Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi ya Jinai Na.137/2018 mbele ya Mhe. Jaji J.C Tiganga imemtia hatiani mshtakiwa Mwita Mgaya Nyamtiba kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kukusudia kumuua mkewe Christina Mwita Mgaya.
Akiielezea
Mahakama Wakili wa Serikali Bw. Nimrod Byamungu amesema kuwa, tukio
hilo lilitokea mnamo tarehe5, Januari 2018 katika Kijiji cha
Kitagasembe Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara ambapo mshtakiwa alimuua
marehemu kwasababu alikuwa anamzuia kuuza ardhi ya familiya kwa ajili ya
kuoa wake wengine pamoja na kunywa pombe.
Marehemu aliuawa kwa kuchinjwa shingo na kukatwa usoni kwa kutumia panga.







No comments:
Post a Comment