Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akihutubia katika hafla fupi ya ukaribisho wa kuanza kazi rasmi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini DodomaMkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amewataka watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kufanya kazi kwa kuzingatia Haki, Ushirikiano kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo ya jamii na Taifa.
Bw. Sylvester amebainisha hayo mapema Mei 24, 2021 wakati akizungumza na viongozi na watumishi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma alipowasili kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester amewaasa Watumsihi wa Ofisi yake pale wanapoona wamekwama wasisite kuhakikisha wanaomba ushauri ili kuweza kutatua changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
“Niwaombe pale mtumishi unapoona ndivyo sivyo njoo tujadiliane ili kuweka mambo sawa, na mimi nitakapobaini tatizo kwenu, sitosita kukuita na kukurekebisha”
Mkurugenzi wa Mashtaka ameongeza kwa kuwataka watumishi wote wa Ofisi ya Taifa ya Mashataka kushikiriana pamoja ili kuwezesha kufikia lengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Niendelee kusema nanyi ndugu zangu watumishi wenzangu, tuna jukumu kubwa mbele yetu la kusimamia mashtaka lakini kubwa zaidi ni kutekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki ambayo inapaswa kutendeka kwa wakati”
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande amesema kuwa ili kufikia malengo yatakayofanikisha utaoji wa haki ni lazima wao kama waendesha Mashtaka wasimame kwa umoja na mshikamano hali itakayochangia kufikia malengo yao kwa wakati.
wakati huo huo Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Biswalo Mganga katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Mei 25 Mei, 2021 katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.














\





















