OFISI YA MASHTAKA
  • Home
  • UONGOZI
  • HISTORIA
  • JARIDA
  • VIDEO
  • MAONI USHAURI
  • MAWASILIANO
  • Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

    Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.

  • UKATAJI WA UTEPE

    UKATAJI

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini

AYUBU KIBOKO NA MKEWE PILLY KIBOKO WAHUKUMIWA JELA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKADecember 19, 2020DAR ES SALAAM No comments

 

Pichani ni Ayubu Mfaume  Kiboko akiwa pamoja na Mke wake Pilly Mohamed Kiboko baada ya kuhukumiwa  kutumikia kifungo cha Miaka 20 Jela. 
NA MARRYGORETH NTANDU ...

Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi Kanda ya Dar es salaam  imemtia hatiani mshtakiwa Ayubu Mfaume Kiboko pamoja na mke wake Pilly Mohamed Kiboko na kuhukumiwa kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya.

Kesi hiyo Na.13/2019,   imetolewa  hukumu  Desemba 18, 2020   mbele ya Mhe. Jaji Lilian Mashaka ambapo Imeelezwa  Mahakamani hapo kuwa mnamo tarehe 23 Mei, 2018 mshtakiwa huyo pamoja na mke wake walikamatwa na Maafisa wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya mara baada ya kufanya upekuzi wa nyumba yao iliyopo eneo la Tegeta Nyuki Jijini Dar es salaam.

Katika  upekuzi huo walifanikiwa kupata Madawa  ya kulevya aina ya Heroid Hydrochloride yenye ujazo wa Gram 251.25
Baada ya kupatikana kwa madawa hayo washtakiwa hao walishtakiwa kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya chini ya kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Katika kuthibitisha shtaka hilo upande wa Jamhuri uliwaita mashahidi 6 na kutoa vielelezo 16 ambapo upande wa utetezi washtakiwa walijitetea wenyewe na kutoa vielelezo viwili.
Baada ya kupitia ushahidi huo kwa ujumla wake, mahakama imejiridhisha kwamba Jamhuri imethibitisha shtaka bila kuacha shaka, hivyo  kuwatia hatiani washtakiwa  wote wawili.

Kesi hiyo imeendeshwa na Mawakili wa Serikali Faraja Nchimbi, Salim Msemo, Costantine Kakula, Candid Nasua pamoja na Tully Helela.

Share:
Read More

MKURUGENZI WA MASHTAKA (DPP) BISWALO MGANGA AFAFANUA KUHUSU UPATU

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKADecember 18, 2020DAR ES SALAAM No comments

Pichani ni Mkurugezi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga. 

DAR ES SALAAM 

  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ni kosa kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na kampuni ya Qnet kisha kudai wametapeliwa kwamba kufanya hivyo ni kosa.

Ameeleza hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ikiwa ni siku mbili baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita kurejesha Sh5.48 milioni kwa mwalimu Rose Mgomba wa Shule ya Msingi Lukaranga aliyedai kutapeliwa.

Wasiwasi watanda kampuni ya Qnet

Katika maelezo yake, Mganga alisema urejeshwaji wa fedha hizo ni kosa kisheria kwa sababu biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni upatu haramu.

Mbali na kukemea suala hilo, alizitaka taasisi zinazofanya uchunguzi kuhusiana na sakata la kampuni ya Qnet kushirikiana kwani wanajenga nyumba moja.

Alisema shughuli inayoendeshwa na kampuni ya Qnet ni upatu na tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ameanza upelelezi kuhusiana na sakata hilo.

Share:
Read More

MR KUKU AHUKUMIWA KULIPA FIDIA YA ZAIDI YA BILIONI 5.4, FAINI YA MILIONI 5 AU KWENDA JELA MIAKA 5

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKADecember 16, 2020DAR ES SALAAM No comments
Picha ni Mkurugenzi wa Kampuni ya  Mr.Kuku Farmer Ltd Bw Tariq  Machibya Marufu kama Mr Kuku aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kufanya biashara haramu ya Upatu.

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Mr. Kuku Farmer Ltd,  Tariq Machibya (29), maarufu kama Mr Kuku, aliyekuwa akikabiliwa  na kesi ya kufanya biashara haramu ya upatu  na kukusanya fedha za umma kiasi cha Shilingi  Bilioni 17, amehukumiwa kulipa fidia ya zaidi ya  Shilingi  Bilioni 5.4 baada ya kukiri Mashtaka ya kushiriki katika upatu na kupokea miamala ya fedha kutoka kwa umma.

Mahakama pia imemuhukumu mshtakiwa  kulipa faini ya shilingi  Milioni tano ama akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitano Gerezani.

Aidha Mahakama imeamuru fedha kiasi cha Shilingi Bilioni  5 na milioni 456 na laki 480.41 (5,456,480.41) ambazo zipo katika akaunti za mshtakiwa zitaifishwe na kuwa mali ya serikali. 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  Godfrey Isaya   amesema mahakama imezingatia kwamba mshtakiwa amekiri mwenyewe makosa yake na ni mkosaji wa mara ya kwanza na wameangalia makubaliano hivyo hakuna sababu ya kumpa adhabu kali.

Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, wamedai mshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) wameingia makubaliano , katika mashtaka saba aliyokuwa anakabiliwa nayo yameondolewa na wamebakisha mashtaka mawili.

Akisomewa mashtaka hayo mawili, katika shtaka la kusimamia biashara ya upatu inadaiwa  kati ya Januari 2018 na Mei, mwaka huu, maeneo tofauti Jijini Dar ea Salaam alijihusisha na biashara hiyo kwa kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma kwa kujifanya  watafanya ujasiriamali wa ufugaji kuku na watapata faida asilimia 70 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji wa uwekezaji wa miezi sita kiasi ambacho ni kikubwa kibiashara kuliko mtaji uliokusanywa.

katika shtaka la pili mshtakiwa anadaiwa kukubali kupokea muamala wa kifedha kutoka kwa umma kiasi cha Sh bilioni 17.

Awali mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka saba ambapo mbali na hayo mawili  yalikuwepo mashtaka matano ya utakatishaji  fedha.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu, Wakili Kadushi aliieleza mahakama kuwa, hawana kumbukumbu za makosa ya nyuma ya washitakiwa hivyo, ameiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria huku ikizingatia hatua ya makubaliano waliyofikia.

Upande wa wakili wa Utetezi, Augustine Shio ameiomba mahakama impunguzie mshtakiwa wake adhabu  kwani amekiri makosa yake mwenyewe na pia ana familia ya wake watatu ambao kila mmoja ana mtoto mchanga na wote wanamtegemea yeye.

Share:
Read More

BABA NA MWANA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA MKOANI KIGOMA KWA KUUA MAKUSUDI

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKADecember 14, 2020KIGOMA No comments

Mwonekano wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma likionekana kwa Mbele 

 Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Wilaya ya Kasulu katika kesi Na.32/2020 mbele ya Mhe. Jaji A. Matuma imewatia hatiani washtakiwa Enock Antony pamoja na baba yake  Antony Kinanila na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kwa makusudi Cosmas Pastory.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 26, Desemba 2018 katika Kijiji cha Katundu Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa walimuua marehemu kwa sababu ya mgogoro wa ardhi na kwamba marehemu alikuwa anajidai kuwa yeye ni tajiri. Washtakiwa walienda kwa marehemu usiku wakamkuta amekaa nje ya nyumba yake na familia yake ndipo wakamkamata, wakamlaza chini chali kisha wakamchoma mkuki kifuani mbele ya familia yake.

Kesi hiyo imeendeshwa na Mawakili wa Serikali Robert Magige na Edna Makala.

Share:
Read More

ASKARI WAWILI, WAFANYABIASHARA WATATU WASHTAKIWA KWA KUTOROSHA MADINI YA DHAHABU MBEYA

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKADecember 10, 2020 No comments

 

Mkurugenzi wa Mashtaka , Biswalo Mganga.




Share:
Read More

MAHABUSU 72 WAFUTIWA MASHTAKA

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKADecember 02, 2020 No comments


 

Jumla ya Mahabusu Sabini na mbili kati yao wanaume 62 na wanawake 10 wamefutiwa Mashtaka na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga baada ya kutembelea gereza la Karanga, Moshi kujionea hali halisi ya gereza pamoja na kuwasikiliza mahabusu

Mkurugenzi wa Mashtaka amefanya tukio hilo leo baada ya kukagua na kujionea hali halisi ya gereza hilo ambapo alipata pia nafasi ya kuwasilikiliza wafungwa na Mahabusu.

Akizungumza baada ya kuwafutia Mashtaka Mahabusu hao Bwana Mganga aliwataka watakaporudi uraiani kuwa raia wema na wale wanaobaki gerezani kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu ili awasamehe dhambi walizotenda na kufungua mlango wa rehema.

Aidha aliwaonya kutorudia kufanya Uhalifu. "Sitegemei kuwakuta mmefanya Uhalifu tena baada ya kutoka hapa, ole wenu mrudie. Kama kuna miongoni mwenu ambaye anajua hawezi kuacha Uhalifu aombe abaki humu ndani" Alisisitiza Bw. Mganga

Mkurugenzi wa Mashtaka alitumia nafasi hiyo kuwaonya watu wanaotishia mashahidi na wanaotaka kupata haki kwa njia ya Udanganyifu kwakuwa akikamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Mashtaka aliahidi kuchukua changamoto zilizotolewa na Mahabusu na wafungwa na kuahidi kuzifanyia kazi.

Mkurugenzi wa Mashtaka na timu ya viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wapo katika Mikoa mbalimbali kukagua namna shughuli za uendeshaji wa shughuli za Mashtaka unavyotekelezwa ikiwapo kutembelea Magereza, mahabusu na kuwatembelea wadau muhimu wanaoshirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Haki Jinai.

Share:
Read More

WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA THELATHINI JELA

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKADecember 01, 2020 No comments




 Mahakama ya Wilaya ya Iringa katika Kesi Na. 139/2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Iringa imewatia hatiani washtakiwa watatu Richard Mbundamila, Taford Kalinga na Haruni Boniface Mgawo  na kuwahukumu kifungo cha miaka thelathini (30) jela kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha, kutoroka chini ya Ulinzi na Kujeruhi.

Watuhumiwa hao wamehukumiwa kifungo cha miaka thelathini (30) jela kwa kosa la kwanza ambalo ni unyang'anyi wa kutumia silaha na miaka Saba kwa kila kosa kwa makosa ya Kujeruhi na kutoroka chini ya Ulinzi.

Katika kosa hilo upande wa Mashtaka uliwasilisha vidhibiti kadhaa vikiwemo bunduki aina ya Uzi gun, mashoka Saba, Mapanga matano, risasi mbili, maganda mawili ya risasi pamoja nasare za wafungwa tatu.

Ilielezwa Mahakamani hapo kuwa watuhumiwa wa
likuwa wafungwa waliokuwa wakitumikia vifungo mbalimbali ambapo siku ya tukio walienda kutafuta kuni na wakiwa huko walimvamia askari aliyekuwa anawalinda na kumkata panga kichwani kisha kumnyang'anya bunduki na kuondoka nayo.

Katika tukio hilo mtuhumiwa mmoja aliuawa katika mapambano akiwa huko Njombe ambapo silaha iliyoibiwa ilikombolewa 

Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Edna Mwangulumba na Brandina Manyanda

Share:
Read More

WASHITAKIWA 16 WA UJANGILI WAFUNGWA MIAKA 20 HADI 30 KWA KUKUTWA HIFADHINI NA NYARA ZA SERIKALI

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 29, 2020MARA No comments

 

Washitakiwa 16 katika kesi Namba  8 wametiwa hatiani kwa makosa ya ujangili na kuhukumiwa jumla ya kifungo kati ya miaka 20 hadi 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti.

Washitakiwa hao walikamatwa mwaka 2019 kwa nyakati tofauti ndani ya  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mapori ya Akiba ya Ikorongo, Grumeti na Hifadhi ya Jamii ya Ikona na kushitakiwa kwa makosa matatu ikiwemo  kuingia,kupatikana na silaha za jadi  na kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao kwa nyakati na sehemu mbalimbali walikamatwa na nyara tofauti ikiwemo vipande vya nyama za Pundamilia, Impala, Nyumbu na Kongoni zenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni 29 na laki 9 na Elfu 55 (29,955,000).

 Akisoma hukumu hiyo  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Serengeti  Ismael Ngaile amesema kuwa  kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ambayo inatoa adhabu ya isiyozidi miaka 30 na isiyopungua miaka 20 .

Washitakiwa hao ni  Makena Mwita (21) Mkazi wa Mbirikiri ,  Rubeni Mwita (28) wa Bonchugu ambao kila mmoja amehukumiwa miaka 30 jela huku  Mugendi Ng’ombe (51) mkazi wa Nyichoka,Richard Nyambaya(35)na Mussa Masese(42)wakazi wa kijiji cha Nyamatoke walihukumiwa kila mmoja miaka 25 

Aidha  Manungu Makoye na Mazoya Daddi ambao wamehukumiwa miaka 20, na wenzao  Simion Nyamhanga(28)mkazi wa Nyamakendo,Benard Gambachera(50)mkazi wa Robanda, Marwa Chacha (30) Marwa Mtatiro(19)Mnanka Bisare(28)Sarya Matiko(20) Maduhu Mila(35)mkazi wa kijiji cha Singisi,Bhoke Mwita(53)na Juma Masyora(43)wakazi wa Bisasara.

Mapema waendesha Mashitaka wa serikali Josephat Emmanuel, Abeid Nnko na Jakobo Matatala mbele ya Hakimu Ngaile waliomba Mahakama kutoa adhabu kali katika kesi hizo za Uhujumu uchumi kwa kuwa vitendo vya ujangili vinazidi kushamiri na kuathiri maliasili za Nchi, huku baadhi ya washitakiwa wakishindwa kujitetea.

Share:
Read More

DPP ATOA MAELEKEZO KWA TAKUKURU NA DCI KUKAMILISHA UCHUNGUZI JUU YA UHABA WA SARUJI NA VIFAA VYA UJENZI NCHINI NDANI YA SIKU 30

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 20, 2020 No comments

                             
                                                       
Share:
Read More

DPP AWAONYA WAUZAJI WANAOFICHA VIFAA VYA UJENZI

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 18, 2020 No comments

 .        Mkurugenzi  wa Mashtaka Nchini Bw.Biswalo Mganga akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi nchini kuacha kuficha Vifaa hivyo.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Biswalo Mganga amewaonya wauzaji wa vifaa vya Ujenzi kufuatia baadhi yao  kuficha Sementi na Mabati kwa lengo la  kuongeza bei  ili kujipatia faida kubwa zaidi, na  kusema kuwa kufanya hivyo  ni  kosa la Jinai

Bw. Mganga ameeleza kuwa watu  wote wanaofanya hivyo wanafanya kosa la uhujumu uchumi ambalo limeanishwa katika Sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 jela   pamoja na  kutaifishwa  mali kwa yeyote atakayekamatwa kwa kutenda kosa hilo.

Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo Jijini Dodoma leo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika yaliyokuwa na lengo la kufahamu mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya  Mashtaka tangu kuanzishwa kwake ambapo ameeleza kuwa imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake.

Aidha, amesema kuwa jukumu la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni kuhakikisha kuwa Haki, Amani na Usalama vinapatikana nchini kwa Maendeleo ya Taifa.                                                                                      Mwonekano wa nembo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma
                                           Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Biswalo Mganga akusoma Dira ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
       Mwonekano wa mbele wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) lililoko Jijini Dodoma

Share:
Read More

MKURUGENZI WA MASHTAKA AZINDUA TOVUTI YA CHAMA CHA WAENDESHA MASHTAKA AFRIKA MASHARIKI

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 17, 2020 No comments

 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo  Mganga amezinduzi Tovuti ya  Chama cha Waendesha  Mashtaka Afrika Mashariki akishirikiana na viongozi wengine kutoka katika  nchi wanachama.

uzinduzi huo umefanyika Novemba 16, 2020 kwa njia ya Mtandao ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini biswalo mganga  ameedesha zoezi hilo akiwa jijini Dodoma huku   Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Kenya  ambaye pia ni Katibu wa chama hicho Bw. Noordin Mohamed Haji  akiwa jijini Nairobi.

 katika uzinduzi huo viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo  Bi. Heather Schildge ambaye  ni    Naibu  Mkurugenzi wa  Misioni kutoka Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani-USAID, Bi. Julie Thomson ambaye ni Mkurugenzi wa Trafiki  Progamu ya Afrika, Wawakilishi Kutoka katika Mashirika ya Kimataifa na Kikanda pamoja na Waendesha Mashtaka kutoka  baadhi ya nchi wanachama wa Umoja huo.

Akieleza umuhimu wa  Tovuti hiyo Bw. Biswalo alisema uzinduzi huo ni miongoni mwa hatua muhimu iliyofikiwa katika  kuimairisha mapambano dhidi ya uhalifu wa wanyamapori  katika nchi za Afrika Mashariki.

Chama Cha Waendesha Mashtaka wa Afrika Mashariki kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na jumla ya wananchama kutoka nchi tano ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na Kenya ambapo hadi  kufika hivi sasa chama hicho kimefanikiwa kuongeza wanachama kutoka nchi nyingine jirani zikiwemo Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Sudan, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Zambia, Malawi na Msumbuji.

Wakati wa Uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mashtaka aliendelea kueleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2014 katika nchi ya Tanzania idadi nyingi ya Tembo ilishuka hadi kufikia asilimia 60 kutokana na ujangili na biashara haramu ya wanyamapori ukilinganisha na matukio ya nchi nyingine za jirani.

''Tovuti hii ni chombo muhimu kwa ajili ya kuhakikisha masuala yote ya taarifa dhidi ya uhalifu wa Wanyama katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa yanarahisishwa ili kupambana na wale wote wanaojihusisha na biashara haramu za Wanyamapori   pamoja na kuimarisha mifumo wa mawasiliano katika nchi wanachama''.

''Ni matumaini yangu kuwa website hii kupitia umoja wa waendesha mashtaka wa masuala ya wanyama na mazingira utaamsha katika matumizi ya sheria mbalimbali za kikanda za wanyama kupelekea kukua kwa uhifadhi wa wanyama na kuwa na kituo cha kutolea taarifa kuhusu makosa hayo''.

''Napenda kushukuru waendesha mashtaka wote kwa ushiriano waliotoa katika kutengeneza na kuanzisha tovuti na juhudi za makusudi za kujenga umoja huu''.amesema Bw Biswalo Mganga

Mwisho aliwashukuru wajumbe waliohudhuria katika kikao hicho wakiwemo Bw. Noordin Mohamed Hji, Bi. Heather Schildge, Bi. Julie Thomson, na wawakilishi mbalimbali kutoka Mataifa mbalimbali ya Kiserikali.

 

Share:
Read More

Wahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 17, 2020 No comments

 


Mahakama Kuu ya Rushwa na Uhujumu Uchumi  Dar es Salaam katika kesi ya Uhujumu Uchumi  namba 14/2018 mbele ya Mhe. Jaji Banzi imewatia hatiani washtakiwa Nabibarkhshsh Pribakhsh na Mohamaddhanif Nazirahmad Dorzade kwa kosa la kupatikana na Madawa ya Kulevya aina ya Heroin Hydrochloride kiasi cha Kilogramu 111.2 na Gramu 451.7 za Bangi na kuwahukumu kwenda jela kifungo cha miaka thelathini  pamoja na kutaifisha jahazi ambalo walitumia kutenda kosa hilo

Shauri hili limeendeshwa na Mawakili wa Serikali Monica Mbogo, Cecilia Shelly, Batilda Mushi  na Clara Charwe

Aidha, mahakama imewaachia huru watuhumiwa kumi na moja (11) katika kesi hiyo ambao majina yao ni
Abdullah Khatoon Sahib,
Ubeidulla Gulamzade Abdi, Naim Baltik Ishqa
Moslem Amiree Golmohamad,
Rashid Badfar, Omary Dorzade Ayoub, Tahir Bishkar Mubarak,
.Abdulmajid Asqan Pirmuhamad,
Ally Abdallah Ally,
Juma Amour Juma,
Omari Saidi Mtangi. 
Mbele ya Mh Jaji Banzi. Mahakama imemtia hatiani Nabibarkhsh Pribakhsh na Mohamaddhanif Nazirahmad Dorzade ambao walikuwa ni miongoni mwa washtakiwa katika shauri hilo. Hata hivyo upande wa Mashtaka haujaridhishwa na Maamuzi ya Mahakama ya kuwaachia huru  Washtakiwa hao na umekata rufaa kupinga hukumu hiyo.





Share:
Read More

Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mkewe

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 17, 2020 No comments

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi ya Jinai Na.137/2018 mbele ya Mhe. Jaji J.C Tiganga imemtia hatiani mshtakiwa Mwita Mgaya Nyamtiba kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kukusudia kumuua mkewe Christina Mwita Mgaya.

Akiielezea Mahakama Wakili wa Serikali Bw. Nimrod Byamungu amesema kuwa, tukio hilo lilitokea mnamo tarehe5, Januari 2018 katika Kijiji cha Kitagasembe  Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara ambapo mshtakiwa alimuua marehemu kwasababu alikuwa anamzuia kuuza ardhi ya familiya kwa ajili ya kuoa wake wengine pamoja na kunywa pombe.
Marehemu aliuawa kwa kuchinjwa shingo na kukatwa usoni kwa kutumia panga.

 

Share:
Read More

Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto) Akiweka kumbukumbu ya Dawa za kulevya

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 13, 2020 No comments

Mahakama Kuu kwa kushirikiana na mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya nchini na ofisi ya mwendesha mashtakaa-DPP wameteketeza zaidi ya kilo 100 za dawa za kulevya ikiwemo heroini, cocaine na bangi ambazo kesi zake zimemalizika kwa kipindi cha miaka miwili na watuhumiwa kuhukumiwa.



Tukio la uteketezaji limefanyika Leo jijini Dar es Salaam katika kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill-TWIGA CEMENT ambapo zoezi zima lilifanyika kwa ulinzi wa jeshi la Polisi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari katika tukio hilo, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Jaji Edwin Kakolaki amesema baada ya kesi kumalizika mahakama hutoa kibali cha kuteketeza Vielelezo na zoezi hilo linaendeshwa kwa uwazi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali.



“Uendeshaji wa tukio hili kwa uwazi husaidia kuandoa dhana inayoenezwa mtaani kuwa dawa za kulevya hurudishwa tena mtaani baada ya kukamatwa”. Amesema Jaji Kakolaki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka nchini-DPP, Biswalo Mganga ameeleza vielelezo hivyo ni vya zaidi ya kesi 30 za dawa za kulevya za watuhumiwa wa ndani na nje ya nchi huku akieleza mbali na watuhumiwa kuhukumiwa pia baadhi ya mali zao zimetaifishwa na Serikali.



Naye kamishna wa sayansi na jinai kutoka mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya nchini Bi.Bertha Mamuya amebainisha kwamba uteketezaji wa dawa hizo hauna athari ndani ya jamii.



Share:
Read More

Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakola akishirikiana na Mkurugenzi wa Mashtaka B

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKANovember 13, 2020 No comments

Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakola akishirikiana na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga kuteketeza Madawa ya kulevya katika zoezi maalum walilolifanya Jijini Dar es Salaam
 

Share:
Read More

TUMEJIPANDA KUTOA HAKI KWA WANANCHI,BILA UONEVU WOWOTE.

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 23, 2020 No comments

 Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa upatikanaji wa haki baina yao bila uonevu wowote.

Akieleza hayo katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani humo, ikiwa ni lengo la kusogeza huduma karibu kwa wananchi walio wengi.

Aidha Bw. Mganga ameongeza kuwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi ni kuwa na utawala bora, kulinda haki na amani kwa kila Mtanzania na kupunguza malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi walio wengi na kuahidi kuwashughulikia wale wote ambao wanavuruga usalama wa nchi yetu.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amepongeza jitihada hizo za kuhakikisha Ofisi hiyo inafunguliwa Wilayani hapo ambapo amesema kufunguliwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imekuwa ni faraja kubwa kwa wananchi wa Taifa letu. Hivyo basi, anaamini wananchi wake watapata elimu ya kutosha juu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, inafanyaje kazi na kuhakikisha haki inatendeka baina ya wananchi. Na pia Mhe. Jamhuri aliwaasa wananchi wake kuitumia vizuri Ofisi hiyo na kuhakikisha kutoa ushirikiano ipasavyo.

Kwa upande wake mmoja wa waandishi waliohudhuria hafla hiyo ameishukuru Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kuwasogezea wananchi huduma hiyo kwa ukaribu zaidi na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wananchi kwani walikuwa wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.


Naye kwa upande wake,Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo alitoa wito kwa Wakuu wa Wilaya waendelea kujitolea Ofisi  kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa Mashtaka kwani Ofisi zilizopo ni chache. "Hadi sasa tumefanikiwa kufungua jumla ya Ofisi za Wilaya 15, ukizingatia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka zinapaswa kuenea jumla ya Wilaya 139".
Share:
Read More

UZINDUZI WA OFISI YA MASHTAKA WILAYA YA SERENGETI, MARA

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 23, 2020 No comments




 

Share:
Read More

MATUKIO YA PICHA YA UZINDUZI WA OFISI MPYA YA TAIFA YA MASHTAKA MUFINDI,IRINGA.

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 22, 2020 No comments
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw, Biswalo Mganga akiwa na Mh.Jamhuri Wiliam wakikata utepe,kuashiria uzinduzi wa ofisi ya taifa ya Mashtaka wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Wilaya hiyo.
     Picha ya pamoja ya Meza kuu katika uzinduzi wa  hafla ya uzinduzi wa ofisi ya 
                                             Taifa ya Mashtaka ufindi Mkoani Iringa.


Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw,Biswalo Mganga wakati akitoa neno katika hafla ya uzinduzi wa Ofisi hiyowilayni Mufindi Mkoa wa Iringa. 

Mkuu wa wilaya hiyoMh,Jamhuri William akitoa neno kwenye uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw,Biswalo Mganga wakiwa na naibu wake Bw,Edson Makallo kwenye uzinduzi wa ofisi hiyo ya mashtaka.

Kamati ya ulinzii na Usalama ,Wilaya ya mufindi Wakijadili Jambo na Naibu Mkurugenzi wa ofisi ya taifa ya Mashtaka Bw,Edson Makallo kwenye uzinduzi huo.Picha ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa serikali wa wilaya ya  Mafinga Mkoa wa Iringa, wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga,wa nne kutoka kushoto ,ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa ofisi mpya ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya  Mafinga Mkoani Iringa.

Share:
Read More

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 21, 2020 No comments


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma. Katika tukio hilo Mhe. Rais aliipongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia mali za Serikali na kuhakikisha hazipotei.
Share:
Read More

Ukataji wa utepe katika uzinduzi

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 21, 2020 No comments


 

Share:
Read More

Uzinduzi wa

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 21, 2020 No comments
Share:
Read More

SHERIA

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 21, 2020 No comments


 

Share:
Read More

Uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 21, 2020 No comments


ofisi_ya_taifa_ya_mashtaka_tz

Picha ya pamoja katika uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti, Mugumu, mkoani Mara. ( Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Bw. Nurudini Babu, wa nne ni Mkurugenzi wa Halmashauri, na nyuma yao wakiwa pamoja na wakurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka 

Share:
Read More

Uzinduzi wa ofisi yetu nyingine

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 21, 2020 No comments


 Mkurugenzi wa ofisi ya Taifa ya Mashtaka akikata utepe katika uzinduzi wa ofisi yetu nyingine, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Serengeti,Mugumu,Mkoani Mara.

Share:
Read More

Ofisi_ya_taifa_ya_mashtaka_tz

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 21, 2020 No comments



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo baada ya kupokea taarifa ya magari yaliyotaifishwa kutokana na Uhujumu Uchumi na kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma. Katika tukio hilo Mhe. Rais aliipongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia mali za Serikali na kuhakikisha hazipotei. 

Share:
Read More

Uzinduzi wa ofisi ya mashtaka wilaya ya kahama

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKAOctober 21, 2020 No comments

 

Tunawakaribisha wadau wetu wote pamoja na wananchi katika Ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani Kahama 03/09/2020

Share:
Read More
← Newer Posts Home

Social Profiles

TwitterFacebookGoogle PlusInstagramRSS FeedEmail
  • Popular
  • Tags
  • Blog Archives

Pages

  • Home
  • MAONI USHAURI
  • JARIDA
  • MAWASILIANO
  • VIDEO
  • MAAFISA TRA NA BENKI WALIOACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA KISUTU WATIWA HATIANI KWA KOSA LA UTAKATISHAJI FEDHA
     Mahakama ya Rufani imetoa hati ya kuwakamata na kuwaweka  rumande washtakiwa wanne, akiwamo aliyekuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanza...
  • UKATILI WA KIJINSIA UATHIRI AFYA NA UCHUMI WA TAIFA - NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA.
    Baadhi ya Wakuu wa Mashtaka kutoka Mikoa na Wilaya zote Tanzania bara wakiendelea kufuatilia hotuba ya ufungaji wa Mafunzo ya kuwajengea uwe...
  • WASHTAKIWA 57 WAFUTIWA MASHTAKA GEREZA LA KAYANGA-KARAGWE MKOANI KAGERA WATAKIWA KWENDA KUWA RAIA WEMA
    Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amon Mpanju ,Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga   ...

Labels

  • DAR ES SALAAM (8)
  • DODOMA (3)
  • KAGERA (2)
  • KIGOMA (1)
  • KITAIFA (2)
  • LINDI (1)
  • MARA (2)
  • MOROGORO (4)
  • mwanza (1)
  • njombe (1)
  • SERENGETI-MARA (1)
  • SINGIDA (2)

Blog Archive

  • ► 2025 (24)
    • ► October (3)
    • ► May (5)
    • ► March (11)
    • ► February (5)
  • ► 2024 (35)
    • ► December (6)
    • ► November (6)
    • ► October (4)
    • ► September (3)
    • ► August (1)
    • ► June (1)
    • ► May (3)
    • ► April (1)
    • ► March (7)
    • ► January (3)
  • ► 2023 (17)
    • ► November (1)
    • ► September (2)
    • ► August (2)
    • ► July (2)
    • ► May (3)
    • ► April (3)
    • ► March (2)
    • ► February (2)
  • ► 2022 (24)
    • ► December (1)
    • ► November (1)
    • ► October (1)
    • ► August (3)
    • ► July (2)
    • ► May (4)
    • ► March (4)
    • ► February (4)
    • ► January (4)
  • ► 2021 (36)
    • ► December (2)
    • ► November (5)
    • ► October (1)
    • ► September (3)
    • ► August (1)
    • ► July (1)
    • ► June (4)
    • ► May (4)
    • ► April (3)
    • ► March (2)
    • ► February (3)
    • ► January (7)
  • ▼ 2020 (26)
    • ▼ December (7)
      • AYUBU KIBOKO NA MKEWE PILLY KIBOKO WAHUKUMIWA JELA...
      • MKURUGENZI WA MASHTAKA (DPP) BISWALO MGANGA AFAFAN...
      • MR KUKU AHUKUMIWA KULIPA FIDIA YA ZAIDI YA BILIONI...
      • BABA NA MWANA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA MKOA...
      • ASKARI WAWILI, WAFANYABIASHARA WATATU WASHTAKIWA K...
      • MAHABUSU 72 WAFUTIWA MASHTAKA
      • WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA THELATHINI JELA
    • ► November (8)
      • WASHITAKIWA 16 WA UJANGILI WAFUNGWA MIAKA 20 HADI ...
      • DPP ATOA MAELEKEZO KWA TAKUKURU NA DCI KUKAMILISHA...
      • DPP AWAONYA WAUZAJI WANAOFICHA VIFAA VYA UJENZI
      • MKURUGENZI WA MASHTAKA AZINDUA TOVUTI YA CHAMA CH...
      • Wahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kukutwa na ma...
      • Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua m...
      • Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto)...
      • Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Edwin Kakola akishirikia...
    • ► October (11)
      • TUMEJIPANDA KUTOA HAKI KWA WANANCHI,BILA UONEVU WO...
      • UZINDUZI WA OFISI YA MASHTAKA WILAYA YA SERENGETI,...
      • MATUKIO YA PICHA YA UZINDUZI WA OFISI MPYA YA TAIF...
      • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
      • Ukataji wa utepe katika uzinduzi
      • Uzinduzi wa
      • SHERIA
      • Uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya S...
      • Uzinduzi wa ofisi yetu nyingine
      • Ofisi_ya_taifa_ya_mashtaka_tz
      • Uzinduzi wa ofisi ya mashtaka wilaya ya kahama

Recent Posts

MKURUGENZI WA MASHTAKA

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE Contact me .
  • Loading...
  • Loading...
  • Kitengo cha TEHAMA

    Lengo: kutoa utaalamu na huduma kwa matumizi ya TEHAMA ; Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo: (i) Kutekeleza mpango mkakati wa TEHAMA na Serikali Mtandao; (ii) Kuendeleza na kuratibu mifumo TEHAMA kwa kushirikiana na wakala ya serikali mtandao;. (iii) Kuhakikisha kwamba vifaa na programu za TEHAMA zinasimamiwa na kutunzwa (iv) Kuratibu na kutoa msaada katika ununuzi wa programu na vifaa vya TEHAMA; .
Copyright © OFISI YA MASHTAKA
-