Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Kwatunza Beach uliyopo Ilemela Jijini Mwanza kuanzia Octoba 31 hadi Novemba 1.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)
Bw. Sylvester Mwakitalu amewaasa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na kanuni za utumishi wa
Umma ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati.
Bw.Mwakitalu amebainisha hayo wakati
akifungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika
katika ukumbi wa Kwatunza Beach uliopo Ilemela Jijini Mwanza leo Oktoba 31, 2024 ambapo
amesema kuwa licha ya wafanyakazi kudai maslahi na stahiki zao ni vema
wakatimiza wajibu wao kwa wakati na kwa ufanisi.
“Nasisitiza uwajibikaji
katika kazi zenu na katika kikao hiki msiwaangushe wenzenu waliobaki kwenye vituo
vyenu vya kazi, kwa kuhakikisha mnatoa mapendekezo, maoni na kueleza changamoto zao ili kuwezesha kikao
hiki kutoka na maazimio ya pamoja yatakoyowezesha kuweka mazingira bora ya
utendaji kazi wetu na masuala yote yanaohusu utumishi” amesema Bw. Mwakitalu
Mkurugenzi wa Mashtaka.
Aidha, Mwakitalu amesema uwepo
wa Baraza la Wafanyakazi katika taasisi ni moja ya njia bora ya kupokea,
kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi katika maeneo
mbalimbali ya kazi kutokana na jiografia ya nchi na hivyo kupitia wawakilishi wao
kwenye baraza inalenga kuleta mitazamo chanya na kuboresha maisha ya watumishi.
Katika hatua nyingine Bw.
Mwakitalu ameitumia nafasi hiyo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo
Bi. Bibiana Kileo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ambaye
kimuundo wa baraza anaingia moja kwa moja kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Naye Naibu Mkurugenzi wa
Mashtaka Bi. Bibiana Kileo amesema tangu kuasisiwa kwa Ofisi ya Taifa ya
Mashtaka mwaka 2018 Ofisi imekuwa ikijadili na kupitia masuala mbalimbali
yanayaohusu wafanyakazi ili kutathmini na kuona ni kwa namna gani Ofisi imeweza
kutekeleza maazimio ya mabaraza yaliyopita
Bibiana amesema Baraza la
Wafanyakazi husaidia kuwapa nafasi ya kutafakari masuala mbalimbali yanayowahusu
zikiwepo changamoto zao ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa
kuzingatia weledi na umahiri walionao sambamba na kuwapongeza watumishi wote
kwa kufanya kazi kwa moyo wa uaminifu ili kusaidia jamii kupata haki zake.
Akizungumza katika Mkutano huo,
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Simon
Ntobi amesema baraza hilo la tatu la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
lina jukumu kubwa la kuishauri taasisi ili maslahi ya wafanyakazi yaweze
kupatikana kwa wakati.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE
Taifa Bw. Rugemalira Rutatina ameipongeza Ofisi ya Mashtaka kwa kulipa hadhi
Baraza la Wafanyakazi kwa kuhakikisha wanapokea na kupitia changamoto za wafanyakazi
katika mazingira rafiki na kuwapa nafasi
ya kueleza changamoto zao ili tija na
ufanisi wa kazi uweze kuonekana.
Rugemalira amewasisitiza wakuu
wa Divisheni kuwahamasisiha wafanyakazi walio chini ya idara zao kujiunga na
mabaraza ya wafanyakazi ili waweze kutoa maamuzi ya pamoja na si kungoja
kuamriwa na kundi la wachache ambao ni wanachama hai wa baraza.
Kwa upande wake Afisa Kazi
Mkuu Kanda ya Kati, Bw. Goodluck Luginga akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Kazi
katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema ni
jukumu la watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kufanya kazi kwa tija ili kuleta matokeo
chanya kwa ajili ya umma.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Kwatunza Beach uliyopo Ilemela Jijini Mwanza kuanzia Octoba 31 hadi Novemba 1.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Bibiana Kileo akitoa salamu fupi na kumkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo Bw. Sylvester Mwakitalu kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Utawala na Raslimaliwatu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Simon Ntobbi akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo kutoa salamu kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu Tughe Taifa Bw. Rugemalira Rutatina akitoa salamu na nasaha kutoka TUGHE wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Afisa Kazi Mkuu wa Kanda ya Dodoma Bw. Goodluck Luginga akiwasilisha mada juu ya Haki na Wajibu wa Wafanyakazi wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Juma Kattanga akitoa neno la ukaribisho na utambulisho katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Makosa dhidi ya Binadamu na Utangamano wa Taifa kutoka Ofisi ya Mashtaka akiongoza Shughuli ya Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo unaofanyika Mkoani Mwanza.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Samwel Nyungwa akiwasilisha mada juu ya Nafasi na Umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi mahali pa kazi wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa Mashtaka wakiendelea kufautilia Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika Jijini Mwanza.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa Mashtaka wakiendelea kufautilia Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika Jijini Mwanza.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa Mashtaka wakiendelea kufautilia Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika Jijini Mwanza.
Picha ya pamoja ikijumuisha Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bi. Bibiana Kileo (wa pili kushoto) pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza