
Kesi hiyo imeendeshwa na Mawakili wa Serikali Faraja Nchimbi, Salim Msemo, Costantine Kakula, Candid Nasua pamoja na Tully Helela.
Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.
UKATAJI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

Kesi hiyo imeendeshwa na Mawakili wa Serikali Faraja Nchimbi, Salim Msemo, Costantine Kakula, Candid Nasua pamoja na Tully Helela.

Pichani ni Mkurugezi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga.
DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ni kosa kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na kampuni ya Qnet kisha kudai wametapeliwa kwamba kufanya hivyo ni kosa.
Ameeleza hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ikiwa ni siku mbili baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita kurejesha Sh5.48 milioni kwa mwalimu Rose Mgomba wa Shule ya Msingi Lukaranga aliyedai kutapeliwa.
Wasiwasi watanda kampuni ya Qnet
Katika maelezo yake, Mganga alisema urejeshwaji wa fedha hizo ni kosa kisheria kwa sababu biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni upatu haramu.
Mbali na kukemea suala hilo, alizitaka taasisi zinazofanya uchunguzi kuhusiana na sakata la kampuni ya Qnet kushirikiana kwani wanajenga nyumba moja.
Alisema shughuli inayoendeshwa na kampuni ya Qnet ni upatu na tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ameanza upelelezi kuhusiana na sakata hilo.

Mahakama pia imemuhukumu mshtakiwa kulipa faini ya shilingi Milioni tano ama akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitano Gerezani.
Aidha Mahakama imeamuru fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 5 na milioni 456 na laki 480.41 (5,456,480.41) ambazo zipo katika akaunti za mshtakiwa zitaifishwe na kuwa mali ya serikali.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Godfrey Isaya amesema mahakama imezingatia kwamba mshtakiwa amekiri mwenyewe makosa yake na ni mkosaji wa mara ya kwanza na wameangalia makubaliano hivyo hakuna sababu ya kumpa adhabu kali.
Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, wamedai mshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) wameingia makubaliano , katika mashtaka saba aliyokuwa anakabiliwa nayo yameondolewa na wamebakisha mashtaka mawili.
Akisomewa mashtaka hayo mawili, katika shtaka la kusimamia biashara ya upatu inadaiwa kati ya Januari 2018 na Mei, mwaka huu, maeneo tofauti Jijini Dar ea Salaam alijihusisha na biashara hiyo kwa kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma kwa kujifanya watafanya ujasiriamali wa ufugaji kuku na watapata faida asilimia 70 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji wa uwekezaji wa miezi sita kiasi ambacho ni kikubwa kibiashara kuliko mtaji uliokusanywa.
katika shtaka la pili mshtakiwa anadaiwa kukubali kupokea muamala wa kifedha kutoka kwa umma kiasi cha Sh bilioni 17.
Awali mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka saba ambapo mbali na hayo mawili yalikuwepo mashtaka matano ya utakatishaji fedha.
Kabla ya kusomwa kwa adhabu, Wakili Kadushi aliieleza mahakama kuwa, hawana kumbukumbu za makosa ya nyuma ya washitakiwa hivyo, ameiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria huku ikizingatia hatua ya makubaliano waliyofikia.
Upande wa wakili wa Utetezi, Augustine Shio ameiomba mahakama impunguzie mshtakiwa wake adhabu kwani amekiri makosa yake mwenyewe na pia ana familia ya wake watatu ambao kila mmoja ana mtoto mchanga na wote wanamtegemea yeye.

Mwonekano wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma likionekana kwa Mbele
Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Wilaya ya Kasulu katika kesi Na.32/2020 mbele ya Mhe. Jaji A. Matuma imewatia hatiani washtakiwa Enock Antony pamoja na baba yake Antony Kinanila na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kwa makusudi Cosmas Pastory.
Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 26, Desemba 2018 katika Kijiji cha Katundu Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa walimuua marehemu kwa sababu ya mgogoro wa ardhi na kwamba marehemu alikuwa anajidai kuwa yeye ni tajiri. Washtakiwa walienda kwa marehemu usiku wakamkuta amekaa nje ya nyumba yake na familia yake ndipo wakamkamata, wakamlaza chini chali kisha wakamchoma mkuki kifuani mbele ya familia yake.
Kesi hiyo imeendeshwa na Mawakili wa Serikali Robert Magige na Edna Makala.
Jumla ya Mahabusu Sabini na mbili kati yao wanaume 62 na wanawake 10 wamefutiwa Mashtaka na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga baada ya kutembelea gereza la Karanga, Moshi kujionea hali halisi ya gereza pamoja na kuwasikiliza mahabusu
Mkurugenzi wa Mashtaka amefanya tukio hilo leo baada ya kukagua na kujionea hali halisi ya gereza hilo ambapo alipata pia nafasi ya kuwasilikiliza wafungwa na Mahabusu.
Akizungumza baada ya kuwafutia Mashtaka Mahabusu hao Bwana Mganga aliwataka watakaporudi uraiani kuwa raia wema na wale wanaobaki gerezani kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu ili awasamehe dhambi walizotenda na kufungua mlango wa rehema.
Aidha aliwaonya kutorudia kufanya Uhalifu. "Sitegemei kuwakuta mmefanya Uhalifu tena baada ya kutoka hapa, ole wenu mrudie. Kama kuna miongoni mwenu ambaye anajua hawezi kuacha Uhalifu aombe abaki humu ndani" Alisisitiza Bw. Mganga
Mkurugenzi wa Mashtaka alitumia nafasi hiyo kuwaonya watu wanaotishia mashahidi na wanaotaka kupata haki kwa njia ya Udanganyifu kwakuwa akikamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Mashtaka aliahidi kuchukua changamoto zilizotolewa na Mahabusu na wafungwa na kuahidi kuzifanyia kazi.
Mkurugenzi wa Mashtaka na timu ya viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wapo katika Mikoa mbalimbali kukagua namna shughuli za uendeshaji wa shughuli za Mashtaka unavyotekelezwa ikiwapo kutembelea Magereza, mahabusu na kuwatembelea wadau muhimu wanaoshirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Haki Jinai.
![]() |
Mahakama ya Wilaya ya Iringa katika Kesi Na. 139/2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Iringa imewatia hatiani washtakiwa watatu Richard Mbundamila, Taford Kalinga na Haruni Boniface Mgawo na kuwahukumu kifungo cha miaka thelathini (30) jela kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha, kutoroka chini ya Ulinzi na Kujeruhi.
Watuhumiwa hao wamehukumiwa kifungo cha miaka thelathini (30) jela kwa kosa la kwanza ambalo ni unyang'anyi wa kutumia silaha na miaka Saba kwa kila kosa kwa makosa ya Kujeruhi na kutoroka chini ya Ulinzi.
Katika kosa hilo upande wa Mashtaka uliwasilisha vidhibiti kadhaa vikiwemo bunduki aina ya Uzi gun, mashoka Saba, Mapanga matano, risasi mbili, maganda mawili ya risasi pamoja nasare za wafungwa tatu.
Ilielezwa Mahakamani hapo kuwa watuhumiwa wa
likuwa wafungwa waliokuwa wakitumikia vifungo mbalimbali ambapo siku ya tukio walienda kutafuta kuni na wakiwa huko walimvamia askari aliyekuwa anawalinda na kumkata panga kichwani kisha kumnyang'anya bunduki na kuondoka nayo.
Katika tukio hilo mtuhumiwa mmoja aliuawa katika mapambano akiwa huko Njombe ambapo silaha iliyoibiwa ilikombolewa
Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Edna Mwangulumba na Brandina Manyanda