Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga amezinduzi Tovuti ya Chama cha Waendesha Mashtaka Afrika Mashariki akishirikiana na viongozi wengine kutoka katika nchi wanachama.
uzinduzi huo umefanyika Novemba 16, 2020 kwa njia ya Mtandao ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini biswalo mganga ameedesha zoezi hilo akiwa jijini Dodoma huku Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Kenya ambaye pia ni Katibu wa chama hicho Bw. Noordin
Mohamed Haji akiwa jijini Nairobi.
katika uzinduzi huo viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo Bi. Heather Schildge ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Misioni kutoka Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani-USAID, Bi. Julie Thomson ambaye ni Mkurugenzi wa Trafiki Progamu ya Afrika, Wawakilishi Kutoka katika Mashirika ya Kimataifa na Kikanda pamoja na Waendesha Mashtaka kutoka baadhi ya nchi wanachama wa Umoja huo.
Akieleza umuhimu wa Tovuti hiyo Bw. Biswalo alisema uzinduzi huo ni miongoni mwa hatua muhimu iliyofikiwa katika kuimairisha mapambano dhidi ya uhalifu wa wanyamapori katika nchi za Afrika Mashariki.
Chama Cha Waendesha Mashtaka wa Afrika Mashariki kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na jumla ya wananchama kutoka nchi tano ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na Kenya ambapo hadi kufika hivi sasa chama hicho kimefanikiwa kuongeza wanachama kutoka nchi nyingine jirani zikiwemo Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Sudan, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Zambia, Malawi na Msumbuji.
Wakati wa Uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mashtaka aliendelea kueleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2014 katika nchi ya Tanzania idadi nyingi ya Tembo ilishuka hadi kufikia asilimia 60 kutokana na ujangili na biashara haramu ya wanyamapori ukilinganisha na matukio ya nchi nyingine za jirani.
''Tovuti hii ni chombo muhimu kwa ajili ya kuhakikisha masuala yote ya taarifa dhidi ya uhalifu wa Wanyama katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa yanarahisishwa ili kupambana na wale wote wanaojihusisha na biashara haramu za Wanyamapori pamoja na kuimarisha mifumo wa mawasiliano katika nchi wanachama''.
''Ni matumaini yangu kuwa website hii kupitia umoja wa waendesha mashtaka wa masuala ya wanyama na mazingira utaamsha katika matumizi ya sheria mbalimbali za kikanda za wanyama kupelekea kukua kwa uhifadhi wa wanyama na kuwa na kituo cha kutolea taarifa kuhusu makosa hayo''.
''Napenda kushukuru waendesha mashtaka wote kwa ushiriano
waliotoa katika kutengeneza na kuanzisha tovuti na juhudi za makusudi za
kujenga umoja huu''.amesema Bw Biswalo Mganga
Mwisho aliwashukuru wajumbe waliohudhuria katika kikao hicho wakiwemo Bw. Noordin Mohamed Hji, Bi. Heather Schildge, Bi. Julie Thomson, na wawakilishi mbalimbali kutoka Mataifa mbalimbali ya Kiserikali.







No comments:
Post a Comment