• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

WAENDESHA MASHTAKA KUWENI WAADILIFU WAKATI MNAPOTEKELEZA MAJUKUMU YENU.

 Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo akifungua mafunzo kwa  Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Carbon uliopo Chuo Kikuu cha Sokoine-SUA mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.

Na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Waendesha Mashtaka Viongozi wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu    na kujituma wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo wakati akifungua mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.

Mafunzo hayo yana lengo la kuwapatia ujuzi Waendesha Mashtaka Viongozi katika maeneo mbalimbali yanayohusu utendaji kazi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha kupata uelewa wa kutosha na wa pamoja juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa  taarifa za kesi mbalimbali katika taasisi .

 Aidha, mafunzo hayo yatawapatia fursa ya kujifunza jinsi ya kukusanya takwimu,kuzichakata na hatimaye kuzifanyia kazi pamoja na kuwapatia ujuzi utakaowasaidia kutekeleza majukumu yao.

Aidha, aliwataka kuwashirikisha watumishi wenzao mafunzo waliyoyapata watakaporejea katika vituo vyao vya kazi na kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma.

Bw. Makallo aliwataka washiriki wa mafunzo kuzingatia Maadili kwakuwa aliwaeleza kuwa wanaweza kufanya kila kitu lakini bila kuzingatia Maadili ni sawa na bure.

Waendesha Mashtaka Viongozi hao pia walipata nafasi ya kujifunza masuala mengine ikiwepo Maadili ya Kiutendaji kwa Waendesha Mashtaka katika kukusanya, kutunza na kuwasilisha taarifa za kesi mbalimbali, Ukusanyaji, uchakataji, Utunzaji na Uwasilishaji wa takwimu za kesi majukumu na wajibu wa wakaguzi katika uendeshaji wa Mashtaka, 

Aidha,Ukusanyaji wa taarifa unavyosaidia Kitengo cha Uhasibu katika kutekeleza majukumu yake pamoja mada juu ya matarajio ya Divisheni ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa kuhusiana na taarifa za takwimu zake zilizokusanywa na kuwasilishwa

Mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za Kesi mbalimbali  kwa Waendesha Mashtaka Arobaini na Mbili kutoka katika Mikoa na Wilaya  yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili, 2021.Mhasibu Mkuu Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Regina Mutagurwa akitoa mada juu ya Ukusanyaji wa taarifa unavyosaidia Kitengo cha Uhasibu katika kutekeleza majukumu yake katika mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za Kesi mbalimbali yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.

Waendesha Mashtaka Viongozi kutoka katika Mikoa na Wilaya wakimsikiliza kwa makini    Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo akifungua mafunzo kwa Waendesha  Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Carbon uliopo Chuo Kikuu cha Sokoine mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.
Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Edson Makallo na Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utumishi na Raslimali Watu Bw. Titus Mkapa na anayefuatia ni Bi. Regina Mutagurwa ambaye ni Mhasibu Mkuu Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakifuatilia mawasilisho yanayotolewa katika Mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.

Baadhi ya viongozi walioshiriki katika Mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.

Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Usimamizi wa Kesi Bw. Tumaini Kweka akitoa utambulisho katika mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Carbon uliopo Chuo Kikuu cha Sokoine mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 27 Aprili,2021 kulia kwa Bw.  Tumaini Kweka ni Bi. Neema  Mwanda ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Upelelezi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Mkurugenzi wa Utumishi na Raslimali Watu Bw. Titus Mkapa akitoa mafunzo juu ya Maadili ya Kiutendaji kwae Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa Taarifa za Takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.
Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo kwa Waendesha Mashtaka Viongozi juu ya Ukusanyaji, Utunzaji na Uwasilishaji wa taarifa za takwimu za kesi mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Carbon uliopo Chuo Kikuu cha Sokoine-SUA mjini Morogoro kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili,2021.


Share:

AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 AU KULIPA KIASI CHA TSH. 1,063,362,000.


Mahakama ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro imemuhukumu mshtakiwa Gerald Damiani Machege kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha shilingi 1,063, 362,000.

Imeelezwa Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Ulanga Mhe. Matugwa Masimbi katika kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 22 ya mwaka 2019 kuwa mshtakiwa Gerald Damiani Machege alikamatwa baada ya kukutwa na vipande 15 vya meno  kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri pasipo kuacha shaka, na hivyo kupelekea  mshtakiwa Gerald Machege kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha  shilingi  bilioni 1,063,362,000.

Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Francis Malembo na Simon Mgonja 
Share:

WAHUKUMIWA MIAKA 20 JELA AU KULIPA KIASI CHA TSH.600,690,000/=


Mahakama ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro, imewahukumu washtakiwa Hassani Chikoko na Sudi Salum kwenda jela miaka 20 au kulipa faini kiasi cha shilingi Milioni mia sita (600,690,000/=) kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali.

Kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi Namba 6 ya mwaka 2019 iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Ulanga Mhe. Mhanusi,  Mahakamani hapo ilielezwa kuwa mshtakiwa Hassani Chikoko na mwenzake Sudi Salum walikutwa na nyara za Serikali ambazo ni vipande 4 vya meno ya tembo.

ambapo hakimu aliwahukumu  kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha Tsh.600,690,000/= kwa kila mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri makahamani hapo pasipo kuacha shaka lolote .

Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .