• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

WASHTAKIWA 183 WAFUTIWA MASHTAKA MKOANI KAGERA DPP AWAONYA KUTORUDIA MAKOSA TENA

Katikati  ni Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Biswalo Mganga  akikata utepe wa ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya  Karagwe akiwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mheshimiwa Godfrey Mheluka pamoja na Viongozi wengine waliohudhuria Sherehe hizo za Ufunguzi wa ofisi. 
                   Na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amewafutia Mashtaka jumla ya washtakiwa 183 katika magereza ya Karagwe, Bukoba, Biharamulo na Muleba mkoani Kagera.

Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP).Biswalo Mganga amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ambapo amesema kuwa mkoa huo unakabiliwa na kesi nyingi za mauaji.

Biswalo ameeleza  baada ya kutembelea magereza mbalimbali  na kuongea na mahabusu walioko ndani ameamua kuwafutia washtakiwa  57 toka wilaya ya  Karagwe, 54 Bukoba, 48 Biharamulo  na Muleba 26 huku katika ziara hiyo akikutana na badhi ya washtakiwa ambao ni wahamiaji haramu 15  waliokuwa wamekaribishwa na wazawa wa mkoa wa Kagera.

"Kimsingi kuna makosa mengi na kesi nyingi ambazo walengwa hawastahili kuwemo gerezani hivyo nimeamua kuwaachia kikubwa niwaombe viongozi wa dini muendelee kuhubiri amani,upendo ili vitamalaki kwani vitasaidia kupunguza hizi kesi"amesema Mganga.

Aidha, Bw.Biswalo  ametanabaisha kuwa hatosita kumchukulia hatua mtu yoyote bila kujali nafasi aliyonayo kisiasa,dini au Serikali ikigundulika kuwa amejihusisha   na vitendo vya Uhalifu ambapo amesisistiza suala la amani ni jukumu la kila mtu hivyo wanawajibika kuitunza kwa kuepuka kufanya makosa ya jinai.

Hata hivyo, Bw. Biswalo amewataka wahusika wote wenye jukumu la kuendesha Mashtaka kutoka Taassi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) na Polisi wote kutumia Ofisi ya Taifa ya  Mashtaka ya wilaya hiyo kinyume cha hapo hatasita kuwanyanganya nyenzo alizowapatia za kibali cha  kuendesha Mashtaka kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mashtaka.

"Ninawaagiza waendesha Mashtaka wote wa wilaya hii kuanzia leo majarada yote nataka  leo yahamie kwenye ofisi hii ,na wote mnaohusika na kuendesha mashtaka uwe Tanapa,Takukuru mtakuwa chini ya Mwanasheria huyu Haruna Shomari na atakayekwambia mimi nipo chini ya DCI niambie sitasita  kumtengua na nitamnyanganya nyenzo zangu."amesma DPP Mganga.

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kagera Mhesimiwa Ntemi Kilekamajenga amesema mkoa wa  Kagera unaongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji ambapo amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani ili kupunguza vitendo vya uhalifu.

Jaji Ntemi amesema  kesi nyingi zinaweza kuishi kwa  njia ya usuluhishi nje ya mahakama hivyo kuipunguzia Serikali gharama za uendeshaji  wa kesi. 

Aidha, Jaji Ntemi amesema mkoa wa Kagera  kesi ambazo zipo katika hatua ya kusikilizwa zinakaribia kuvuka 450 hivyo mkoa wa Kagera  unaweza kuwa wa pili au watatu kwa Tanzania kuwa na kesi nyingi za mauaji

Askofu wa Jimbo  Katoliki la Kayanga Mhasham, Almachius Rweyongeza  amebainisha kuwa  kufunguliwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  katika wilaya ya Karagwe kutasaidia wananchi kupata haki kwa wakati sambamba na kuwakumbusha viongozi wenzake wa dini kutimiza wajibu wao wa kuhubiri upendo na amani kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) mkoa wa Kagera Liberatha  Bamporiki ameeleza kufunguliwa kwa Ofisi hiyo ya Mashtaka katika wilaya ya Karagwe  kutapunguza gharama na muda mwingi waliokuwa wakiutumia kwenda Manispaa ya Bukoba kufautilia kesi zao hali itakyoaaidia kasi ya mashauri kuongezeka na kusaidia kukamilika kwa wakati

Nao baadhi ya wakazi wa Karagwe akiwemo Clemence Isherenguzi na Selestine John wamesema kuwa kufunguliwa kwa ofisi hiyo ni ukombozi kwao kutokana na awali walikuwa wakitumia gharama kubwa kusafiri toka Karagwe kwenda Manispaa ya  Bukoba umbali mrefu kufuata huduma za Mashtaka ambapo kwa sasa uwepo wa ofisi hiyo utasaidia kupunguza mzigo wa gharama  kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera
Baadhi ya Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi  Wilayani Karagwe Mkoani Kagera wakiwa wameketi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Mashtaka wilayani humo Januri 21.
Baadhi ya Watumishi  kutoka idara mbalimbali za Serikali wakiwa wameketi wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa hafla ya  ufunguzi wa  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Karagwe.  
Wakazi wa mji wa Kayanga-Karagwe waliofika kushuhudia ufunguzi wa Ofisi ya  Taifa ya Mashtaka wilayani humo wakiendelea kufuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa na viongozi wa Serikali na Dini.
Askofu wa Jimbo  Katoliki la Kayanga Mhasham, Almachius Rweyongeza akizungumzia namna ambavyo viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kukuza na kuimarisha amani kwa kuhubiri ujumbe wa upendo,umoja na mshikamano nyakati zote hali itakayochangia kupungua kwa vitendo vya uhalifu.
Mkuu wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Godfrey Mheluka akisisitiza jambo kwa wakazi wa wilaya hiyo kuitumia vema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo uwepo wake Utasaidia kupunguza malalamiko na kero zao. 
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga Mhashamu Almachius Rweyongeza kabla ya ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani Karagwe Januari 21.
Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakifuatilia maelezo na hotuba za viongozi.  
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Rebecka Kwandu akiendelea kufutilia hotuba za viongozi mbalimbali. 
Wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia  hotuba za Viongozi  mbalimbali. 
Wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia  hotuba za Viongozi  mbalimbali. 

Mwonekano wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe  mkoani Kagera kabla ya ufunguzi wake. 
Wakazi wa Kayanga-Karagwe wakiwa wamesimama wakishuhudia ufunguzi wa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe. 
 
Wa nne toka kushoto, ni Mkurugenzi wa Mashtaka  Bw.Biswalo Mganga akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo, Mkuu wa wilaya ya Karagwe Mheshimiwa Godfrey Mheluka, Askofu wa Jimbo Katoliki  Kayanga Mhasham Almachius Rweyongeza, watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na wajumbe wa kamati  ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.




Share:

WASHTAKIWA 57 WAFUTIWA MASHTAKA GEREZA LA KAYANGA-KARAGWE MKOANI KAGERA WATAKIWA KWENDA KUWA RAIA WEMA

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amon Mpanju ,Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga   wakijadiliana jambo baada ya kutoka kukagua gereza la Kayanga-Karagwe Mkoani Kagera.

Jumla ya Washtakiwa 57 wanaume 54 na wanawake 3 wamefutiwa mashtaka katika Gereza la Kayanga, wakati Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga,  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju,pamoja na  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Godfrey Mheluka walipotembelea na kukagua hali ya gereza hilo wilayani Karagwe Januari 21.

Bw. Biswalo amewaachia washtakiwa hao na kuwataka waliofutiwa mashtaka  kujirekebisha na kwenda kuwa raia wema watakaporudi uraiani ikiwa ni pamoja na kujishulisha na shughuli za uzalishaji.

Washtakiwa  wamefutiwa mashtaka mbalimbali yaliyokuwa yanawakabili ikiwepo wizi wa mifugo,ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi na ugomvi wa mipaka ya mashamba.

"Nendeni mkawe raia wema, badilikeni na msirudie tena kutenda uhalifu". Amesisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga.

Katika kundi la Washtakiwa walioachiwa huru wapo  raia toka  nchi  jirani ya Burundi ambapo  amewataka   kufuata taratibu za kisheria  endapo wanataka kuishi nchini.

Aidha Bw.Biswalo amewataka , Washtakiwa  waliobaki gerezani kuendelea kujifunza na kubadilika wakati pia wakiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kuwasamehe na kuwafungulia nuru ili siku moja warejee uraia na kuendelea na maisha yao kama kawaida.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga na viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka walipotoka kukagua gereza lae Kayanga, Karagwe,mkoani kagera

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amony Mpanju mara baada ya kutembelea na kukagua hali ya Gereza la Kayanga-Kagera Januari 21,2020.


Mwonekano wa Nje wa Jengo la Gereza la Kayanga wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.

Share:

DPP KUFUNGUA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA WILAYANI KARAGWE MKOANI KAGERA JANUARI 21

 

Katika kuhakikisha kuwa huduma za Mashtaka zinazosegezwa karibu na wananchi Mkurugenzi wa Mashtaka Bw Biswalo Mganga anatarajia kuzindua ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilayani  Karagwe Januari 21 ikiwa ni  sehemu ya kusogeza huduma karibu na wananchi 

Tembelea Mitandao yetu ya Kijamii 

Youtube Mashtaka tv , Instagram, Blog na  Website www.nps.go.tz 

Share:

SITA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA MAUAJI YA WATU 17 WA FAMILIA MOJA MKOANI MARA


Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mkoani Mara  imewahukumu watu 6 kunyongwa hadi kufa kwa kosa la Kuuwa watu 17  wa familia Moja.

Akisoma hukumu hiyo Januari  15, 2021 mbele ya Mheshimiwa Jaji Mustapha Siyani katika Kesi ya Jinai Na. 56 ya Mwaka 2018  Jamhuri dhidi ya Juma Mugaya na wenzake 8, katika Kesi  ya mauaji ya watu 17 maarufu kama kesi ya Mugaranjabo, imewatia hatiani washtakiwa sita na kuwapa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa makosa yote 17 ya kuua watu wa familia moja ili kulipiza kisasi kutokana na ndugu yao Fred Mugaya kuuawa na wananchi kwa tuhuma za wizi wa mifugo.

Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo  tarehe 16 februari 2010, katika eneo la Mugaranjambo lililopo Musoma Mkoa wa Mara ili kulipiza kisasi kwa kuwaua watu 17 wa familia moja kama sehemu ya kulipiza kisasi kutokana na ndugu yao Marehemu Fredy Mugaya kuuawa na wananchi wa Mgaranjambo mwaka 2005 kwa tuhuma za wizi wa mifugo,  baada ya mzee wa familia hiyo Marehemu Kawawa Kinguye kupiga yowe wakati wizi wa mifugo unafanyika nyumbani kwake hivyo baada ya tukio hilo washitakiwa walipanga.kulipa kisasi.

Hivyo  siku ya tukio walitekeleza kwa kuwakata kata  kwa mapanga na kuwauwa watu kumi na Saba(17) wa familia moja huku wengine watatu wakiwaacha na vilema vya kudumu.

Awali kesi hiyo  ilikuwa na washtakiwa kumi na sita  lakini wengine walifariki vifo vya kawaida wakiwa Magereza kabla ya  kesi kusikilizwa.

 Akitoa hukumu hiyo  Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa  Mustapha Siyani aliwatia hatiani washitakiwa sita  na kutoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa  na kuwaachia huru washitakiwa watatu.

Washtakiwa waliotiwa hatiani ni Juma Mugaya,Aloyce Nyabasi, Nyakaranga Wambura Biraso, Nyakaranga Masemere Mugaya, Sadock Alphonce  Ikaka na Kumbasa Buruai Bwire na walioachiwa huru ni Marwa Maua Mugaya, Ngoso Mgendi Ngoso na Sura Bukaba Sura

Kesi hiyo  iliendeshwa na Mawakili wa Serikali, Renatus Mkude, Valence Mayenga,  Robert Kidando,  Ignatus Mwinuka na Yese Temba ambapo upande wa utetezi uliwakilishwa na Mawakili tisa .

Share:

SITA WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 3 AU KULIPA FAINI YA LAKI TANO KILA MMOJA BUKOBA ,18 WAFUTIWA MASHTAKA PWANI

BUKOBA-KAGERA 

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba katika Shauri Na. Ec 05/2020 imewatia hatiani washtakiwa sita akiwepo Deziderius Dominician na wenzake watano kwa kosa la  kupatikana na nyavu haramu za uvuvi wa Samaki na kuwapa adhabu ya kulipa faini ya Shilingi Laki tano (500,000/=) kila mmoja au kwenda jela miaka mitatu pamoja na kutaifishwa mali zao zilizotokana na makosa ya uhalifu waliyoyafanya.

Hukumu hiyo imetolewa tarehe Desemba 30  baada ya washtakiwa kukiri Makosa na kuingia makubaliano  na  Mkurugenzi wa Mashtaka  ambayo ni (plea bargaining) .

Katika shauri hil0  Mahakama pia imewaamuru washtakiwa kuilipa  Serikali fidiia ya  kiasi cha shilingi Milioni Hamsini ambapo washtakiwa wamelipa  fedha hizo  kupitia  akaunti ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Sambamba na amri hizo  Mahakama pia imetoa amri ya kutaifishwa mali za washtakiwa zikiwepo gari aina ya Mitsubishi Canter lenye namba ya usajili T.683 CPL , Nyumba ya kulala Wageni, Nyumba ya kupangisha, Kiwanja kilicho na Mashine ya Kusaga na Kukoboa vyote vikiwa na thamani ya Shilingi za kitanzania Milioni Mia Moja na Hamsini na Tisa (159,000,000/=)

Kesi hiyo imeendeshwa na Wakili wa Serikali  Shomari Haruna


Mwonekano wa Mbele wa  Gereza la Mahabusu lililopo Mkuza Wilayani Kabaha Mkoani Pwani.

KIBAHA-PWANI 

Wakati huo huo Jumla ya Washtakiwa Kumi na Nane (18) wamefutiwa Mashtaka  na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Biswalo Mganga na kuachiliwa huru na Mahakama baada ya kutembelea Gereza la Mkuza lililopo wilayani Kibaha Mkoani Pwani hivi karibuni.

Zoezi hilo limefanyika Desemba  30, 2020 baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka kutembelea gereza hilo na kujionea hali halisi.

Baada ya kuwafutia Mashtaka, Mkurugenzi wa Mashtaka aliwataka washtakiwa hao walioachiwa huru wanaporudi uraiani, kuhakikisha   wanaenda kuwa raia wema.

Tembelea Mitandao yetu ya kijamii ikiwemo instagram,youtube,tovuti 

Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .