Mkurugenzi wa Mashtaka nchini aishukuru PAMS Foundation

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu ametoa shukrani zake kwa Shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kudhamini mafunzo ya Upelelezi na uendeshaji wa kesi za wanyamapori na misitu kwani mafunzo hayo waliyoyapata washiriki hao yatawasaidia kuwaongezea ujuzi na uzoefu katika kazi zao. 

Mafunzo hayo yameshirikisha wadau kutoka Taasisi mbalimbali wakiwemo Mawakili wa Serikali, Waendesha Mashtaka, Wapelelezi na Maafisa wa Wanyamapori


Bw. Mwakitalu alieleza kuwa ana imani kwa washiriki wote wa mafunzo hayo kuwa hawataenda kumuangusha bali watafanya kazi kwa matokeo chanya na kwa uadilifu wa hali ya juu kwani mafunzo hayo yatakuwa yamewajengea uwezo wa kupeleleza na kuendesha Mashtaka ipasavyo.


Mkurugenzi wa Mashtaka aliwahakikishia washiriki mawazo yao waliyoyatoa yatafanyiwa kazi na kwa yale ambayo yanahitaji marejeo ya kisheria wadau husika watashirikishwa.

Na pia Bw. Sylvester aliwashukuru Majaji wote, pamoja na watoa mada wengine  waliotenga muda wao na kukubali kushiriki kwenye utoaji wa mada mbalimbali katika mafunzo hayo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Makosa dhidi ya Mazingira na Maliasili kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Rosemary Shio alimshukuru Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kukubali kushiriki kufunga mafunzo hayo, na pia alishukuru uongozi wa PAMS Foundation kwa kudhamini mafunzo hayo.

Aliendelea kueleza kuwa siku tano za mafunzo ya Upelelezi na uendeshaji wa kesi za wanyamapori na misitu yamewajengea uwezo maofisa hao katika maeneo mbalimbali ikiwepo hati za Mashtaka,  mawasilisho yanayohusiana na hoja za wanyamapori na misitu.

Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .