DPP AWATAKA MAWAKILI WA SERIKALI NCHINI KUFUATA MAADILI KWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA RUSHWA

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga akifungua mafunzo kwa  mawakili 29 wa serikali toka mikoa yote nchini  juu ya kuwajengea uwezo wa Utendaji kazi. 

Mashtaka wa Serikali wameaswa kufanya kazi zao kwa kufuata maadili Ili kuepusha malalamiko kutoka kwa Umma juu ya utendaji kazi wao.

Akizungumza Machi 16, 2021 Jijini Mwanza wakati akifungua mafunzo ya mawakili 39 kutoka katika  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mikoa na Wilaya  ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga amesema kuwa mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo wa utendaji kazi, katika uendeshaji wa kesi za rushwa, utakatishaji fedha na udanganyifu kwa njia ya kimtandao.

Biswalo amesema Dunia ya sasa inaendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia hivyo lengo la kuwakutanisha mawakili hawa ni  kuwajengea uwezo,  kubadilishana uzoefu na wakati huo huo kujifunza mbinu mpya za kuenenda na nyakati za mabadiliko.

Bw. Mganga aliendelea kueleza kuwa Taasisi yao inaendelea kufanya kazi ili kuhakikisha kuwa wanapambana kuharakisha kutatua changamoto ya makosa hayo kwa haraka ili jamii iweze kupata haki kwa wakati, na kuwezesha kufanya kazi zao za kimaendeleo kwa wakati.

Biswalo amesema Ofisi ya Taifa ya  Mashtaka pamoja na Waendesha Mashtaka ina changamoto nyingi inazokabiliana nazo hivyo kuwepo kwa mafunzo ya mara kwa mara ni mhimu kwa watendaji hao.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Suleiman Nyakulinga amesema kutokana na ongezeko la changamoto ya uhalifu wa kimtandao mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji hao itawasaidia kufahamu namna nzuri ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Nyakulinga ameeleza kuwa  makosa ya Utakatishaji Fedha na Uhalifu wa Kimtandao yameongezeka hivyo kuwa na Waendesha Mashtaka wenye uelewa mkubwa ni mhimu kwa wakati huu.

Naye Wakili wa Serikali toka Mkoani Arusha ambaye amehudhuria mafunzo hayo Bw. Tusaje Samwel amesema kutokana na changamoto zinazojitokeza katika nyanja ya makosa hayo ni mhimu kwao kubadilishana uzoefu na kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kuwawezesha kukabiliana na makosa mbalimbali ya kiuhalifu.

Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Suleiman Nyakulinga akizungumza na washiriki wa mafunzo ambao ni mawakili wa serikali katika ukumbi wa TMDA  Buzuruga Jijini Mwanza 

Baadhi ya mawakili wa serikali toka mikoa yote ya Tanzania Bara wakiendelea kufuatilia kwa ukaribu na umakini  elimu inayotolewa  kuhusiana na uendeshaji wa kesi za rushwa, utakatishaji fedha na udanganyifu kwa njia ya kimtandao
Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga akiwa na baadhi ya  Wakurugenzi wa Idara katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya kuhusiana na uendeshaji wa kesi za rushwa, utakatishaji fedha na udanganyifu kwa njia ya kimtandao
Baadhi ya mawakili wa serikali toka mikoa yote ya Tanzania Bara wakiendelea kufuatilia kwa ukaribu na umakini  elimu inayotolewa 

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa Upelelezi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambaye anashughulikia Usimamizi wa Kesi Bw. Tumaini Kweka akizungumza  na washiriki wa mafunzo hayo jijini Mwanza 

Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .