivyo mna kila sababu ya kuzingatia nidhamu, uadilifu na kuwa wastahimilifu kwasababu ya vishawishi mbalimbali vinavyoweza kutokea." Amefafanua hayo Dkt. Amani.

Aidha Mkurugenzi Amani ameeleza kuwa Serikalini imeyapa umuhimu mkubwa sana mafunzo hayo elekezi ya awali kwasababu watumishi ambao wanaingia moja kwa moja na wakaendelea kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupatiwa mafunzo hayo inatarajiwa hawataweza kutekeleza majukumu kwa ufanisi zaidi na kuwa na utendaji kazi hafifu, uvunjaji wa taratibu za utendaji kazi na migogoro katika utendaji kazi.



Share:

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AZINDUA MIONGOZO MIWILI KUTOKA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amefanya uzinduzi wa Miongozo ya Ushughulikiaji wa Kesi za Wanyamapori na Misitu pamoja na Kesi za Uvuvi Haramu kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi.

Amezindua miongozo hiyo Jijini Arusha tarehe 19 Februari, 2024 wakati wa hafla ya uzinduzi wa miongozo hiyo katika mkutano wa mafunzo  kwa Wapelelezi na Waendesha Mashtaka nchini.

Dkt.Chana amesema miongozo hiyo itawasaidia wadau wa kesi hizo kuziendesha kwa haki na kuleta manufaa kwa rasilimali nchini.

"Jukumu la kulinda rasilimali zetu ni letu sisi wenyewe hivyo naamini wapelelezi na waendesha mashtaka kwa sasa mtasaidia kukomesha ujangili wa wanyamapori wetu, uvuvi haramu kwenye maziwa na bahari, lakini pia kukomesha uharibifu wa misitu yetu." Amezungumza hayo Mhe. Waziri

Aidha alisema rasilimali zilizopo nchini  zinachangia pato la Taifa na fedha hizo zinafanikisha kuendesha shughuli mbalimbali za maendelo.

Amesema baada ya uzinduzi huo anawatahadharisha wanaojihusisha na ujangili wa rasilimali za Taifa kuacha kwani wadau wa maeneo hayo wamejipanga vizuri kuhakikisha wana komesha tabia hizo.

Dkt. Chana amesema Taifa haliwezi kuacha baadhi ya watu wakiendelea kuvuna rasilimali za nchi kwa manufaa yao peke yao, bila kufuata sheria  ni lazima wadhibitiwe.

Awali akimakaribisha mgeni rasmi Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chama, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Sylvester Mwakitalu alisema uzinduzi wa miongozo hiyo ina manufaa makubwa kwa maliasili nchini.

"Tumeona tuhuhishe muongozo wa Ushughulikiaji wa Kesi za  Wanyamapori na Misitu na Muongozo wa Kesi za  Uvuvi haramu sababu tumeona tusipokua makini katika kulinda rasilimali zetu kama bahari na maziwa yatabaki tupu kutokana na uvunaji haramu wa mazao haya unavyozidi kushamiri." Amefafanua hayo Mkurugenzi Mwakitalu.

Alisema kuna wakati makosa hayo yanafanywa kwa kupanga  kitaifa na kimataifa, hivyo kupitia miongozo hiyo itawasaidia kudhibidi uhalifu huo ndani na nje ya nchi.

Pia katika ukusanyaji wa ushahidi  wa makosa hayo kupitia miongozo hiyo itasaidia  kufanywa kisanyansi, teknolojia na kielekroniki na mafunzo hayo yatatolewa kwa wadau wa sekta hiyo nchi nzima kwa  Waendesha Mashtaka kutoka Taasisi za utalii kama TANAPA, TAWA, NCAA, TFS, POLISI na TAKUKURU

Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashataka nchini  Bi. Javelin Rugaihuruza alisema  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeona kuna umuhimu wa kuandaa mafunzo hayo ili kufundisha wadau mbinu mpya zinazotumiwa na wahalifu wa rasilimali nchini  kwa manufaa ya Taifa.

Kwa upande wake Katto Wambua kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuzuia Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC)  ambao ndiyo wameandaa miongozo hiyo na kuwezesha mafunzo kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelzi nchini alisema watatengeneza APP itakayowezesha  kuisoma miongozo hiyo kwenye simu, pamoja na kusoma miongozo ya nchi zingine.




Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .