Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bi. Bibiana Kileo,amekutana na kuzungumza na Waajiriwa Wapya 60 wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kutoka kada mbalimbali (Mawakili, Madereva na Mkutubi) kwa lengo la kuwakaribisha na kufahamiana.
Waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wamewasili Makao Makuu Jijini Dodoma tarehe 19 Septemba, 2024 kwa lengo la kupatiwa barua zao za ajira ili kwenda kuanza kazi rasmi katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa.
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka amewaasa Waajiriwa Wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uadilifu,bidii, na uzalendo mara wafikapo katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa ili kuleta chachu katika utendaji kwa ofisi na jamii yote kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Simon Ntobbi akizungumza na Waajiriwa Wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kuwataka kwenda kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia misingi ya haki pamoja na kufuata sheria na kanuni zote za utumishi wa umma.
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bi. Bibiana Kileo akiwa katika picha ya pamoja na Waajiriwa Wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka mara baada ya kuwasili Makao Makuu Jijini Dodoma tarehe 19 Septemba, 2024 kwa lengo la kupatiwa barua zao za ajira ili kwenda kuanza kazi rasmi
Waajiriwa Wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bi. Bibiana Kileo wakati akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika tarehe 19 Septemba, 2024 Jijini Dodoma






No comments:
Post a Comment