
Mahakama ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro, imewahukumu washtakiwa Hassani Chikoko na Sudi Salum kwenda jela miaka 20 au kulipa faini kiasi cha shilingi Milioni mia sita (600,690,000/=) kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali.
Kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi Namba 6 ya mwaka 2019 iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Ulanga Mhe. Mhanusi, Mahakamani hapo ilielezwa kuwa mshtakiwa Hassani Chikoko na mwenzake Sudi Salum walikutwa na nyara za Serikali ambazo ni vipande 4 vya meno ya tembo.
ambapo hakimu aliwahukumu kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha Tsh.600,690,000/= kwa kila mmoja.
Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri makahamani hapo pasipo kuacha shaka lolote .






No comments:
Post a Comment