FANYENI KAZI KWA KUZINGATI HAKI NA USHIRIKIANO ILI KUFIKIA MALENGO YA NCHI-DPP MWAKITALU

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akihutubia katika hafla fupi ya ukaribisho wa kuanza kazi rasmi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu  amewataka watumishi wa  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kufanya kazi kwa kuzingatia Haki, Ushirikiano  kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo ya jamii na Taifa.

Bw. Sylvester amebainisha hayo mapema Mei 24, 2021 wakati akizungumza na viongozi na  watumishi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma alipowasili kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester amewaasa Watumsihi wa Ofisi yake pale wanapoona wamekwama wasisite  kuhakikisha wanaomba ushauri ili kuweza kutatua changamoto zinazokwamisha  utekelezaji wa shughuli za  maendeleo.

“Niwaombe pale mtumishi unapoona ndivyo sivyo njoo tujadiliane ili kuweka mambo sawa, na mimi nitakapobaini tatizo kwenu, sitosita kukuita na kukurekebisha”

Mkurugenzi wa Mashtaka ameongeza kwa kuwataka watumishi wote wa Ofisi ya Taifa ya Mashataka kushikiriana pamoja ili kuwezesha kufikia lengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi. 

“Niendelee kusema nanyi ndugu zangu watumishi wenzangu, tuna jukumu kubwa mbele yetu la kusimamia mashtaka lakini kubwa zaidi ni kutekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia misingi ya sheria  na haki ambayo inapaswa kutendeka kwa wakati”

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande amesema kuwa ili kufikia malengo  yatakayofanikisha utaoji wa haki ni lazima wao kama waendesha Mashtaka wasimame kwa umoja na mshikamano hali itakayochangia kufikia malengo yao kwa wakati.

wakati huo huo Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye  sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Biswalo Mganga katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Mei 25 Mei, 2021 katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande wakipokea maua ishara ya ukaribisho kwenye Ofisi ya Mashtaka kuanza utekelezaji wa Majukumu yao.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande kwa nyuma wakiingai rasmi Ofisii kuanza Majukumu yao.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akisaini kitabu cha wageni katika hafla fupi ya ukaribisho wao iliyofanyika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao makuu Jijini Dodoma
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande akisaini kitabu cha wageni katika hafla fupi ya ukaribisho wao iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao makuu Jijini Dodoma
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande akihutubia katika hafla fupi ya ukaribisho wa kuanza kazi rasmi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma tarehe 24 Mei, 2021
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (katikati),  Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma iliyofanyika tarehe 24 Mei, 2021.
Watumishi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu wakati akihutubia katika hafla fupi ya ukaribisho wao iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  Makao Makuu Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande wakikata keki mara baada ya kukaribishwa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka   Makao Makuu jijini Dodoma.
Watumishi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu wakati akihutubia katika hafla fupi ya ukaribisho wao iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  Makao Makuu Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (katikati),  Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mawakili  wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma katika hafla ya ukaribisho wa kuanza kazi rasmi  iliyofanyika tarehe 24 Mei, 2021
 Tazama picha  mbalimbali katika tukio la Kuwasili kwa Mkurugenzi na Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa  ya Mashtaka  Makao Makuu Jijini Dodoma.



\


Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akisaini kitabu cha Makabidhianao ya Ofisi na  aliyekuwa Mkurugenzi wa Ofisi hiyo Biswalo Mganga ambaye kwa sasa ni Jaji wa mahakama ya Rufani nchini Tanzania 


Nakukabidhi Ofisi, endeleza  mapambano ya kuhakikisha  Mashauri yanaendeshwa kwa wakati. 

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi Rebeca Kwandu akiendelea kufuatilia na kusikiliza maneno ya Mkurugenzi Mashtaka wakati akikaribishwa na watumishi na wafanyakazi wa Ofisi hiyo Makao  Makuu Jijini Dodoma.
Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .