OFISI YA MASHTAKA
  • Home
  • UONGOZI
  • HISTORIA
  • JARIDA
  • VIDEO
  • MAONI USHAURI
  • MAWASILIANO
  • Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • UKATAJI WA UTEPE

    UKATAJI

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

WASHITAKIWA 16 WA UJANGILI WAFUNGWA MIAKA 20 HADI 30 KWA KUKUTWA HIFADHINI NA NYARA ZA SERIKALI

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 29, 2020MARA No comments

 

Washitakiwa 16 katika kesi Namba  8 wametiwa hatiani kwa makosa ya ujangili na kuhukumiwa jumla ya kifungo kati ya miaka 20 hadi 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti.

Washitakiwa hao walikamatwa mwaka 2019 kwa nyakati tofauti ndani ya  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mapori ya Akiba ya Ikorongo, Grumeti na Hifadhi ya Jamii ya Ikona na kushitakiwa kwa makosa matatu ikiwemo  kuingia,kupatikana na silaha za jadi  na kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao kwa nyakati na sehemu mbalimbali walikamatwa na nyara tofauti ikiwemo vipande vya nyama za Pundamilia, Impala, Nyumbu na Kongoni zenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni 29 na laki 9 na Elfu 55 (29,955,000).

 Akisoma hukumu hiyo  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Serengeti  Ismael Ngaile amesema kuwa  kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ambayo inatoa adhabu ya isiyozidi miaka 30 na isiyopungua miaka 20 .

Washitakiwa hao ni  Makena Mwita (21) Mkazi wa Mbirikiri ,  Rubeni Mwita (28) wa Bonchugu ambao kila mmoja amehukumiwa miaka 30 jela huku  Mugendi Ng’ombe (51) mkazi wa Nyichoka,Richard Nyambaya(35)na Mussa Masese(42)wakazi wa kijiji cha Nyamatoke walihukumiwa kila mmoja miaka 25 

Aidha  Manungu Makoye na Mazoya Daddi ambao wamehukumiwa miaka 20, na wenzao  Simion Nyamhanga(28)mkazi wa Nyamakendo,Benard Gambachera(50)mkazi wa Robanda, Marwa Chacha (30) Marwa Mtatiro(19)Mnanka Bisare(28)Sarya Matiko(20) Maduhu Mila(35)mkazi wa kijiji cha Singisi,Bhoke Mwita(53)na Juma Masyora(43)wakazi wa Bisasara.

Mapema waendesha Mashitaka wa serikali Josephat Emmanuel, Abeid Nnko na Jakobo Matatala mbele ya Hakimu Ngaile waliomba Mahakama kutoa adhabu kali katika kesi hizo za Uhujumu uchumi kwa kuwa vitendo vya ujangili vinazidi kushamiri na kuathiri maliasili za Nchi, huku baadhi ya washitakiwa wakishindwa kujitetea.

Share:
Read More

DPP ATOA MAELEKEZO KWA TAKUKURU NA DCI KUKAMILISHA UCHUNGUZI JUU YA UHABA WA SARUJI NA VIFAA VYA UJENZI NCHINI NDANI YA SIKU 30

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 20, 2020 No comments

                             
                                                       
Share:
Read More

DPP AWAONYA WAUZAJI WANAOFICHA VIFAA VYA UJENZI

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 18, 2020 No comments

 .        Mkurugenzi  wa Mashtaka Nchini Bw.Biswalo Mganga akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi nchini kuacha kuficha Vifaa hivyo.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Biswalo Mganga amewaonya wauzaji wa vifaa vya Ujenzi kufuatia baadhi yao  kuficha Sementi na Mabati kwa lengo la  kuongeza bei  ili kujipatia faida kubwa zaidi, na  kusema kuwa kufanya hivyo  ni  kosa la Jinai

Bw. Mganga ameeleza kuwa watu  wote wanaofanya hivyo wanafanya kosa la uhujumu uchumi ambalo limeanishwa katika Sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 jela   pamoja na  kutaifishwa  mali kwa yeyote atakayekamatwa kwa kutenda kosa hilo.

Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo Jijini Dodoma leo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika yaliyokuwa na lengo la kufahamu mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya  Mashtaka tangu kuanzishwa kwake ambapo ameeleza kuwa imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake.

Aidha, amesema kuwa jukumu la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni kuhakikisha kuwa Haki, Amani na Usalama vinapatikana nchini kwa Maendeleo ya Taifa.                                                                                      Mwonekano wa nembo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma
                                           Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Biswalo Mganga akusoma Dira ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
       Mwonekano wa mbele wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) lililoko Jijini Dodoma

Share:
Read More

MKURUGENZI WA MASHTAKA AZINDUA TOVUTI YA CHAMA CHA WAENDESHA MASHTAKA AFRIKA MASHARIKI

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 17, 2020 No comments

 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo  Mganga amezinduzi Tovuti ya  Chama cha Waendesha  Mashtaka Afrika Mashariki akishirikiana na viongozi wengine kutoka katika  nchi wanachama.

uzinduzi huo umefanyika Novemba 16, 2020 kwa njia ya Mtandao ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini biswalo mganga  ameedesha zoezi hilo akiwa jijini Dodoma huku   Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Kenya  ambaye pia ni Katibu wa chama hicho Bw. Noordin Mohamed Haji  akiwa jijini Nairobi.

 katika uzinduzi huo viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo  Bi. Heather Schildge ambaye  ni    Naibu  Mkurugenzi wa  Misioni kutoka Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani-USAID, Bi. Julie Thomson ambaye ni Mkurugenzi wa Trafiki  Progamu ya Afrika, Wawakilishi Kutoka katika Mashirika ya Kimataifa na Kikanda pamoja na Waendesha Mashtaka kutoka  baadhi ya nchi wanachama wa Umoja huo.

Akieleza umuhimu wa  Tovuti hiyo Bw. Biswalo alisema uzinduzi huo ni miongoni mwa hatua muhimu iliyofikiwa katika  kuimairisha mapambano dhidi ya uhalifu wa wanyamapori  katika nchi za Afrika Mashariki.

Chama Cha Waendesha Mashtaka wa Afrika Mashariki kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na jumla ya wananchama kutoka nchi tano ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na Kenya ambapo hadi  kufika hivi sasa chama hicho kimefanikiwa kuongeza wanachama kutoka nchi nyingine jirani zikiwemo Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Sudan, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Zambia, Malawi na Msumbuji.

Wakati wa Uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mashtaka aliendelea kueleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2014 katika nchi ya Tanzania idadi nyingi ya Tembo ilishuka hadi kufikia asilimia 60 kutokana na ujangili na biashara haramu ya wanyamapori ukilinganisha na matukio ya nchi nyingine za jirani.

''Tovuti hii ni chombo muhimu kwa ajili ya kuhakikisha masuala yote ya taarifa dhidi ya uhalifu wa Wanyama katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa yanarahisishwa ili kupambana na wale wote wanaojihusisha na biashara haramu za Wanyamapori   pamoja na kuimarisha mifumo wa mawasiliano katika nchi wanachama''.

''Ni matumaini yangu kuwa website hii kupitia umoja wa waendesha mashtaka wa masuala ya wanyama na mazingira utaamsha katika matumizi ya sheria mbalimbali za kikanda za wanyama kupelekea kukua kwa uhifadhi wa wanyama na kuwa na kituo cha kutolea taarifa kuhusu makosa hayo''.

''Napenda kushukuru waendesha mashtaka wote kwa ushiriano waliotoa katika kutengeneza na kuanzisha tovuti na juhudi za makusudi za kujenga umoja huu''.amesema Bw Biswalo Mganga

Mwisho aliwashukuru wajumbe waliohudhuria katika kikao hicho wakiwemo Bw. Noordin Mohamed Hji, Bi. Heather Schildge, Bi. Julie Thomson, na wawakilishi mbalimbali kutoka Mataifa mbalimbali ya Kiserikali.

 

Share:
Read More

Wahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 17, 2020 No comments

 


Mahakama Kuu ya Rushwa na Uhujumu Uchumi  Dar es Salaam katika kesi ya Uhujumu Uchumi  namba 14/2018 mbele ya Mhe. Jaji Banzi imewatia hatiani washtakiwa Nabibarkhshsh Pribakhsh na Mohamaddhanif Nazirahmad Dorzade kwa kosa la kupatikana na Madawa ya Kulevya aina ya Heroin Hydrochloride kiasi cha Kilogramu 111.2 na Gramu 451.7 za Bangi na kuwahukumu kwenda jela kifungo cha miaka thelathini  pamoja na kutaifisha jahazi ambalo walitumia kutenda kosa hilo

Shauri hili limeendeshwa na Mawakili wa Serikali Monica Mbogo, Cecilia Shelly, Batilda Mushi  na Clara Charwe

Aidha, mahakama imewaachia huru watuhumiwa kumi na moja (11) katika kesi hiyo ambao majina yao ni
Abdullah Khatoon Sahib,
Ubeidulla Gulamzade Abdi, Naim Baltik Ishqa
Moslem Amiree Golmohamad,
Rashid Badfar, Omary Dorzade Ayoub, Tahir Bishkar Mubarak,
.Abdulmajid Asqan Pirmuhamad,
Ally Abdallah Ally,
Juma Amour Juma,
Omari Saidi Mtangi. 
Mbele ya Mh Jaji Banzi. Mahakama imemtia hatiani Nabibarkhsh Pribakhsh na Mohamaddhanif Nazirahmad Dorzade ambao walikuwa ni miongoni mwa washtakiwa katika shauri hilo. Hata hivyo upande wa Mashtaka haujaridhishwa na Maamuzi ya Mahakama ya kuwaachia huru  Washtakiwa hao na umekata rufaa kupinga hukumu hiyo.





Share:
Read More

Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mkewe

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 17, 2020 No comments

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi ya Jinai Na.137/2018 mbele ya Mhe. Jaji J.C Tiganga imemtia hatiani mshtakiwa Mwita Mgaya Nyamtiba kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kukusudia kumuua mkewe Christina Mwita Mgaya.

Akiielezea Mahakama Wakili wa Serikali Bw. Nimrod Byamungu amesema kuwa, tukio hilo lilitokea mnamo tarehe5, Januari 2018 katika Kijiji cha Kitagasembe  Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara ambapo mshtakiwa alimuua marehemu kwasababu alikuwa anamzuia kuuza ardhi ya familiya kwa ajili ya kuoa wake wengine pamoja na kunywa pombe.
Marehemu aliuawa kwa kuchinjwa shingo na kukatwa usoni kwa kutumia panga.

 

Share:
Read More

Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto) Akiweka kumbukumbu ya Dawa za kulevya

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 13, 2020 No comments

Mahakama Kuu kwa kushirikiana na mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya nchini na ofisi ya mwendesha mashtakaa-DPP wameteketeza zaidi ya kilo 100 za dawa za kulevya ikiwemo heroini, cocaine na bangi ambazo kesi zake zimemalizika kwa kipindi cha miaka miwili na watuhumiwa kuhukumiwa.



Tukio la uteketezaji limefanyika Leo jijini Dar es Salaam katika kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill-TWIGA CEMENT ambapo zoezi zima lilifanyika kwa ulinzi wa jeshi la Polisi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari katika tukio hilo, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Jaji Edwin Kakolaki amesema baada ya kesi kumalizika mahakama hutoa kibali cha kuteketeza Vielelezo na zoezi hilo linaendeshwa kwa uwazi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali.



“Uendeshaji wa tukio hili kwa uwazi husaidia kuandoa dhana inayoenezwa mtaani kuwa dawa za kulevya hurudishwa tena mtaani baada ya kukamatwa”. Amesema Jaji Kakolaki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka nchini-DPP, Biswalo Mganga ameeleza vielelezo hivyo ni vya zaidi ya kesi 30 za dawa za kulevya za watuhumiwa wa ndani na nje ya nchi huku akieleza mbali na watuhumiwa kuhukumiwa pia baadhi ya mali zao zimetaifishwa na Serikali.



Naye kamishna wa sayansi na jinai kutoka mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya nchini Bi.Bertha Mamuya amebainisha kwamba uteketezaji wa dawa hizo hauna athari ndani ya jamii.



Share:
Read More

Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakola akishirikiana na Mkurugenzi wa Mashtaka B

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 13, 2020 No comments

Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakola akishirikiana na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga kuteketeza Madawa ya kulevya katika zoezi maalum walilolifanya Jijini Dar es Salaam
 

Share:
Read More
← Newer Posts Older Posts → Home

Social Profiles

TwitterFacebookGoogle PlusInstagramRSS FeedEmail
  • Popular
  • Tags
  • Blog Archives

Pages

  • Home
  • MAONI USHAURI
  • JARIDA
  • MAWASILIANO
  • VIDEO
  • MAAFISA TRA NA BENKI WALIOACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA KISUTU WATIWA HATIANI KWA KOSA LA UTAKATISHAJI FEDHA
     Mahakama ya Rufani imetoa hati ya kuwakamata na kuwaweka  rumande washtakiwa wanne, akiwamo aliyekuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanza...
  • UKATILI WA KIJINSIA UATHIRI AFYA NA UCHUMI WA TAIFA - NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA.
    Baadhi ya Wakuu wa Mashtaka kutoka Mikoa na Wilaya zote Tanzania bara wakiendelea kufuatilia hotuba ya ufungaji wa Mafunzo ya kuwajengea uwe...
  • WASHTAKIWA 57 WAFUTIWA MASHTAKA GEREZA LA KAYANGA-KARAGWE MKOANI KAGERA WATAKIWA KWENDA KUWA RAIA WEMA
    Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amon Mpanju ,Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga   ...

Labels

  • DAR ES SALAAM (8)
  • DODOMA (3)
  • KAGERA (2)
  • KIGOMA (1)
  • KITAIFA (2)
  • LINDI (1)
  • MARA (2)
  • MOROGORO (4)
  • mwanza (1)
  • njombe (1)
  • SERENGETI-MARA (1)
  • SINGIDA (2)

Blog Archive

  • ► 2025 (24)
    • ► October (3)
    • ► May (5)
    • ► March (11)
    • ► February (5)
  • ► 2024 (35)
    • ► December (6)
    • ► November (6)
    • ► October (4)
    • ► September (3)
    • ► August (1)
    • ► June (1)
    • ► May (3)
    • ► April (1)
    • ► March (7)
    • ► January (3)
  • ► 2023 (17)
    • ► November (1)
    • ► September (2)
    • ► August (2)
    • ► July (2)
    • ► May (3)
    • ► April (3)
    • ► March (2)
    • ► February (2)
  • ► 2022 (24)
    • ► December (1)
    • ► November (1)
    • ► October (1)
    • ► August (3)
    • ► July (2)
    • ► May (4)
    • ► March (4)
    • ► February (4)
    • ► January (4)
  • ► 2021 (36)
    • ► December (2)
    • ► November (5)
    • ► October (1)
    • ► September (3)
    • ► August (1)
    • ► July (1)
    • ► June (4)
    • ► May (4)
    • ► April (3)
    • ► March (2)
    • ► February (3)
    • ► January (7)
  • ▼ 2020 (26)
    • ► December (7)
    • ▼ November (8)
      • WASHITAKIWA 16 WA UJANGILI WAFUNGWA MIAKA 20 HADI ...
      • DPP ATOA MAELEKEZO KWA TAKUKURU NA DCI KUKAMILISHA...
      • DPP AWAONYA WAUZAJI WANAOFICHA VIFAA VYA UJENZI
      • MKURUGENZI WA MASHTAKA AZINDUA TOVUTI YA CHAMA CH...
      • Wahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kukutwa na ma...
      • Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua m...
      • Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto)...
      • Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakola akishirikia...
    • ► October (11)

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .
  • Loading...
  • Loading...
  • Kitengo cha TEHAMA

    Lengo: kutoa utaalamu na huduma kwa matumizi ya TEHAMA ; Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo: (i) Kutekeleza mpango mkakati wa TEHAMA na Serikali Mtandao; (ii) Kuendeleza na kuratibu mifumo TEHAMA kwa kushirikiana na wakala ya serikali mtandao;. (iii) Kuhakikisha kwamba vifaa na programu za TEHAMA zinasimamiwa na kutunzwa (iv) Kuratibu na kutoa msaada katika ununuzi wa programu na vifaa vya TEHAMA; .
Copyright © OFISI YA MASHTAKA
-