AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 AU KULIPA KIASI CHA TSH. 1,063,362,000.


Mahakama ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro imemuhukumu mshtakiwa Gerald Damiani Machege kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha shilingi 1,063, 362,000.

Imeelezwa Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Ulanga Mhe. Matugwa Masimbi katika kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 22 ya mwaka 2019 kuwa mshtakiwa Gerald Damiani Machege alikamatwa baada ya kukutwa na vipande 15 vya meno  kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri pasipo kuacha shaka, na hivyo kupelekea  mshtakiwa Gerald Machege kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha  shilingi  bilioni 1,063,362,000.

Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Francis Malembo na Simon Mgonja 
Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .