DPP AFUNGUA MAFUNZO YA IDARA YA DoCP KUHUSU NAMNA BORA YA UDHIBITI WA UPELELEZI NA UENDESHAJI WA MASHTAKA KWA MAWAKILI WA SERIKALI

 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amefungua Mafunzo ya Idara ya Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi (DoCP) kuhusu namna bora ya Udhibiti wa Upelelezi na Uendeshaji wa Mashtaka kwa Mawakili wa Serikali yanayofanyika tarehe 29 na 30 Januari, 2024 Makao makuu Jijini Dodoma.

Katika ufunguzi huo Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuendelea kutekeleza mkakati wa kuboresha utendaji kazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ikiwa ni pamoja na kuwezesha kuimarisha kazi kuu mbili ya Kuratibu  upelelezi na Kuendesha Mashtaka.

Amesema katika mada zitakazowasilishwa zimebeba lengo kubwa la kujenga uwezo wa watendaji ili kuongeza tija kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

“Utendaji wetu wa kazi unapimwa kwa vitu vichache sana kwa kuangalia kiwango cha ushindi wetu wa kesi mahakamani.” Ameyasema hayo DPP Mwakitalu.

Aidha, Mkurugenzi wa Mashtaka ameongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ubora katika uendeshaji wa mashtaka na kuratibu upelelezi ili kuwawezesha kupata matokeo chanya.

“Tunataka tufike mahali ambapo tukimpeleka mtuhumiwa mahakamani ajue kwa 90% tumeridhika na ushahidi uliokusanywa na aina ya mashahidi wetu.” Amebainisha hayo Mkurugenzi Mwakitalu. 

Pia Mkurugenzi Mwakitalu amesema kuwa kuna changamoto nyingi zinazojitokeza katika usimamizi wa mashtaka kwani ushindi wa kesi mahakamani bado hauridhishi.

“Ninaamini baada ya mafunzo haya tutapata kitu cha kutuwezesha kuongeza tija katika kazi zetu na kuhakikisha kwamba mafunzo haya yanawafikia Mawakili wote wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mikoa yote.” Ameyasema hayo Mkurugenzi Mwakitalu.



Share:

No comments:

Post a Comment

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .