DPP ASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza  la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Kwatunza Beach uliyopo Ilemela Jijini Mwanza kuanzia Octoba  31 hadi Novemba 1.   


Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu amewaasa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na kanuni za utumishi wa Umma ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Bw.Mwakitalu amebainisha hayo wakati akifungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika katika ukumbi wa Kwatunza Beach uliopo Ilemela  Jijini Mwanza leo Oktoba 31, 2024 ambapo amesema kuwa licha ya wafanyakazi kudai maslahi na stahiki zao ni vema wakatimiza wajibu wao kwa wakati na kwa ufanisi.

Nasisitiza uwajibikaji katika kazi zenu na katika kikao hiki msiwaangushe wenzenu waliobaki kwenye vituo vyenu vya kazi, kwa kuhakikisha mnatoa mapendekezo, maoni  na kueleza changamoto zao ili kuwezesha kikao hiki kutoka na maazimio ya pamoja yatakoyowezesha kuweka mazingira bora ya utendaji kazi wetu na masuala yote yanaohusu utumishi” amesema Bw. Mwakitalu Mkurugenzi wa Mashtaka.

Aidha, Mwakitalu amesema uwepo wa Baraza la Wafanyakazi katika taasisi ni moja ya njia bora ya kupokea, kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi katika maeneo mbalimbali ya kazi kutokana na jiografia ya nchi na hivyo kupitia wawakilishi wao kwenye baraza inalenga kuleta mitazamo chanya na kuboresha maisha ya watumishi.

Katika hatua nyingine Bw. Mwakitalu ameitumia nafasi hiyo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Bi. Bibiana Kileo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ambaye kimuundo wa baraza anaingia moja kwa moja kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo amesema tangu kuasisiwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka mwaka 2018 Ofisi imekuwa ikijadili na kupitia masuala mbalimbali yanayaohusu wafanyakazi ili kutathmini na kuona ni kwa namna gani Ofisi imeweza kutekeleza maazimio ya mabaraza yaliyopita

Bibiana amesema Baraza la Wafanyakazi husaidia kuwapa nafasi ya kutafakari masuala mbalimbali yanayowahusu zikiwepo  changamoto zao  ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na umahiri walionao sambamba na kuwapongeza watumishi wote kwa kufanya kazi kwa moyo wa uaminifu ili kusaidia jamii kupata haki zake.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Simon Ntobi amesema baraza hilo la tatu la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka lina jukumu kubwa la kuishauri taasisi ili maslahi ya wafanyakazi yaweze kupatikana kwa wakati.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa Bw. Rugemalira Rutatina ameipongeza Ofisi ya Mashtaka kwa kulipa hadhi Baraza la Wafanyakazi kwa kuhakikisha wanapokea na kupitia changamoto za wafanyakazi  katika mazingira rafiki na kuwapa nafasi ya kueleza  changamoto zao ili tija na ufanisi wa kazi uweze kuonekana.

Rugemalira amewasisitiza wakuu wa Divisheni kuwahamasisiha wafanyakazi walio chini ya idara zao kujiunga na mabaraza ya wafanyakazi ili waweze kutoa maamuzi ya pamoja na si kungoja kuamriwa na kundi la wachache ambao ni wanachama hai wa baraza.

Kwa upande wake Afisa Kazi Mkuu Kanda ya Kati, Bw. Goodluck Luginga akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Kazi katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema ni jukumu la watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  kufanya kazi kwa tija ili kuleta matokeo chanya kwa ajili ya umma.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza  la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Kwatunza Beach uliyopo Ilemela Jijini Mwanza kuanzia Octoba  31 hadi Novemba 1.Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Bibiana Kileo akitoa salamu fupi na kumkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo Bw. Sylvester Mwakitalu kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.Mkurugenzi wa  Utawala na Raslimaliwatu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Simon Ntobbi akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo kutoa salamu kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu Tughe Taifa Bw. Rugemalira Rutatina akitoa salamu na nasaha kutoka TUGHE wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Afisa Kazi Mkuu wa Kanda ya Dodoma Bw. Goodluck Luginga  akiwasilisha mada juu ya  Haki na Wajibu wa Wafanyakazi wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Juma Kattanga akitoa neno la ukaribisho na utambulisho katika  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Makosa dhidi ya Binadamu na Utangamano wa Taifa  kutoka Ofisi ya Mashtaka akiongoza Shughuli ya  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi  wa Ofisi hiyo unaofanyika Mkoani Mwanza.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Samwel Nyungwa akiwasilisha mada juu ya Nafasi na Umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi mahali pa kazi wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza.


Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa Mashtaka wakiendelea kufautilia Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa  ya Mashtaka unaofanyika Jijini Mwanza.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa Mashtaka wakiendelea kufautilia Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa  ya Mashtaka unaofanyika Jijini Mwanza.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa Mashtaka wakiendelea kufautilia Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa  ya Mashtaka unaofanyika Jijini Mwanza.

Picha ya pamoja ikijumuisha Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  Bw. Sylvester Mwakitalu (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bi. Bibiana Kileo (wa pili kushoto) pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaofanyika tarehe 31 Oktoba hadi 01 Novemba, 2024 Jijini Mwanza





Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .