MWANZA-
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeingia Makubaliano (MOU) na Shirika lisilo la Kiserikali la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) juu ya utekelezaji wa Mradi wa Kukabiliana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu katika maeneo ya Upelelezi na Mashtaka.
Makubalianao hayo yamefanyika leo Jijini Mwanza kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawayers Without Borders) Bi .Roben Tylor.
Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amesema kuwa moja ya ajenda za kukabiliana nazo ni uhalifu wa kusarifisha binadamu kinyume cha Sheria ya a Haki za Binadamu.
Amesema
makubaliano hayo yalipaswa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2023 lakini kutokana na
sababu zilizo nje ya uwezo ilishindikana
na kufanyika mwezi huu wa Januari ambapo makubaliano haya yatasaidia kuongeza
na kuwajengea uelewa wapelelezi na Wachunguzi katika uendeshaji wa kesi
zinazohusiana na usafirishaji wa haramu wa binadamu.
Mwakitalu
amesema mahusiano ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wanasheria Wasio na Mipaka (Laywers
Without Borders) yameanza mwaka 2017 pale wanasheria kutoka taasisi ya
Wanasheria Wasio na Mipaka walipotembelea ofisi ya Taifa ya Mashtaka na
kuonyesha utayari wa kushirikiana kwa kutoa mafunzo kwa Waendesha Mashtaka ili
kuwajengea uwezo mzuri wa kuendesha kesi zinazohusiana na usafirshaji haramu wa
binadamu.
Katika
hatua nyingine Mwakitalu amesema suala la Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu
limekuwa tatizo kwa nchi nyingi, kanda na duniani kote hali ambayo, nguvu ya
pamoja ya kupambana na tatizo hilo inahitajika.
Ameeleza
kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazokabiliana na tatizo hilo hivyo vita
dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu ikiwemo hatua ya kutambua na kuchukua
hatua kwa wale wanaobainika kuhusika na usafirishaji huu ambapo Serikali tayari
inatekeleza Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu ya mwaka 2008.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Wanashria Wasio na Mipaka (Lawyers
Without Borders). Bi Robin Tylor amesema Makubalina hayo ina dhamira ya
kuwaleta pamoja wadau wa mapambano dhidi ya biashara ya usafiriahaji haramu wa binadamu
kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha
wahalifu na magenge ya biashara hiyo wanafikishwa mbele ya vyombo vya dola na waathirika
wa biashara hizo wanapata haki.
“Juhudi
hizi zitafikiwa iwapo wadau wote tutaunganisha nguvu ya kupambana dhidi ya biashara
hiyo ambayo ninaamini chini ya uongozi thabiti wa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP)
na kwa kusaini makubaliano haya malengo yatafikiwa”alisema Bi. RobinMkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lwayers without Borders) Bi. Robin Tylor akizungumza katika hafla fupi ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2024 Jijini Mwanza.
Bi.
Robin ameongeza kuwa kuna haja wadau kutumia sheria ya mapambano dhidi ya Usafirishaji
wa Binadamu ya Mwaka 2008 iliyofanyiwa maboresho 2022 katika kuandaa Hati za Mashtaka pale
wahalifu wanapokamatwa na wakati upelelezi na ushahidi kukamilika.
Bi
Robin amehitimisha hotuba yake alisema kuwa, kwa sasa dunia iko katika matumizi
ya teknolojia hivyo ni vema tukajikita katika kutumia teknolojia kwenye upelelezi
na ukusanyaji wa vielelezo vya kesi zinazohusiana na biashara haramu na ulinzi
wa waathirika na mashahidi wa biashara hiyo.
Wakati huo huo, Robin ameishukuru Serikali ya Marekani kupitia Ofisi ya Ufuatiliaji na Upambanaji wa Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu (J/TIP) kutoa ufadhili wa mradi huo.
Naye
Mkuu wa Kikosi kazi ya Kukabiliana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu Tulibake
Faidon Kasongwa amewashukuru wadau mbalimbali katika jitihada zao za kifedha na
kimafunzo katika kuwajengea uwezo ndani ya Kikosi Kazi ambacho kimekuwa kikipambana
na kuzuia Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu kwa kuwa wamekuwa chachu
katika utendaji kazi wao.
Kasongwa
amelishukuru Shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders)
kwa kuwajengea ujuzi wadau wa Haki Jinai
ikiwa ni njia mojawapo ya ushirikiano na kuwawezesha kuwa na uwezo wa
kuwajibika kwa haraka na kwa wakati yanapotokea masuala ya biashara haramu ya binadamu.
Amesema
kuwa biashara haramu ya binadamu ni janga la dunia ambalo linahitaji ushirikiano wa wadau wote
wa ndani na nje ya nchi katika
kukabiliana na dhuluma zinazofanyika kupitia biashara hiyo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kamishna wa Polisi Salehe Ambika Mussa amesema
suala la biashara haramu ya binadamu ni janga linalohitaji ushirikiano wa wadau
wanaohitaji kuunganisha nguvu za pamoja
ili kuweza kuyafikia mafanikio kusudiwa.
Kamishna
Mussa amebainisha kuwa licha ya kuwa na jukumu kubwa la kupeleleza kesi
mbalimbali kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhakikisha haki
inatendeka, suala la biashara haramu ya binadamu
ni jambo linalohitaji wadau wote kushirikiana na jeshi la polisi linapokuwa
linafanya uchunguzi.






No comments:
Post a Comment