• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

KAIMU NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA AISHUKURU UNICEF

 Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda amelishukuru Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF) kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kufadhili  Mafunzo na maelekezo ya utekelezaji wa ukaguzi  wa vizuizi vya watoto wanaokinzana na sheria wakishirikiana na timu ya maandalizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo  yamefanyika leo tarehe 15 Novemba, 2021  katika Ukumbi wa Rafiki Hotel Jijini Dodoma.



"Elimu mnayopata hapa mkawape na wenzenu, msikae kimya kwani haitaleta tija katika utendaji wa kazi zetu. Na pia mkifika mkawe waalimu wa Mawakili wenzenu mliowaacha ili kesi za watoto ziweze kuendeshwa kwa ufanisi mkubwa na weledi."

Alizungumza hayo Bi. Neema Mwanda wakati akitoa neno la kufunga mafunzo hayo.


Nae pia Mratibu wa Ulinzi na Usalama wa Mtoto kutoka Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF) Bi. Victoria Mgonela ametoa shukrani kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kueleza jinsi wanavyoshirikiana kikamilifu na ofisi hiyo katika kushughulikia mashauri ya watoto.

 


Share:

DPP AMEWATAKA MAWAKILI KUZINGATIA HAKI ZA WATOTO


 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu awataka Mawakili wa Serikali kufanya kazi zao kwa umakini, kupitia majalada yote kwa umakini ili kuweza kulinda haki za watoto.


Mkurugenzi wa Mashtaka akizungumza hayo wakati akifungua Mafunzo na maelekezo ya utekelezaji wa ukaguzi  wa vizuizi vya watoto wanaokinzana na sheria ambayo yamedhaminiwa na Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF) yanayofanyika leo tarehe 15 Novemba, 2021  katika Ukumbi wa Rafiki Hotel Jijini Dodoma. 


Mkurugenzi Mwakitalu alieleza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inayo jukumu la kusimamia haki jinai kwa maana ya kuendesha kesi za jinai, lakini katika Uendeshaji wa Mashtaka hayo, ofisi ina jukumu pia la kuratibu Upelelezi, na pia kufanya ukaguzi kwenye mahabusu, magereza na mahala pengine ambapo washtakiwa wa uhalifu wanatunzwa.


Mwakitalu aliendelea kueleza kuwa mafunzo hayo pia yataongeza tija kwenye utendaji wa kazi, na pia lile kundi la Watoto wanaokinzana na sheria au wale ambao ni waanga ni kundi muhimu  sana katika utendaji wa kazi za ofisi hii.


Aidha alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwasababu yatasaidia kuhakikisha kuwa haki za watoto za zinalindwa, na pia kupata uelewa utakaowezesha kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua stahiki katika haki za watoto.


Nae pia Kaimu Mkurugenzi Divisheni ya Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi Bw. Tumaini Kweka alieleza kuwa mafunzo hayo ni ya kwanza katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo yamewakutanisha kushughulikia mashauri katika ofisi za mikoa na wilaya. Na lengo la mafunzo hayo ni kuboresha na kuweka namna bora ya jinsi ya kuendesha mashauri hayo Mahakamani na vilevile kuona namna bora ya kushughulika na kesi zinazowahusu watoto ambao wamekinzana na sheria.

"Dhima au lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uelewa wa pamoja juu ya utaratibu mzuri wa kukagua magereza, kukagua mahabusu za polisi na mahabusu za watoto ambao wamekinzana na sheria wanakuwa wamehifadhiwa." Akizungumza hayo Mkurugenzi Kweka.

Share:

DPP MWAKITALU AZINDUA MWONGOZO JUU YA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWENYE MASUALA YA JINAI

 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amewaasa wananchi kuachana na vitendo vya kiuhalifu kwani uhalifu haulipi


Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amesema uwepo wa uhalifu uliokuwa ukizihangaisha baadhi ya nchi sasa limekuwa ni suala la kidunia kwakuwa  uhalifu huo umekuwa ukizuia maendeleo ya jamii zetu.


Akizindua Mwongozo ya  Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Masuala ya Jinai katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Bw. Mwakitalu alisema utoaji wa haki ikiwemo kuzuia vitendo vya uhalifu, ulinzi na Usalama wa raia ni msingi wa maendeleo ya jamii yoyote.



Mkurugenzi Mwakitalu alitaka uwepo wa ushirikiano wa nchi mbalimbali katika kupambana na uhalifu kwani juhudi za kupambana na uhalifu haziwezi kuishia katika nchi moja tu kwakuwa uhalifu wa kupangwa ni uhalifu unaovuka mipaka.


Mwakitalu aliendelea kueleza kuwa Tanzania imeridhia  Mikataba mbalimbali ya Kimataifa  ya kupambana na uhalifu wa kupangwa na unaovuka mipaka ikiwemo mikataba juu ya Ushirikiano wa Kimataifa ya kupambana na uhalifu.




 Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.  David Concar alisema uzinduzi wa Mwongozo juu ya Ushirikiano wa Kimataifa juu ya kukabiliana na Jinai  sio jambo dogo kwakuwa mamilioni ya watu duniani wanaathiriwa na  kukua kwa Masuala ya uhalifu, kuongezeka kwa Masuala ya kigaidi na rushwa.



Balozi Concar alisema uzinduzi wa Mwongozo juu ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Masuala ya Jinai ni matokeo ya Ushirikiano katika ya ubalozi wa Uingereza na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kufanikisha juhudi mbalimbali za kupambana na uhalifu.


 Naye Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Manfred Kanti aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua iliyofikia kama chombo muhimu cha kupambana na uhalifu wa Kimataifa na ule unaovuka mipaka



Share:

WAKUU WA MASHTAKA WA NCHI ZA AFRIKA NA NCHI ZA KIARABU WAKUTANA MISRI KWA MARA YA KWANZA..

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Mashtaka barani Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka wa Tanzania Ndugu Sylvester Mwakitalu  akihudhuria Mkutano wa Kamati ya Uongozi wa Umoja wa Wakuu wa Mashtaka barani Afrika unaofanyika  katika jiji la Cairo nchini Misri.

Mkutano huu unafanyika sambamba na Wakuu wa Mashtaka wa nchi za Kiarabu na unahudhuriwa na jumla ya washiriki 120 kutoka nchi za Afrika na za Kiarabu
 Ni kwa mara ya kwanza Wakuu wa Mashtaka wa Afrika na  Nchi za  Kiarabu wanafanya Kongamano pamoja kabla ya kila Umoja kufanya Mkutano wake .

Share:

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini aishukuru PAMS Foundation

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu ametoa shukrani zake kwa Shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kudhamini mafunzo ya Upelelezi na uendeshaji wa kesi za wanyamapori na misitu kwani mafunzo hayo waliyoyapata washiriki hao yatawasaidia kuwaongezea ujuzi na uzoefu katika kazi zao. 

Mafunzo hayo yameshirikisha wadau kutoka Taasisi mbalimbali wakiwemo Mawakili wa Serikali, Waendesha Mashtaka, Wapelelezi na Maafisa wa Wanyamapori


Bw. Mwakitalu alieleza kuwa ana imani kwa washiriki wote wa mafunzo hayo kuwa hawataenda kumuangusha bali watafanya kazi kwa matokeo chanya na kwa uadilifu wa hali ya juu kwani mafunzo hayo yatakuwa yamewajengea uwezo wa kupeleleza na kuendesha Mashtaka ipasavyo.


Mkurugenzi wa Mashtaka aliwahakikishia washiriki mawazo yao waliyoyatoa yatafanyiwa kazi na kwa yale ambayo yanahitaji marejeo ya kisheria wadau husika watashirikishwa.

Na pia Bw. Sylvester aliwashukuru Majaji wote, pamoja na watoa mada wengine  waliotenga muda wao na kukubali kushiriki kwenye utoaji wa mada mbalimbali katika mafunzo hayo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Makosa dhidi ya Mazingira na Maliasili kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Rosemary Shio alimshukuru Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kukubali kushiriki kufunga mafunzo hayo, na pia alishukuru uongozi wa PAMS Foundation kwa kudhamini mafunzo hayo.

Aliendelea kueleza kuwa siku tano za mafunzo ya Upelelezi na uendeshaji wa kesi za wanyamapori na misitu yamewajengea uwezo maofisa hao katika maeneo mbalimbali ikiwepo hati za Mashtaka,  mawasilisho yanayohusiana na hoja za wanyamapori na misitu.

Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .