Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo akifungua mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Carbon uliopo Chuo Kikuu cha Sokoine-SUA mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.
Na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Waendesha Mashtaka Viongozi wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na kujituma wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo wakati akifungua mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.
Mafunzo hayo yana lengo la kuwapatia ujuzi Waendesha Mashtaka Viongozi katika maeneo mbalimbali yanayohusu utendaji kazi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha kupata uelewa wa kutosha na wa pamoja juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za kesi mbalimbali katika taasisi .
Aidha, mafunzo hayo yatawapatia fursa ya kujifunza jinsi ya kukusanya takwimu,kuzichakata na hatimaye kuzifanyia kazi pamoja na kuwapatia ujuzi utakaowasaidia kutekeleza majukumu yao.
Aidha, aliwataka kuwashirikisha watumishi wenzao mafunzo waliyoyapata watakaporejea katika vituo vyao vya kazi na kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma.
Bw. Makallo aliwataka washiriki wa mafunzo kuzingatia Maadili kwakuwa aliwaeleza kuwa wanaweza kufanya kila kitu lakini bila kuzingatia Maadili ni sawa na bure.
Waendesha Mashtaka Viongozi hao pia walipata nafasi ya kujifunza masuala mengine ikiwepo Maadili ya Kiutendaji kwa Waendesha Mashtaka katika kukusanya, kutunza na kuwasilisha taarifa za kesi mbalimbali, Ukusanyaji, uchakataji, Utunzaji na Uwasilishaji wa takwimu za kesi majukumu na wajibu wa wakaguzi katika uendeshaji wa Mashtaka,
Aidha,Ukusanyaji wa taarifa unavyosaidia Kitengo cha Uhasibu katika kutekeleza majukumu yake pamoja mada juu ya matarajio ya Divisheni ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa kuhusiana na taarifa za takwimu zake zilizokusanywa na kuwasilishwa
Mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za Kesi mbalimbali kwa Waendesha Mashtaka Arobaini na Mbili kutoka katika Mikoa na Wilaya yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili, 2021.
Mhasibu Mkuu Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Regina Mutagurwa akitoa mada juu ya Ukusanyaji wa taarifa unavyosaidia Kitengo cha Uhasibu katika kutekeleza majukumu yake katika mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za Kesi mbalimbali yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.












No comments:
Post a Comment