• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

DPP AFUNGUA MAFUNZO YA IDARA YA DoCP KUHUSU NAMNA BORA YA UDHIBITI WA UPELELEZI NA UENDESHAJI WA MASHTAKA KWA MAWAKILI WA SERIKALI

 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amefungua Mafunzo ya Idara ya Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi (DoCP) kuhusu namna bora ya Udhibiti wa Upelelezi na Uendeshaji wa Mashtaka kwa Mawakili wa Serikali yanayofanyika tarehe 29 na 30 Januari, 2024 Makao makuu Jijini Dodoma.

Katika ufunguzi huo Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuendelea kutekeleza mkakati wa kuboresha utendaji kazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ikiwa ni pamoja na kuwezesha kuimarisha kazi kuu mbili ya Kuratibu  upelelezi na Kuendesha Mashtaka.

Amesema katika mada zitakazowasilishwa zimebeba lengo kubwa la kujenga uwezo wa watendaji ili kuongeza tija kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

“Utendaji wetu wa kazi unapimwa kwa vitu vichache sana kwa kuangalia kiwango cha ushindi wetu wa kesi mahakamani.” Ameyasema hayo DPP Mwakitalu.

Aidha, Mkurugenzi wa Mashtaka ameongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ubora katika uendeshaji wa mashtaka na kuratibu upelelezi ili kuwawezesha kupata matokeo chanya.

“Tunataka tufike mahali ambapo tukimpeleka mtuhumiwa mahakamani ajue kwa 90% tumeridhika na ushahidi uliokusanywa na aina ya mashahidi wetu.” Amebainisha hayo Mkurugenzi Mwakitalu. 

Pia Mkurugenzi Mwakitalu amesema kuwa kuna changamoto nyingi zinazojitokeza katika usimamizi wa mashtaka kwani ushindi wa kesi mahakamani bado hauridhishi.

“Ninaamini baada ya mafunzo haya tutapata kitu cha kutuwezesha kuongeza tija katika kazi zetu na kuhakikisha kwamba mafunzo haya yanawafikia Mawakili wote wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mikoa yote.” Ameyasema hayo Mkurugenzi Mwakitalu.



Share:

DPP AWATAKA WATUMISHI WA OTM KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA


Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Sylvester Mwakitalu akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakati wa ufunguzi wa Baraza la pili la  Wafanyakazi wa Ofisi leo Januari 025,2024 katika hoteli ya Lenana Jijini Mwanza

Na Marrygoreth Ntandu.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amewataka watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (OTM) kufanya kazi zao kwa bidii na kuzingatia weledi wa taaluma yao ikiwemo kufanya kazi kwa uaminifu ili kutenda haki kwa umma.

Mwakitalu ametoa rai hiyo mapema leo Januari 25, 2024 katika ukumbi wa hoteli ya Lenana ya Jijini Mwanza wakati akifungua mkutano wa baraza la kwanza la mwaka la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka lililojumuisha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa na Wilaya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi.

Bw. Mwakitalu amesema katika kipindi cha mwaka mmoja,Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeweza kufikia sehemu kubwa ya utekelezaji wa malengo iliyokuwa imejiwekea  yakiwepo masuala ya mashauri ya jinai kuendeshwa na kutolewa maamuzi kwa haraka na kupelekea kupungua kwa mrundikano wa kesi za muda mrefu katika mahakama nyingi nchini.

Katika hatua nyingine Mwakitalu ameeleza kuwa kutokana na kuimarika kwa utendaji wa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kumesaidia kupunguza mrundikano wa mahabusu  katika magereza mbalimbali nchini pamoja na kupungua kwa malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wananchi kwa njia mbalimbali ikiwemo barua pepe, simu na wengine kufika ofisini.

Amesema, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeundwa ili kurahisisha utoaji wa huduma za mashtaka kwa wananchi kwa kuwezesha kesi nyingi kuendeshwa kwa wakati  na kuhakikisha haki inatendeka kwa lengo la kuwepo kwa haki, amani na usalama katika nchi yetu.

Aidha, Mwakitalu amesema katika kuhakikisha watumishi wote wanafanya kazi zao kwenye mazingira salama, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeendelea kutekeleza   miradi mbalimbali ya majengo ya ofisi za mikoa 10 ambapo mikoa miwili kati yake imekamilika ikiwemo mkoa wa Pwani na Ilala eneo la Kinyerezi ambapo mwishoni mwa mwezi Januari, 2024, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inatarajiwa  kupokea majengo ya Ofisi kutoka mikoa ya Shinyanga na Manyara.

Bw. Mwakitalu amesema kuwa mpaka sasa jumla ya ofisi 92 za mashtaka zimefunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mikoa 30 ya kimashtaka na wilaya 62 za Tanzania Bara ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya ofisi katika kusogeza huduma za kimashtaka karibu na wananchi.Vile vile Mwakitalu amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itaendelea kufungua ofisi katika wilaya 47 zilizobaki ili kuendelea kutoa huduma bora kwa watanzania wenye kesi mbalimbali.

Naye Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambaye ni Afisa Tawala Mkuu Bw.Juma Katanga amesema kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kinalenga katika kujadili na kupitia Mipango na Makisio ya Mapitio ya bajeti katika kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai 2023 hadi Januari, 2024.

Katanga amesema wafanyakazi wa OTM bado wanakabiliwa na baadhi ya changamoto zikiwepo uhaba wa wafanyakazi katika maeneo mbalimbali, upungufu wa vitendea kazi katika ofisi nyingi za wilaya zilizofunguliwa hivi karibuni huku akisema kuwa Baraza la Wafanyakazi limekuwa sehemu ya msukumo kwa menejimenti kupunguza baadhi ya changamoto ikiwemo kununua magari mapya, kuajiri  watumishi pamoja na kununua samani za ofisi katika Wilaya na Mikoa.

Wakati huohuo,   Katanga ameiomba Serikali kuona namna ya kuongeza bajeti katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kutokana na majukumu nyeti inayoyatekeleza kwa Maendeleo ya Taifa  ikiwemo kupatikana kwa nyumba za wafanyakazi zitakazosaidia kuishi katika mazingira salama.

“Mfano Wakili wa Serikali anaendesha kesi za Ugaidi,Ujambazi, Masuala ya pesa haramu alafu anaishi kwenye nyumba ya kupanga pengine ni ya jambazi  fikiria jinsi mazingira hayo yalivyo hatari, serikali inapaswa kuliona hili kwa jicho la zaidi” amesema Katanga

Awali akizungumza kabla ya ufunguzi wa mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi.Javelin Rugaihuruza amesema mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashataka ulikusudiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2023   lakini kutokana na sababu zilizojitokeza nje ya uwezo wa taasisi ulishindwa kufanyika na umefanyika leo tarehe 25 mwezi Januari 2024.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika leo  tarehe 25 Januari, 2024 Jijini MwanzaKaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Javelin Rugaihuruza akitoa neno la utangulizi pamoja na kumkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka uliofanyika tarehe 25 Januari, 2024 Jijini Mwanza.Picha za baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kutoka mikoa yote ya Tanzania bara wakiwa katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika leo Januari 25,2024 Jijini Mwanza.





Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amefanya Uzinduzi wa Mikopo ya Mashtaka Saccos kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka uliofanyika tarehe 25 Januari, 2024 Jijini Mwanza.






Share:

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA YASAINI MAKUBALIANO (MOU) DHIDI YA KUKABILIANA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu kulia akibadilishana Hati ya Makubalino (MOU) na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) kushoto baada ya kusaini Makubaliano hayo  juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu . Makubaliano hayo yamefanyika leo Januari 24,2024 Jijini Mwanza.

MWANZA-

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeingia Makubaliano (MOU) na Shirika  lisilo la Kiserikali la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) juu ya utekelezaji wa Mradi wa Kukabiliana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu katika maeneo ya Upelelezi na Mashtaka.

Makubalianao hayo yamefanyika leo Jijini Mwanza kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria           Wasio na Mipaka (Lawayers Without Borders) Bi  .Roben Tylor.

Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amesema kuwa moja ya ajenda za kukabiliana nazo ni uhalifu wa kusarifisha binadamu kinyume cha Sheria ya a Haki za Binadamu.Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akizungumza  katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano (MOU) juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.

Amesema makubaliano hayo yalipaswa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2023 lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo  ilishindikana na kufanyika mwezi huu wa Januari ambapo makubaliano haya yatasaidia kuongeza na kuwajengea uelewa wapelelezi na Wachunguzi katika uendeshaji wa kesi zinazohusiana na usafirishaji wa haramu wa binadamu.

Mwakitalu amesema mahusiano ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wanasheria Wasio na Mipaka (Laywers Without Borders) yameanza mwaka 2017 pale wanasheria kutoka taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka walipotembelea ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kuonyesha utayari wa kushirikiana kwa kutoa mafunzo kwa Waendesha Mashtaka ili kuwajengea uwezo mzuri wa kuendesha kesi zinazohusiana na usafirshaji haramu wa binadamu.

Katika hatua nyingine Mwakitalu amesema suala la Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu limekuwa tatizo kwa nchi nyingi, kanda na duniani kote hali ambayo, nguvu ya pamoja ya kupambana na tatizo hilo inahitajika.

Ameeleza kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazokabiliana na tatizo hilo   hivyo vita dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu ikiwemo hatua ya kutambua na kuchukua hatua kwa wale wanaobainika kuhusika na usafirishaji huu ambapo Serikali tayari inatekeleza Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu ya mwaka 2008.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Wanashria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders). Bi Robin Tylor amesema Makubalina hayo ina dhamira ya kuwaleta pamoja wadau wa mapambano dhidi ya biashara ya usafiriahaji haramu wa binadamu   kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha wahalifu na magenge ya biashara hiyo wanafikishwa mbele ya vyombo vya dola na waathirika wa biashara hizo wanapata haki.

“Juhudi hizi zitafikiwa iwapo wadau wote tutaunganisha nguvu ya kupambana dhidi ya biashara hiyo ambayo ninaamini chini ya uongozi thabiti wa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) na kwa kusaini makubaliano haya malengo yatafikiwa”alisema Bi. RobinMkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lwayers without Borders) Bi. Robin Tylor akizungumza  katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.

Bi. Robin ameongeza kuwa kuna haja wadau kutumia sheria ya mapambano dhidi ya Usafirishaji wa Binadamu ya Mwaka 2008 iliyofanyiwa maboresho 2022 katika kuandaa Hati za Mashtaka pale wahalifu wanapokamatwa na wakati upelelezi na ushahidi kukamilika.

Bi Robin amehitimisha hotuba yake alisema kuwa, kwa sasa dunia iko katika matumizi ya teknolojia hivyo ni vema tukajikita katika kutumia teknolojia kwenye upelelezi na ukusanyaji wa vielelezo vya kesi zinazohusiana na biashara haramu na ulinzi wa waathirika na mashahidi wa biashara hiyo.

Wakati huo huo, Robin ameishukuru Serikali ya Marekani kupitia Ofisi ya Ufuatiliaji na Upambanaji wa Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu (J/TIP) kutoa ufadhili wa mradi huo.

Naye Mkuu wa Kikosi kazi ya Kukabiliana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu Tulibake Faidon Kasongwa amewashukuru wadau mbalimbali katika jitihada zao za kifedha na kimafunzo katika kuwajengea uwezo ndani ya Kikosi Kazi ambacho kimekuwa kikipambana na kuzuia Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu kwa kuwa wamekuwa chachu katika utendaji kazi wao.

Kasongwa amelishukuru Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) kwa  kuwajengea ujuzi wadau wa Haki Jinai ikiwa ni njia mojawapo ya ushirikiano na kuwawezesha kuwa na uwezo wa kuwajibika kwa haraka na kwa wakati  yanapotokea masuala ya biashara haramu ya binadamu.

Amesema kuwa biashara haramu ya binadamu ni janga la dunia  ambalo linahitaji ushirikiano wa wadau wote wa ndani na nje ya nchi  katika kukabiliana na dhuluma zinazofanyika kupitia biashara hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini  Kamishna wa Polisi Salehe Ambika Mussa amesema suala la biashara haramu ya binadamu ni janga linalohitaji ushirikiano wa wadau wanaohitaji  kuunganisha nguvu za pamoja ili kuweza kuyafikia mafanikio kusudiwa.

Kamishna Mussa amebainisha kuwa licha ya kuwa na jukumu kubwa la kupeleleza kesi mbalimbali kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhakikisha haki inatendeka, suala la biashara  haramu ya binadamu ni jambo linalohitaji wadau wote kushirikiana na jeshi la polisi linapokuwa linafanya uchunguzi.

Mradi wa Kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu umeanza kutekelezwa mwezi Mei mwaka 2023 na  unatarajiwa kukamilika mwaka 2026.  Mradi huu umelenga katika kuwajengea uwezo Waendesha Mashtaka na Watekelezaji wa Sheria katika kuendesha Upelelezi, kuratibu ushahidi,na kuendesha Mashtaka ya Makosa ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji katika mapambano ya Usafirshaji  Haramu wa Binadamu.Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Javelin Rugaihuruza akimkaribisha Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu kuzungumza katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai Nchini Kamishna wa Polisi CP. Salehe Ambika Mussa akizungumza  katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.Tulibake Faidon Kasongwa  Mkuu wa Kikosi Kazi cha  Kukabiliana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu   akizungumza  katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu.Mkurugenzi Divisheni ya Utaifishaji Mali, Makosa yanayovuka Mipaka na Uhalifu Mahususi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Faraja Nchimbi akizungumza  katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu  na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lwayers Without Borders) Wakisaini Makubaliano (MOU) juu ya Utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu. Makubaliano hayo yamefanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (kulia) akibadilishana Hati ya Makubaliano na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lwayers Without Borders)  baada ya kusaini Makubaliano hayo (MOU) juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu kulia na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lwayers Without Border) kushoto Wakionesha hati za Makubaliano (MOU) mara baada ya kusainiwa.Baadhi ya washiriki wa hafla ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa Mradi wa wa Kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu wakifuatilia hotuba za Viongozi mbalimbali katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (kushoto) akikabidhiwa picha inayoonyesha ramani ya bara la Afrika na utajiri wa Wanyama pori pamoja na Picha ya Mchoraji wa Ramani hiyo kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) Bi. Robin Tylor.
Baadhi ya Wakuu wa  Mashtaka kutoka Mikoa mblimbali wakifuatilia hotuba za Viongozi  katika hafla ya kusaini Makubaliano (MOU) kati ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (LWOB).Baadhi ya Watendaji kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtka wakifuatilia hotuba za Viongozi mbalimbali katika hafla ya kusaini Makubaliano kati ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka.

Baadhi ya Wakurugenzi Wasaidizi  kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtka wakifuatilia hotuba za Viongozi mbalimbali katika hafla ya kusaini Makubaliano kati ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa hafla ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa Mradi wa wa Kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza


















 

 

Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .