Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu,hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Mei,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Mei 19,2021 amewaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni wakiwemo, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande, wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania bara hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Wakuu Mikoa pamoja na Watendaji wakuu wa Taasisi aliowateua Mhe.
Rais Samia Suluhu amesema Uongozi ni kazi ya Mungu hivyo amewaasa kumtanguliza
Mwenyezi Mungu wanapotekeleza majukumu yao.
Rais Samia amesema
Tanzania ina watu wasiopungua Milioni Sitini ambapo kati ya hao Milioni
Kumi na tano wanazo sifa za kuwa Viongozi lakini wao ni miongoni mwa wachache
waliofanikiwa kuteuliwa.
Awali Akizungumza katika tukio hilo Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Philip Isdory Mpango amewataka kila mmoja wa Viongozi
walioteuliwa kufuata taratibu na kuheshimu Sheria sanjali na kuzingatia uongozi
wa pamoja kwa kuwa ni wa muhimu sana
Dkt.Mpango amesema kuwa Kazi kubwa waliyonayo Wakuu wa
Mikoa ni kusimamia uchumi wa Mikoa hususani kujielekeza kuongeza uzalishaji hasa
kwenye kilimo lakini pia viwanda.
Aidha Dkt.Mapngo amewataka kwenda kushughulikia masoko ya wananchi, hasa kukuza uchumi wa
nchi ili kuwezesha upatikanaji wa maisha bora zaidi kwa wananchi
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Job Ndugai amewataka viongozi walioteuliwa kuhakikisha wanafanya kazi kama timu na
inapotokea kuwa kuna jambo linahitajika uwajibikaji basi.kuwepo na uwajibikaji
wa pamoja.
“Sisi pendekezo letu tuweke syncronization
kati ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi ili kama Halmashauri
hazitekelezi vizuri, wawajibike wote”amesema Mh.Job ndugai Spika wa Bunge
Mh. Ndugai amesema haiwezekani sheria itungwe kwamba
asilimia 10 ya fedha iende kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, halafu
zinakuja Halmashauri kadhaa ndani ya Mkoa uleule hazijatenga. Jambo ambalo
linapaswa kuangaliwa kwa umakini
Naye Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa amewaasa kujifunza na kutambua majukumu ya Taasisi
walizopewa kuziongoza .
"
Tambua majukumu ya Taasisi uliyopewa, jifunze nini kinachotakiwa kwenye ofisi
yako, fahamu mipaka yako pamoja na kuwafahamu vizuri waliokuzunguka”amesema
Kassim Majaliwa Waziri Mkuu .
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma amesema DPP na TAKUKURU ni wadau muhimu katika mnyororo wa kusimamia na kutoa haki katika Mahakama ya Tanzania kwa sababu DPP na TAKUKURU ni wadau muhimu sana wa Mahakama kwani haki uanzia kwenye ngazi ya upelelezi na kuishia mahakamani.
"Tufanye
kazi kama timu Inapotokea uwajibikaji tuwajibike wote RC, DC, RAS haipendezi
inapotokea uwajibikaji haipendezi kuona Mkurugenzi anawajibika peke yake”amesema
Profesa Juma Ibrahim Jaji Mkuu Tanzania.
Jaji Juma Ibrahim amesema ili haki ipatikane kwa wakati
Upelelezi na uendeshaji wa Kesi ni lazima ufanyike kwa wakati hivyo aliitaka
ofisi ya DPP na TAKUKURU kutembelea tovuti ya Mahakama ili kuangalia kesi zilizopo
mahakani na muda zinazotakiwa kuisha ili waweze kuzifanyia kazi .
" Tembeleeni tovuti ya Mahakama kuangalia
wapi kuna tatizo. Endapo kesi imepitiliza muda iliyopangwa kuisha huwa tunaweka
alama nyekundu ili muweze kuangalia wapi kuna tatizo na kurekebisha. Endapo
kuna tatizo katika sheria
unaokwamisha katika utoaji haki
wasione haya katika kurekebisha sheria. Amesisitiza Profesa Juma Jaji Mkuu.









No comments:
Post a Comment