WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA NJOMBE

Washtakiwa watano waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji Kesi namba 84 ya mwaka 2014 ya Alice Mtokoma (56), mkazi wa Kijiji cha Usalule kilichopo Mkoani Njombe wamehukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Wakisomewa shtaka hilo Machi 31, 2021 na wakili wa serikali Andrew Mandwa  na Matiko Nyangelo katika kikao cha Mahakama Kuu kilichofanyika mbele ya Jaji Firmin Matogolo walisema watuhumiwa hao Mei 13,  2012 walimuua  kwa kumpiga Alice Mtokoma kwa kitu chenye ncha kali, kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha sheria namba  196 na 197, kanuni ya adhabu sura ya 16, marejeo ya 2019.

Wakili Nyangelo alieleza kuwa siku ya tukio hilo, watuhumiwa walimfuata nyumbani kwake marehemu na kumueleza kuna sehemu wanatakiwa kwenda naye ndipo walipotekeleza mauaji hayo.

Hukumu hiyo ya kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa hao ilitolewa na Jaji Matogolo katika kikao cha Mahakama Kuu kilichofanyika Mkoani Njombe.

Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .