• Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

DPP AWATAKA MAKATIBU SHERIA KUFUATA MAADILI YA KAZI.

 



Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amewataka Makatibu Sheria kufanya kazi zao kwa kuzingatia miiko na misingi ya utumishi wa umma.


Mkurugenzi Mwakitalu ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu Sheria kutoka Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini kilichoanza leo tarehe 17 hadi 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.


Bw. Mwakitalu aliendelea kuwaasa Makatibu Sheria kuwa baada ya kumaliza kikao kazi hiki wanapaswa kubadilika na kwenda kufanya kazi zao kwa uadilifu, na kwa moyo wa kujituma.


"Tumekabidhiwa dhamana Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tucheze kama timu moja, tufanye kazi kwa kushirikiana ili kwa pamoja tusimame na tusonge mbele. Pamoja na changamoto mbalimbali tulizonazo lakini tujitahidi kufanya kazi kwa bidii." Amezungumza hayo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.

Nae pia Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda alieleza kuwa lengo kuu la kikao kazi hiki ni kujifunza na kuongeza uelewa zaidi juu ya masuala mbalimbali ya kiutendaji katika kazi zinazofanywa na Makatibu Sheria, hivyo basi kupitia kikao kazi hiki ana mategemeo ya kuwa washiriki wote watatoka wakiwa wameongeza uelewa zaidi katika kazi zao tofauti na walivyokuja.

Share:

DPP AWATAKA MAKATIBU SHERIA KUFUATA MAADILI YA KAZI

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akitoa neno la ufunguzi wa kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu sheria kilichoanza leo tarehe 17 Disemba, 2021 hadi tarehe 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.

Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu kwa lengo la kufungua  kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu Sheria kilichoanza leo tarehe 17 Disemba, 2021 hadi tarehe 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Bw. Titus Mkapa akielezea malengo ya kukutana katika kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu sheria kilichoanza leo tarehe 17 Disemba, 2021 hadi tarehe 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.






katika kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu sheria kilichoanza leo tarehe 17 Disemba, 2021 hadi tarehe 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.



Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu Sheria wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (hayupo pichani)  wakati akihutubia katika kikao hicho kilichoanza leo tarehe 17 hadi 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Mipango Bw. Mussa Magunguli akiwasilisha mada juu ya Mipango, Bajeti na Taarifa za Utekelezaji katika kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu sheria kilichoanza leo tarehe 17 Disemba, 2021 hadi tarehe 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Bw. Leonard Mehta akitoa mada juu ya Wasilisho la Rasimu ya Mapendekezo ya Miundo ya Kiutumishi ya Makatibu Sheria katika kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu Sheria kilichoanza leo tarehe 17 Disemba, 2021 hadi tarehe 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.













Picha ya pamoja ikijumuisha Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (katikati), Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Bw. Titus Mkapa (kulia), Kaimu Naibu Mkurugenzi ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda wakiwa na Makatibu Sheria kutoka Mikoa na Wilaya mbalimbali  walioshiriki katika kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu sheria kilichoanza leo tarehe 17 Disemba, 2021 hadi tarehe 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.








Share:

KAIMU NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA AISHUKURU UNICEF

 Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda amelishukuru Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF) kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kufadhili  Mafunzo na maelekezo ya utekelezaji wa ukaguzi  wa vizuizi vya watoto wanaokinzana na sheria wakishirikiana na timu ya maandalizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo  yamefanyika leo tarehe 15 Novemba, 2021  katika Ukumbi wa Rafiki Hotel Jijini Dodoma.



"Elimu mnayopata hapa mkawape na wenzenu, msikae kimya kwani haitaleta tija katika utendaji wa kazi zetu. Na pia mkifika mkawe waalimu wa Mawakili wenzenu mliowaacha ili kesi za watoto ziweze kuendeshwa kwa ufanisi mkubwa na weledi."

Alizungumza hayo Bi. Neema Mwanda wakati akitoa neno la kufunga mafunzo hayo.


Nae pia Mratibu wa Ulinzi na Usalama wa Mtoto kutoka Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF) Bi. Victoria Mgonela ametoa shukrani kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kueleza jinsi wanavyoshirikiana kikamilifu na ofisi hiyo katika kushughulikia mashauri ya watoto.

 


Share:

DPP AMEWATAKA MAWAKILI KUZINGATIA HAKI ZA WATOTO


 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu awataka Mawakili wa Serikali kufanya kazi zao kwa umakini, kupitia majalada yote kwa umakini ili kuweza kulinda haki za watoto.


Mkurugenzi wa Mashtaka akizungumza hayo wakati akifungua Mafunzo na maelekezo ya utekelezaji wa ukaguzi  wa vizuizi vya watoto wanaokinzana na sheria ambayo yamedhaminiwa na Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF) yanayofanyika leo tarehe 15 Novemba, 2021  katika Ukumbi wa Rafiki Hotel Jijini Dodoma. 


Mkurugenzi Mwakitalu alieleza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inayo jukumu la kusimamia haki jinai kwa maana ya kuendesha kesi za jinai, lakini katika Uendeshaji wa Mashtaka hayo, ofisi ina jukumu pia la kuratibu Upelelezi, na pia kufanya ukaguzi kwenye mahabusu, magereza na mahala pengine ambapo washtakiwa wa uhalifu wanatunzwa.


Mwakitalu aliendelea kueleza kuwa mafunzo hayo pia yataongeza tija kwenye utendaji wa kazi, na pia lile kundi la Watoto wanaokinzana na sheria au wale ambao ni waanga ni kundi muhimu  sana katika utendaji wa kazi za ofisi hii.


Aidha alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwasababu yatasaidia kuhakikisha kuwa haki za watoto za zinalindwa, na pia kupata uelewa utakaowezesha kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua stahiki katika haki za watoto.


Nae pia Kaimu Mkurugenzi Divisheni ya Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi Bw. Tumaini Kweka alieleza kuwa mafunzo hayo ni ya kwanza katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo yamewakutanisha kushughulikia mashauri katika ofisi za mikoa na wilaya. Na lengo la mafunzo hayo ni kuboresha na kuweka namna bora ya jinsi ya kuendesha mashauri hayo Mahakamani na vilevile kuona namna bora ya kushughulika na kesi zinazowahusu watoto ambao wamekinzana na sheria.

"Dhima au lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uelewa wa pamoja juu ya utaratibu mzuri wa kukagua magereza, kukagua mahabusu za polisi na mahabusu za watoto ambao wamekinzana na sheria wanakuwa wamehifadhiwa." Akizungumza hayo Mkurugenzi Kweka.

Share:

DPP MWAKITALU AZINDUA MWONGOZO JUU YA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWENYE MASUALA YA JINAI

 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amewaasa wananchi kuachana na vitendo vya kiuhalifu kwani uhalifu haulipi


Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amesema uwepo wa uhalifu uliokuwa ukizihangaisha baadhi ya nchi sasa limekuwa ni suala la kidunia kwakuwa  uhalifu huo umekuwa ukizuia maendeleo ya jamii zetu.


Akizindua Mwongozo ya  Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Masuala ya Jinai katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Bw. Mwakitalu alisema utoaji wa haki ikiwemo kuzuia vitendo vya uhalifu, ulinzi na Usalama wa raia ni msingi wa maendeleo ya jamii yoyote.



Mkurugenzi Mwakitalu alitaka uwepo wa ushirikiano wa nchi mbalimbali katika kupambana na uhalifu kwani juhudi za kupambana na uhalifu haziwezi kuishia katika nchi moja tu kwakuwa uhalifu wa kupangwa ni uhalifu unaovuka mipaka.


Mwakitalu aliendelea kueleza kuwa Tanzania imeridhia  Mikataba mbalimbali ya Kimataifa  ya kupambana na uhalifu wa kupangwa na unaovuka mipaka ikiwemo mikataba juu ya Ushirikiano wa Kimataifa ya kupambana na uhalifu.




 Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.  David Concar alisema uzinduzi wa Mwongozo juu ya Ushirikiano wa Kimataifa juu ya kukabiliana na Jinai  sio jambo dogo kwakuwa mamilioni ya watu duniani wanaathiriwa na  kukua kwa Masuala ya uhalifu, kuongezeka kwa Masuala ya kigaidi na rushwa.



Balozi Concar alisema uzinduzi wa Mwongozo juu ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Masuala ya Jinai ni matokeo ya Ushirikiano katika ya ubalozi wa Uingereza na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kufanikisha juhudi mbalimbali za kupambana na uhalifu.


 Naye Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Manfred Kanti aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua iliyofikia kama chombo muhimu cha kupambana na uhalifu wa Kimataifa na ule unaovuka mipaka



Share:

WAKUU WA MASHTAKA WA NCHI ZA AFRIKA NA NCHI ZA KIARABU WAKUTANA MISRI KWA MARA YA KWANZA..

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Mashtaka barani Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka wa Tanzania Ndugu Sylvester Mwakitalu  akihudhuria Mkutano wa Kamati ya Uongozi wa Umoja wa Wakuu wa Mashtaka barani Afrika unaofanyika  katika jiji la Cairo nchini Misri.

Mkutano huu unafanyika sambamba na Wakuu wa Mashtaka wa nchi za Kiarabu na unahudhuriwa na jumla ya washiriki 120 kutoka nchi za Afrika na za Kiarabu
 Ni kwa mara ya kwanza Wakuu wa Mashtaka wa Afrika na  Nchi za  Kiarabu wanafanya Kongamano pamoja kabla ya kila Umoja kufanya Mkutano wake .

Share:

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini aishukuru PAMS Foundation

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu ametoa shukrani zake kwa Shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kudhamini mafunzo ya Upelelezi na uendeshaji wa kesi za wanyamapori na misitu kwani mafunzo hayo waliyoyapata washiriki hao yatawasaidia kuwaongezea ujuzi na uzoefu katika kazi zao. 

Mafunzo hayo yameshirikisha wadau kutoka Taasisi mbalimbali wakiwemo Mawakili wa Serikali, Waendesha Mashtaka, Wapelelezi na Maafisa wa Wanyamapori


Bw. Mwakitalu alieleza kuwa ana imani kwa washiriki wote wa mafunzo hayo kuwa hawataenda kumuangusha bali watafanya kazi kwa matokeo chanya na kwa uadilifu wa hali ya juu kwani mafunzo hayo yatakuwa yamewajengea uwezo wa kupeleleza na kuendesha Mashtaka ipasavyo.


Mkurugenzi wa Mashtaka aliwahakikishia washiriki mawazo yao waliyoyatoa yatafanyiwa kazi na kwa yale ambayo yanahitaji marejeo ya kisheria wadau husika watashirikishwa.

Na pia Bw. Sylvester aliwashukuru Majaji wote, pamoja na watoa mada wengine  waliotenga muda wao na kukubali kushiriki kwenye utoaji wa mada mbalimbali katika mafunzo hayo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Makosa dhidi ya Mazingira na Maliasili kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Rosemary Shio alimshukuru Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kukubali kushiriki kufunga mafunzo hayo, na pia alishukuru uongozi wa PAMS Foundation kwa kudhamini mafunzo hayo.

Aliendelea kueleza kuwa siku tano za mafunzo ya Upelelezi na uendeshaji wa kesi za wanyamapori na misitu yamewajengea uwezo maofisa hao katika maeneo mbalimbali ikiwepo hati za Mashtaka,  mawasilisho yanayohusiana na hoja za wanyamapori na misitu.

Share:

UFUNGUZI WA MAFUNZO YA UPELELEZI NA UENDESHAJI WA KESI ZA WANYAMAPORI NA MISITU


Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi ameitaka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuhakikisha upelelezi wa makosa ya Jinai kuhusiana na misitu na wanyamapori unaratibiwa vizuri, watuhumiwa wanafikishwa mahakamani na Mashtaka yanaendeshwa kwa ufanisi mkubwa kwa lengo la kutokomeza ujangiri, kulinda rasilimali zetu na kuikuza sekta ya utalii na uhifadhi nchini. "Ninafurahi kuona mafunzo haya ninayofungua leo yamejumuisha wadau wote muhimu katika mfumo wa upelelezi na Uendeshaji wa makosa ya Jinai yahusuyo misitu na wanyamapori. Hivyo, sina shaka kwamba, mafunzo haya yatakuwa chachu ya mabadiliko na mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya ujangiri na ulinzi wa maliasili zetu." Akizungumza hayo Profesa Kabudi wakati akifungua mafunzo ya upelelezi na Uendeshaji wa Kesi za wanyamapori na misitu yanayofanyika Mkoani Morogoro katika Ukumbi wa Nashera Hotel.

baadhi ya washiriki 


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ameeleza kwamba kumekuwa na ongezeko la makosa ya wanyapori na mazao ya misitu nchini hivyo mafunzo haya kwao yana tija katika kulinda maslahi ya Taifa. Akifafanua ukubwa wa tatizo hilo, Bw. Mwakitalu amesema kuwa katika kikao cha Mahakama ya Rufaa kilichoanza leo tarehe 18 Oktoba, 2021 Musoma mkoani Mara, imebainika kuwa kuna kesi 18, ambapo kesi 14 kati ya hizo ni za wanyamapori na misitu. 



Naye Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Makosa ya Mazingira na Maliasili wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,
 Rosemary Shio alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na kuwapatia ujuzi utakao wawezesha kupeleleza na kuendesha kesi za wanyamapori na misitu kwa weledi na uadilifu







 

Share:

KAMISHNA WA KAZI ATOA RAI KWA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

 


Kamishna wa Kazi Brigedia Jenerali Francis Mbindi amelitaka Baraza la Wafanyakazi litumike kuimarisha Taasisi katika kazi zake kwa kufuata matakwa ya kisheria na katiba kwa kuwa ni chachu ya kuimarisha mahusiano mema mahali pa kazi.

Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka uliofanyika leo tarehe 24 Septemba, 2021 katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.

Kamishna huyo ametoa rai kwa Menejimenti pamoja na uongozi wa TUGHE kuzingatia Kalenda za vikao vya Baraza la Wafanyakazi ya kwamba kufanya vikao kwa mujibu wa sheria.

Brigedia Jenerali aliendelea kueleza kuwa Taasisi za umma ambazo bado hazijaunda Mabaraza ya Wafanyakazi, kuunda maramoja na pia kufanya vikao kwa mujibu wa sheria iliyounda mabaraza hayo kwani kufanya hivyo ni kujenga na kudumisha utawala bora katika utumishi wa umma.




Nae pia Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu ameeleza kuwa Baraza la Wafanyakazi ni chombo muhimu katika Taasisi za Utumishi wa Umma kwa maana ni chombo ambacho kinashauri Menejimenti kwenye masuala mbalimbali ambayo yanaweza kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Ofisi na pia kuishauri Menejimenti kuhusu haki,  wajibu, maslahi na mazingira bora ya watumishi pamoja na kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sheria, bajeti, miongozo na Sera za Ofisi ili ziweze kufanya kazi ni lazima zipitishwe na baraza.

''Hivyo basi kuzinduliwa kwa baraza hili kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni hatua kubwa na ni muhimu sana kwetu"
Amezungumza hayo Bw. Mwakitalu.




Aidha Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Juma Katanga ambaye pia Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ameahidi kudumisha ushirikiano na Wafanyakazi wote katika kutekeleza  majukumu yake ya Uratibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Share:

UFUNGUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA



 

Share:

PROFESA KABUDI AITAKA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA(NPS) KUONGEZA KASI YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA.

 Waziri wa Katiba na Sheria (Kushoto) Mh.Profesa Palamagamba Kabudi akifungua jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara lililoko katika Mji Mdogo wa Mugumu

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Profesa Palamagamba Kabudi amesema umefika,wakati sasa wa  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuongeza kasi ya kusimamia makosa ya uharibifu wa mazingira kwa ukubwa wake badala ya kazi hizo kufanywa na Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira ( NEMC) pekee kwakuwa uharibifu wa mazingira ni kosa ni uhujumu uchumi.

Mazingira yetu yanazidi kuharibiwa sana, kuharibu mazingira ni kosa la jinai. Tunakata miti bila huruma. Umefika wakati sasa jukumu la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kusimamia na kutunza mazingira lionekane wazi ili watu wajue kuwa kuharibu mazingira ni kosa la jinai na ni uhujumu uchumi.

Mhe. Kabudi ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Serengeti zilizofanyika mjini Mugumu leo tarehe 21 Septemba, 2021 ambapo alisema sasa kuna umuhimu wa kuipitia  Sheria kuu “Penal Code” ili kuhakikisha baadhi ya makosa yanayohusiana na uharibifu wa mazingira na maliasili yanaingizwa.

Alisema uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Serengeti litasaidia kusogezwa kwa karibu kwa  huduma za mashtaka kwa wananchi pamoja na kuipunguzia serikali gharama za uendeshaji kesi na pia itasaidia kupambana na ujangili katika wilaya ya Serengeti.

Mhe. Kabudi  alisema uhifadhi wa  maliasili za nchi yetu unahitaji ukali wa sheria ili kudhibiti vitendo viovu na kutaka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuyachukulia kwa uzito makosa hayo kwa kuwa yanahujumu uchumi ambapo alitaka maeneo yote yenye maliasili kuwa na Mawakili wa Serikali ili kupambana na makosa ya uharibifu wa mazingira.

Aidha, Mhe. Kabudi alitumia fursa hiyo kuipongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua ya kupata ofisi na wadau wote waliohisani na kuhakikisha kuwa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka linajengwa.

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka Ndg. Slyvester Mwakitalu alisema uwepo wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilayani Serengeti utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuongeza kasi ya utendaji kwakuwa mazingira ya utendaji kazi utakuwa umeboreshwa.

Alisema ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Serengeti ni jambo la kujivunia kwakuwa ni jengo la kwanza kujengwa tangu kuanzishwa kwa Ofisi yaTaifa ya Mashtaka mnamo mwezi Februari 2018. Aidha. Aliwashuru wadau wa Makampuni ya GRUMET kwa kufadhili ujenzi wa jengo hilo na kuwaomba wadau wengine pia kujitokeza kufanya hivyo wanapoombwa kuhisani ujenzi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Vincent Mashinji akizungumza katika hafla hiyo alisema uwepo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Serengeti utasaidia kuboresha huduma na utaipunguzia serikali gharama za uendeshaji wa kesi na upelelezi ambapo aliahidi kuongeza ushirikiano katika utendaji wa kazi.

Aidha, Mhe. Mashinji aliwataka wakazi wa Serengeti kutii sheria bila shuruti na kuitumia ofisi hiyo kwa kutoa ushirikiano mzuri pale wanapohitajika kutoa ushahidi hali ambayo itapelekea kesi kuisha kwa wakati.Mwonekano wa  mbele wa  Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya  ya  Serengeti Mjini Mugumu Mkoani Mara 

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba  Kabudi akikata utepe  kuashiria Ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mugumu-Serengeti Mkoani Mara.

Baadhi ya Viongozi wakeindelea kufautailia Burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendele wakati wa Ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani Serengeti Mkoani Mara.

Baadhi ya wakazi wa Serengeti wakiedelea kufuatilia hotuba za Viongozi 

Viongozi mbalimbali wakiendelea kufautilia na kutazama burudani wakati wa ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashataka Seregenti Mara

Viongozi mbalimbali wakiendelea kufautilia na kutazama burudani wakati wa ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashataka Seregenti Mara


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba  Kabudi akitoa zawadi wa wacheza ngoma  wakati wa ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti.

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba  Kabudi akitoa tuzo ya  zawadi  kwa Mkurugenzi Mkuu wa Grumet Fund Bw. Noel Mbise ikiwa ni sehemu ya kkutambua mchango wao kwenye ujenzi wa jengo hilo wakati wa ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti. 


 

Share:

MKUTANO WA SEKRETARIETI YA JUKWAA LA HAKI JINAI TAIFA

 


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa kesi na Uratibu wa Upelelezi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Neema Mwanda akifungua Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa, ambae pia ni Mwenyekiti wa mkutano huo ulioanza leo tarehe 2 Agosti, 2021 na kumalizika tarehe 3 Agosti, 2021 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.



Kaimu Mkurugenzi msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Peter Maugo akitoa muongozo wa ratiba ya mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa unaofanyika leo tarehe 2 hadi 3 Agosti, 2021 katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha St. John Dkt. Alfred Sebahene akiwasilisha mada juu ya uandishi wa taarifa katika Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa ulioanza leo tarehe 2 Agosti, 2021 na kumalizika tarehe 3 Agosti, 2021 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.


Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha St. John Dkt. Alfred Sebahene akiwasilisha mada juu ya uandishi wa taarifa katika Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa ulioanza leo tarehe 2 Agosti, 2021 na kumalizika tarehe 3 Agosti, 2021 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.


Wajumbe walioshiriki kwenye Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa wakifuatilia kwa umakini mada inayowasilishwa na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha St. John Dkt. Alfred Sebahene (Hayupo pichani) katika Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa ulioanza leo tarehe 2 Agosti, 2021 na kumalizika tarehe 3 Agosti, 2021 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.



Mkurugenzi wa Divisheni ya Urejeshaji wa Mali zinazohusiana na uhalifu, uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Paul Kadushi akiwasilisha mada juu ya uhalifu wa kimtandao katika Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa ulioanza leo tarehe 2 Agosti, 2021 na kumalizika tarehe 3 Agosti, 2021 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa Bi. Neema Mwanda ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa Upelelezi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa walioshiriki kwenye Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa ulioanza leo tarehe 2 Agosti, 2021 na kumalizika tarehe 3 Agosti, 2021 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa Bi. Neema Mwanda ambae pia Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa kesi na Uratibu wa Upelelezi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa ulioanza leo tarehe 2 Agosti, 2021 na kumalizika tarehe 3 Agosti, 2021 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.



Picha ya pamoja inayojumuisha Wajumbe wote walioshiriki kwenye Mkutano wa Sekretarieti ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa ulioanza leo tarehe 2 Agosti, 2021 na kumalizika tarehe 3 Agosti, 2021 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.





Share:

Labels

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .