WANANCHI WATAADHALISHWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA UPATU

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini akiwa na Wakuregenzi wa idara mbalimbali toka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Na Mwandishi NPS 

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw Biswalo Mganga amewataka Wananchi kujiepusha na kujihusisha na biashara haramu ya upatu kwakuwa ni kosa la Jinai kwa mhamasishaji na mtoaji fedha.

Bw. Mganga ameyasema hayo leo katika kikao chake na vyombo vya habari kilichofanyika jijini Dodoma ambacho alikitumia kuelekeza na kuelimisha umma kutokana na kuibuka upya kwa biashara ya upatu unaojitokeza katika siku za hivi karibuni.

Alisema vitendo vya ushiriki katika biashara haramu ya upatu ( pyramid schemes) vinakiuka masharti ya Sheria ya Benki na Taasisi za Kifedha Na.5 ya Mwaka 2006 inayokataza mtu yeyote kupokea.miamala ya Kifedha kutoka kwa umma bila leseni na ni kosa la Jinai siyo tu kwa anayehamasisha na kupokea fedha bali hata kwa wanaotoa fedha hizo.

Alisema wanaofanya na kushiriki katika biashara hiyo wapo katika hatari ya kupoteza fedha zao pamoja na kushtakiwa Mahakamani kwa kosa la kushiriki biashara haramu ya upatu.

Alisema Umma unakumbushwa kuwa mipango.kama hii ya kilaghai imewahi kujitokeza siku za nyuma na kusababisha wananchi wengi kupoteza fedha zao ambapo aliitaja baadhi ya mipango hiyo danganyifu kuwa ni.pamoja na Rifaro Africa, IMS, D9, miradi ya kuku kupitia kampuni ya Mr. Kuku na Development Enterpreneurship Initiative ( DECI).

Alisema mipango hiyo kwasasa imeibuka na sura Mpya kama Biashara y Kimtandao ambapo wananchi wanaalikwa kushiriki kwa kuwashawishi wengine kujiunga

Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na vifungu vya 8 na 9(1)(c) vya Sheria ya Usimamizi wa Mashtaka (Sura 430 Marejeo 2019) 

ambapo ametoa maelekezo ya vyombo vyote vya Upelelezi kutorejesha fedha kwa watu walioshiriki katika makosa ya upatu ambapo ameeleza kuwa utaratibu wa kurejesha mali za wahanga au kutaifisha mali zinazohusiana na Uhalifu umeainishwa katika Sheria mbalimbali na hivyo kuwataka wale wote wanaotaka kurejesha fedha au mali zinazohusiana na Uhalifu kwa wahanga kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria

 

Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .