Na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka --DSM.
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amekutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, mapema leo ikiwa ni sehemu ya kukuza Uhusiano na Ushirikiano katika utendaji, ili kuwezesha kumalizika kwa mrundikano wa Mashauri yaliyoko katika Mahakama hiyo.
Akizungumza na Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Mkurugenzi wa Mashataka Bw. Mwakitalu amesema kuwa ili kesi ziweze kwenda kwa
kasi na usikilizwaji ufanyike kwa haraka, ni lazima Taasisi hizo zishirikiane
kwa ukaribu hali itakayosaidia kuondoa kero na changamoto zinazosababisha
kuchelewa kesi.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Mwakitalu amesema kuwa changamoto
ya Maridhiano(Pre Bargaining) ambayo imeonekana kuwa tatizo amehaidi ndani ya
wiki moja itashughulikiwa na kufanyiwa kazi ili ufanisi wa kazi uweze kuendelea,ambapo
timu ya maalumu ya Serikali ya mauala ya Kisheria itakutana na kuona namna ya kuboresha Sheria ya Maridhiano
katika Kesi mbalimbali hususani za Uhujumu Uchumi .
Kuhusiana na suala la Mashauri ambayo awali yalikuwa yana
Mkurugenzi, kutoa kibali cha kuendesha kesi, ili hali anaweza kuwakasimisha Utoaji
wa vibali hivyo Waendehsa Mashtaka wa Mikoa, Bw. Mwakitalu amesema kuwa yapo
Mashauri ambayo kwa mujibu wa Sheria
anaweza kuwaelekeza Waendesha Mashtaka wa Mikoa kuyashughulia, lakini yapo
mengine ambayo yanahitaji kibali chake.
“Kwa sasa Mashauri yote yatakayofikishwa Mahakamani ni yale
tu ambayo upelelezi wake umekamilika ikiwa ni mkakaki wa Mahakama ya Tanzania kupitia
kwa Jiji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Profesa Ibrahim Juma wa kutakwa Mashauri
yasizidishe Mwaka yakiwa hayajasikiizwa”Alisema Bw.Mwakitalu
Aidha Bw. Mwakitalu amesema kuwa kwa sasa atahakikisha
anasaini Kesi zote zinazo hitaji kibali chake ili zianze kusikilizwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuondoa mrundikano wa Mashauri hayo
Mahakamani.
Bw. Mwakitalu Ameongeza kwa kusema kuwa Kesi inapochukua muda mrefu upelekea
Mashahidi wengi kupotea na wengine kutoonekana kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo Kuhama au Vifo, ambapo amewahakikishia watendaji wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Ushirikiano mkubwa ili kuwezesha ufanikishaji wa Kesi na
kupunguza Mlundikano wake Katika Mahakama hiyo.
“Mfano mpaka sasa jumla ya Kesi 369 zimekwisha pitisha muda
wake hali inayochangia uwepo wa Malalamiko
ya Wananchi, hivyo basi mimi niwahakikishie Ofisi yangu na Watendeji wangu
hawatakuwa kikwazo kwa hili nikiwa DPP wakati wangu” Alisema Mkurugenzi wa
Mashtaka Bw. Mwakitalu.
Awali akisoma Risala kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)
Sylvester Mwakitalu, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Gedfrey Isaya amesema kuwa mkoa wa Dar es salaam unazo Mahakama za
Hakimu Mkazi Nne ambazo ni Hakimu Mkazi Kisutu,Mahakama ya Watoto,Hakimu Mkazi
Kivukoni/Kinondoni na Mahakama ya Jiji/Sokoine.
Hakimu Mkazi Isaya amesema kuwa kwa kipindi cha Januari
2021 hadi Juni 10,2021 Mashauri mbalimbali yameshughulikiwa ambapo Kesi 579
zilibaki kwa Mwaka 2020 huku Kesi 132 zikipokelewa hadi Mei, Kesi 167
zikisikiliszwa
Aidha Hakimu Isaya amesema kuwa zipo jumla ya Kesi 8 ambazo
zimechukua muda mrefu kutokana na Mashahidi kuwa changamoto katika upatikanaji
wake hali ambayo inapelekea Kesi hizo kuchukua muda mrefu pasipo kusikilizwa.
Hakimu Mkazi Isaya ameongeza kwa kusema kuwa wanakabiliwa
na changamoto kubwa moja ni Upelelezi wa Mashauri kuchukua muda mrefu hata kwa
Mashauri ya bhangi na kuchangia Mlundikano wa Kesi, pili Mashauri mengi kuwa ya
muda mrefu hii ikisababishwa na kutopatikana kwa Mashahidi, Mashauri mengi kusubiri Kibali cha Mkurugenzi
wa Mashataka na hivyo mengi yanachelewa hata kabla ya kibali kutolewa.
Hakimu Mkazi Isaya maehitimisha kwa kusema kuwa Mashauri
mengi ya Nyara za Serikali,Madawa ya kulevya na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA)huchukua muda mrefu sana katika
upelelezi wake.
Kikao hicho kilichofanyika leo Juni 11, ni Mwendelezo wa kikao cha awali ambacho kilifanyika mwezi Mei Tarehe 21, mwaka huu kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Watendaji na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kikiwa na lengo la kutatua changamoto na malalamiko ya Mlundikano wa Kesi katika Mahakama hiyo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Mashtaka ametembelea gereza la Keko jijini Dar es Salaam kujionea hali halisi ya gereza hilo na kuzungumza na wafungwa pamoja na mahabusu wa gereza hilo.
Akizungumza katika gereza hilo Mkurugenzi wa Mashtaka alisema hali ya mrundikano wa mahabusu na wafungwa katika gereza hilo inampa hamasa ya kufanya kazi kwa nguvu, bidii na maarifa ili kutatua changamoto za Msongamano magereza
Bw. Sylvester amesema kuwa changamoto ya kuchelewa kwa upelelezi iliyowasilishwa kupitia risala iliyotolewa na mahabusu na wafungwa wa gereza hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka alisema atakaa na wapelelezi ili kutatua changamoto hiyo na kufanya maamuzi yatakayosaidia kuondoa changamoto hiyo.
Aidha, Mkurugenzi wa Mashtaka aliahidi kwenda kuangalia upya hati za dhamana zilizotolewa ili kuona kama sababu zilizopelekea kutolewa kwa dhamana hizo zipo au hazipo na endapo zitakuwa hazipo kwa sasa ataziondoa.
Mkurugenzi
wa Mashtaka Nchini Bw. Sylvester Mwakitalu akizungumza na Wafanyakazi na Watendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam(hawapo Pichani) ikiwa ni mojawapo ya Mkakati wa Ofisi yake kuhakikisha Mashauri yanaendeshwa kwa weledi na kwa wakati.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylivester Mwakitalu akizungumza na watendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kujadili namna Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam wanavyoweza kushirikiana kuondoa mashauri yaliyochukua muda mrefu yaliyokaa kwa muda mrefu katika mahakama hiyo. Jumla ya mashauri 369 bado hayajafanyiwa kazi ambapo kufuatia kikao hicho maamuzi ya kumaliza changamoto hiyo yamefikiwa Kulia kwake ni Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mhe. Godfrey Isaya.






No comments:
Post a Comment