DPP ATEMBELEA MAGEREZA JIJINI DAR ES SALAAM.

 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu, afanya ziara ya siku tatu ya kutembelea magereza ya mahabusu Mkoa wa Dar es saalam kwa lengo la kuongea na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo mahabusu na wafungwa ili kuweza kuzifanyia kazi kwa wakati.

Katika ziara hiyo,  Bw. Mwakitalu aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Chalamila, Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Aretas Lyimo, viongozi ngazi ya mkoa wanaounda mnyororo wa Haki Jinai pamoja na  Waendesha Mashataka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Ziara hiyo inafanyika tarehe 18-20 Novemba, 2024 Jijini Dar es salaam.



Picha ya pamoja ikijumuisha Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Chalamila, Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Aretas Lymo wakiwa na viongozi wa ngazi ya mkoa wanaounda mnyororo wa Haki Jinai, Waendesha Mashataka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka mara baada ya kutembelea gereza la Mahabusu Segerea Jijini Dar es salaam

Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .