MKURUGENZI WA MASHTAKA (DPP) BISWALO MGANGA AFAFANUA KUHUSU UPATU


Pichani ni Mkurugezi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga. 

DAR ES SALAAM 

  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ni kosa kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na kampuni ya Qnet kisha kudai wametapeliwa kwamba kufanya hivyo ni kosa.

Ameeleza hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ikiwa ni siku mbili baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita kurejesha Sh5.48 milioni kwa mwalimu Rose Mgomba wa Shule ya Msingi Lukaranga aliyedai kutapeliwa.

Wasiwasi watanda kampuni ya Qnet

Katika maelezo yake, Mganga alisema urejeshwaji wa fedha hizo ni kosa kisheria kwa sababu biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni upatu haramu.

Mbali na kukemea suala hilo, alizitaka taasisi zinazofanya uchunguzi kuhusiana na sakata la kampuni ya Qnet kushirikiana kwani wanajenga nyumba moja.

Alisema shughuli inayoendeshwa na kampuni ya Qnet ni upatu na tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ameanza upelelezi kuhusiana na sakata hilo.

Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .